CCM mtandao watajuta milele kuruhusu Magufuli awe Rais wa Tanzania

Dah, Etwege mzee wangu, uchambuzi wako nimeusoma kwa umakini sana na kiukweli umechambua mambo mazito ambayo yanatafakarisha. Kuna maeneo umegonga msumari penyewe kabisa.
Kwanza, suala la yeye kuvunja ile dhana ya unyonge wetu liko wazi. Alitupa ule ujasiri kwamba kama taifa tunaweza kusimamia miradi mikubwa kama SGR au lile bwawa la umeme la rasilimali zetu bila kusubiri mpaka wazungu waje kutushika mkono. Hata kwenye siasa, ujio wake uliwanyoosha wengi—ndani ya CCM na upinzani kama akina Mbowe—wote ilibidi wajipange upya maana gia zilibadilika ghafla.

Lakini sasa, mzee wangu Etwege, ili tuwe wakweli kwa nchi yetu, lazima tuangalie na ule upande wa pili ambao mara nyingi huwa hauongelewi sana. Kuna mambo mawili matatu yalienda mrama sana kiuchumi na kisheria:
Kwanza kabisa, ni hili suala la matumizi ya pesa za serikali. Unajua Katiba yetu kwenye Ibara ya 135 na 136 iko wazi sana; Rais sio mmiliki wa fedha za walipakodi. Kazi ya kuidhinisha matumizi ni ya Bunge. Lakini pale tuliona maamuzi mengi ya mabilioni yakifanyika jukwaani kama mtu anayetoa hela mfukoni kwake.
Chukua ule mfano wa elimu bure ya Januari 2016. Uchaguzi uliisha Novemba, Bunge jipya likasimikwa, na kabla hata hawajakaa kupitisha bajeti yoyote ya nyongeza, hela ikaanza kumwagika mashuleni. Ni jambo jema, sawa, lakini kisheria zile hela zilitoka wapi bila kibali cha Bunge? Huo ukiukwaji wa taratibu ulisababisha matumizi mengi kufanyika kiholela nje ya bajeti rasmi ya nchi.

Pili, hii story ya kwamba tulikuwa tunajenga kwa "fedha za ndani kwa asilimia 100" ilikuwa ni maneno ya kisiasa tu ya kufurahisha umati. Ripoti za Benki Kuu (BoT) hazidanganyi. Mwaka 2015 Magufuli anaingia madarakani, deni la taifa lilikuwa kwenye trilioni 35 hivi. Cha kushangaza, mpaka anafariki mapema 2021, lile deni lilikuwa limepaa mpaka kufikia karibu trilioni 70! Yaani ndani ya miaka mitano tu tulikopa kiasi cha deni tulilolundika tangu uhuru. Tulikopa sana mikopo ya kibiashara yenye riba kubwa na tukakausha ukwasi kwenye mabenki ya ndani, kitu kilichoua mzunguko wa hela mtaani na kuumiza wafanyabiashara wetu.

Mwisho kabisa, ni ule upendeleo wa wazi wa kupeleka miradi mikubwa kule Chato ambako hakukuwa na tija yoyote ya kiuchumi. Kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini na kulazimisha mapori ya akiba kuwa Hifadhi ya Burigi-Chato kumegharimu mabilioni ya walipakodi ambayo leo hii yangekuwa yamesaidia sekta za kilimo au afya kwenye mikoa yenye uzalishaji mkubwa. Uzalendo gani huo unaoishia nyumbani kwenu tu?

Kwa hiyo Etwege mzee wangu, ni kweli alitikisa nchi na kutuamsha, lakini ukweli mchungu ni kwamba "muujiza" wake ulitugharimu sana kiuchumi kwa kutuachia madeni makubwa, na ulivunja kabisa misingi ya sheria za nchi yetu. Uzalendo wa kweli hauwezi kupatikana kwa kuvunja Katiba na taratibu tulizojiwekea.
 
Maguf.uli alianzisha uhuni wa kuteka na kupoteza watu
Magufuli alinajisi tume huru ya uchaguzi na kuipendelea CCM kuanzia urais, ubunge, diwani hadi serikali za mitaa
Hapo kabla ya magufuri kulikuwa na time huru mkuu
 
Siyo mbaya, ila kuua hilo halifutiki.
Magufuli ana mikono yenye damu.
Ben Saanane inasemekana alimuua mwenyewe.
Kiongozi akiwa na mikono ya damu, kwanza Mungu hapendi, pili, kama alivyoua naye anapotea kinyemela.
 
Hujagusia utekaji na watu kupotea chini ya Magufuli.
 
Kubwa jinga kazi yako kulamba kende za lumumba
 
watu wanamuona kama Malaika hawajui huyu aliyemfuata kafuata nyayo zake na wanaolalamika walikua washangiliaji wake kama yule Polepole
Anafuata nyayo za kuteka na kuuwa tu alafu nyayo za kujenga flyovers anaacha
 
Kama JPM angeendelea kuwa hai nisingekuwa hata na muda wa kubishana na wakina tilatila na shoga yake mwashambwa labda ningewaunga mkono.

RIP JPM
 
 
kwanini usingetumika ya JK? maana ipo, Kosa ni la nani?
Nyakati; Playbook ya JK iliwezekana kwake kwa sababu upinzani hakuwa na nguvu kama kuanzia 2015.

Mabadiliko ya chama; Jiwe aliibadilisha CCM kutoka chama cha hoja kiasi mpaka chama dola kikamilifu kisichoona haja ya kupambana kwa hoja tena

Upinzani ndani ya chama; Timu jiwe wakina Polepole, Mpina na wengineo walikuwa wanavuruga hesabu

Miscalculation; Playbook ya jiwe ilionekana nafuu, nyepesi na yenye faidi zaidi kama ilivyotumika 2019/2020 bila purukushani zozote kwa hiyo ilionekana inaweza kurudiwa tu tena ikaleta matokeo yaleyale bila matatizo makubwa.
 
Nakubaliana na hoja .
CCM sasa hivi si chama cha siasa, CCM ni idara ya uenezi serikalini.
CCM ina watu toka serikalini,
CCM ina watu wa idara ya usalama
CCM inafadhiliwa na serikali.
Mbaya zaidi, CCM inahodhi serikali.
Hivi majuzi mtu wa serikalini, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora ndg Chacha, amediriki kusema CCM ina vimiliki vyombo vyote vya ulinzi na usalama.

HAPO CCM kama chama ni kwishney.
 
Kama ni kweli basi alibugi big time!. Kwa nini asingewekeza nguvu kubwa kuwaonesha wananchi tena kwa ushahidi namna wapinzani wake wanavyohujumu jitihada zake za kutetea maslahi ya taifa?.

Huyu mtu wenu kumtetea ni kazi sana!
 
Kiuchumi Tanzania iliingia uchumi wa kati enzi ya Magufuli
Muda uli
Kama JPM angeendelea kuwa hai nisingekuwa hata na muda wa kubishana na wakina tilatila na shoga yake mwashambwa labda ningewaunga mkono.

RIP JPM
Umenena vyema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…