CCM na wanaccm, nini kosa la Bashiru? Demokrasia kwenu ni nongwa?

Kazi Yetu Ccm Ni Kuzima Kisemeo Muda Wote Hatuna Mchezo
 
Ndiyo maana nimeseandika kuwa kosa halisahihishwi kwa kurudia kosa.
 
Katiba yetu ya sasa imemfanya Rais na mwenyekiti wa CCM kuwa na nguvu chini kidogo ya mungu, wengine wanauita Urais wa kifalme.

Ndugai angefutwa uanachama na chama chake angepoteza kila kitu, kuanzia ubunge hadi uspika wenyewe, huenda pia kufukuzwa huko kungemkosesha hata mafao na matunzo mengine ya wastaafu.
 
UCHAWA ndani ya NCHI UMEVUNJA REKODI Huyo KATIBU MKUU UVCCM ameamua KUJIPENDEKEZA kwa Mwenyekiti ili ASIONDOLEWE kwenye hiyo NAFASI kwani Uchaguzi upo karibu wa UVCCM TAIFA
 
Naye aliwananga waliokuwa wanamkosoa JPM

Mpatie nafasi siti ya mbele anywe kilevi alichoshiriki kukiandaa
 

Sasa kwa nini hakumuacha huyo Mwenyekiti wa CCM na kundi lake wamfute uanachama tuone kafutwa uanachama wakati anasimamia upande wake?

Ina maana aliogopa kupoteza ubunge kuliko alivyotaka kusimamia upande wake?

Wewe unaona hii ni point ya maana hapa?

Wewe mwananchi unayemtegemea Spika na mbunge akutetee kwa kusimamia principle na wewe unatoa hii sababu ya kuogopa kupoteza ubunge kama sababu muhimu?

Ndipo Watanzania walipofika hapa kiujumla au ni wewe tu?
 
Ndiyo maana nimeseandika kuwa kosa halisahihishwi kwa kurudia kosa.
hapana cha kosa hapo leo akiteuliwa nafasi fulani atayasahau yote na kuanza kuimba sifa kama wenzake.

Ni sawa na ile hadithi ya sungura alipokosa zabibu akasema 'sizitaki mbichi hizi'
 
Imagine unatumia jukwaa la wakulima kuleta nongwa na fitina ,Ni Bora angetumia jukwaa la siasa
 
Hii nchi ikikosa wasema ukweli itakuwa nchi inayoteketea... wapumbafu hawaelewi ndomana watawala wanatuswaga kama ng'ombe!!
 
Zidumu fikra za Mwenyekiti? Au twende na KATIBA MPYA
 
Inawezekana yeye alikuwa tayari lakini vipi kuhusu mke wake ambaye inasemekana ni Mkurugenzi(wa kuteuliwa) mahali fulani?
Hatujui alikuwa anamwambia nini, hatuji watoto wake walikuwa wanamtaka afanye nini. Presha za aina hii sio ndogo katika kamari ya kuonekana shujaa au kupoteza kila kitu.

Tanzania sio kama Marekani, ukishakuwa mwanasiasa bongo fursa ni chache sana nje ya siasa ndio maana sio rahisi kuwa na msimamo usioyumba katika siasa zetu. Huko US wanaotoka kwenye siasa wanazo fursa nyingi sana. Wanakuwa wachumbuzi katika CNN, Fox News, MSNBC, wanaandika vitabu, wanafundisha vyuo, wanaweza kuingia kwenye sekta binafsi wakalipwa vizuri na kuwa na maisha mazuri kuliko hata waliyokuwa nayo katika siasa.

Pia mtu akiondoka federal anaweza kwenda kugombea ugavana, useneta, n.k katika majimbo. Tanzania hali ni tofauti sana, hasa ukiondoka au ukiondolewa serikalini kwa kugombana na mkuu ndio unaweza kuumia zaidi kwa sababu kuna taasisi na sheria nyingi sana zinazoweza kuwa weaponized zikakukoponda kama nyanya. Trump alihisiwa ku weaponize IRS dhidi ya mahasimu wake wa FBI, James Comey na McCabe sasa hivi ime back fire baada ya mnadhimu wake John Kelly kuthibitisha.
 
Sasa hivi husikii tena mtu katekwa
Unaweza usisikie ila haina maana kwamba uhalifu wa kutekena hakuna, kama kipindi hiki panya road wameibuka tena kwa kasi wanapiga watu mapanga na hadi kuuwa ndio itakuwa huo uhalifu wa kutekana? Itakuwa akili mbovu kuaminishana kwamba kabla ya Magufuli kulikuwa hakuna uhalifu wa kutekwa watu.
 
Tuna watu wenye kupigia kelele demokrasia ila wao wenyewe hawaamini katika demokrasia, ulichoeleza hapo ni mfano mmoja wapo.
 
Uzuri wanakosoana ila hawatekani tofauti kabisa na awamu iliyo pita
Wanakosoana wapi mkuu wakati unaona kabisa ukikosoa wanakujia juu hakuna uvumilivu wa kukosoana, hapo wanataka aadhibiwe kisa kakosoa halafu wewe unasema wanakosoana!
 
Haya matendo ya kijinga ya kukataa kusikia kauli zinazokosoa yanafuta zile sifa zote anazosimega shaka kuhusu ccm.

Chama kikongwe lazima kiwe na open arms za public critism sio kuficha mambo. Dunia inapoelekea information hata ukizikalia zitasambaa kwa kasi ya 5g.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…