CCM sasa tunaelewana, Chongolo amekubali mkataba DP World ulikuwa na makosa! Sasa tusonge mbele!

EEEEEeeeeenHHHeeeeeeee!

Nimecheka kwa kicheko cha juu sana niliposoma huo mstari wa kwanza katika hayo uliyoandika hapo, na bado naendelea na kicheko cha chini chini!

Hakuna wakati wowote chini ya Mwalimu Nyerere CCM ilipofikia kwenye kiwango hiki ilichofikia hii ya sasa.
In fact, ile CCM ya "kujisahihisha" iliondoka siku nyingi sana baada ya Azimio la Zanzibar.

Sasa unanishangaza kweli kweli na kukumbuka maneno aliyosema Mwalimu, katika nyakati tofauti kabisa, na chama kilicho tofauti kabisa, kasoro ya jina tuu.

Hiyo unayoiita "TUJISAHIHISHE" ni kiini macho tu,; mbinu inayotumiwa na Mwenyekiti, ambayo sasa kila mtu anaijua vizuri.

KUJISAHIHISHA kwa CCM ni kazi nzito sana na yenye gharama kubwa sana sasa hivi. Kama huko ndani ya chama kuna kundi hili la kutaka kujisahihisha, itabidi wafanye kazi kubwa sana ya ziada. Huko kwenye uongozi wa juu wa chama sioni mtu mwenye sifa za kuongoza kazi ya "KUJISAHIHISHA".
 
Pumbafu wote waliokuja wanautetea huu mkataba
 
Wrong, inaelekea we kijana wa juzi.
Azimio la Arusha 1967.
TANU na Tujisahihishe 1976/77.
Tukijiita ma kada mtuelewe, tena si hawa wa juzi kina Bashite au Nape Nnauye.
 
mangikule
Hapa uliandika madini sana

"Mtu hawezi kwenda nje akafanywa kimtindo akaamua kuuza nchi!"
 
Wrong, inaelekea we kijana wa juzi.
Azimio la Arusha 1967.
TANU na Tujisahihishe 1976/77.
Tujiita ma kada mtuelewe, tena si hawa wa juzi kina Bashite au Nape Nnauye.
Sasa unachobishia hapa ni kipi, tarehe, au maudhui ya maelezo juu ya hali iliyomo ndani ya chama?

Hao akina Nape, Makamba, Bashite ndio wenye chama sasa; na nyuma yao "CHAWA" tele wakifanya kazi zao.
Sitaki kukuhusisha na "Uchawa", lakini inaelekea kuwa unafanya kampeni zile zile wanazofanya makundi hayo maalum.
 
Natamani ma Sa-100 aweanasoma mara kwa mara hapa JF.

Narudia kumwambia, mitego ya kisiasa aliyowekewa imeshaanza kumuumiza kwa kasi ya 5G. Hao anaodhani ni ELITE wa siasa na uongozi nchini hawapo pamoja naye.

Kinachoendelea huku mitaani ni pandikizo la chuki dhidi yake linalofanywa na WANACCM waandamizi.

Akiendelea kuwakumbatia, atakumbuka shuka kumepambazuka
 
Ninabisha wapi mkuu.
Nakuelewesha ili ufahamu wako ukue.
Narudia tena kama hukunielewa.
Sera ya TUJISAHIHISHE ndani ya CCM hsikuanza jana.
Na Chongolo kafanya vizuri kubadilika U-Turn suala la DP World, baada ya CCM kunyooshewa kidole kutaka kuuza nchi.
Alichoongea Chongolo mwezi uliopita na juzi vitu viwili tofauti.
TUJISAHIHISHE.
 
Acha kwenda kwa upepo wewe,hakuna Cha kujisahihisha Wala nini hapa,we kubali tu kuwa mliingia chaka
 
Kwani nimeanza kukufahamu leo, mkuu wangu 'Jidu'?

CCM hii chini ya Samia haina uwezo wa "KUJISAHIHISHA", hili unaweza kulipeleka benki moja kwa moja bila ya hofu ya kujiumauma ulimi.
 
Wapeni pongezi wapinzani

Tatizo mkuu unadandia treni kwa mbele na husomi ili kuwa na hoja.
Soma mchango wangu nikikinanga chama changu kwa maamuzi ya DP World.
 
Ndio vijana "wale" wako kwenye mchakato wa kuurekebisha uwe na tarehe ya kuexpire na marekebisho au kifungu cha kuweza kuutengua endapo watashindwa kukidhi vigezo na masharti watakao wekewa
 
Kwani nimeanza kukufahamu leo, mkuu wangu 'Jidu'?

CCM hii chini ya Samia haina uwezo wa "KUJISAHIHISHA", hili unaweza kulipeleka benki moja kwa moja bila ya hofu ya kujiumauma ulimi.
Unajishushia hadhi mkuu, una jina hapa JF.
Sasa hii U-Turn ya Chongolo, kama si kujisahihisha, basi tuambie ni nini!
 
Unajishushia hadhi mkuu, una jina hapa JF.
Sasa hii U-Turn ya Chongolo, kama si kujisahihisha, basi tuambie ni nini!
Husomi ninayojibishana nawe hapa?

Mbona nimekwishajibu hili swali hapo juu, #81, au unataka jibu la namna gani?

Usijali sana juu ya mimi kujishushia hadhi inapohusu maslahi ya Tanzania na CCM ilikotufikisha; niko radhii kabisa nipoteze kila kitu juu ya hilo.
 
Dhamira ya mkataba haikuwa nzuri na hilo lipo wazi,
Kulekebisha ili kuendelea na muwekezaji huyo huyo si jambo zuri pia,
Mkataba usiwepo kabisaaa kama ni muwekezaji awe mwingine..
TPA inatosha Atafutwe Msimamiaji tu! Na Sio Mwekezaji
 
Usomi wa Tulia ni ulizo kuu la dunia hii na kwangu mimi alitakiwa anyongwe kwa ujinga wake kwa mkataba huu bungeni
 
Ni jambo jema

Marekebisho ni hadi DP World wakubali

Wayahudi wakamwambia Pilato " Usiandike Mfalme wa Wayahudi bali andika Huyu alijifanya Mfalme wa Wayahudi"

Pontio Pilato akawaambia " Niliyoandika Nimeyaandika'
CCM wameingiza Nchi (Bandari) ktk mdomo wa Mamba (Mwarabu)....hakika hpa mpaka Dp Wedi akubali.


Tumeliwa Twafwaaaa....,[emoji31]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…