EEEEEeeeeenHHHeeeeeeee!Mkuu sera za CCM toka miaka ya Mwalimu ni Tujisahihishe.
CCM kupitia Katibu Mkuu wake imefanya vizuri kukubali mapungufu katika mkataba wa DP World.
Huo si udhaifu, na nyuma yake lazima kulikuwa na malumbano mazito, lakini CCM imetoka na msimamo mmoja, TUJISAHIHISHE.
Nimecheka kwa kicheko cha juu sana niliposoma huo mstari wa kwanza katika hayo uliyoandika hapo, na bado naendelea na kicheko cha chini chini!
Hakuna wakati wowote chini ya Mwalimu Nyerere CCM ilipofikia kwenye kiwango hiki ilichofikia hii ya sasa.
In fact, ile CCM ya "kujisahihisha" iliondoka siku nyingi sana baada ya Azimio la Zanzibar.
Sasa unanishangaza kweli kweli na kukumbuka maneno aliyosema Mwalimu, katika nyakati tofauti kabisa, na chama kilicho tofauti kabisa, kasoro ya jina tuu.
Hiyo unayoiita "TUJISAHIHISHE" ni kiini macho tu,; mbinu inayotumiwa na Mwenyekiti, ambayo sasa kila mtu anaijua vizuri.
KUJISAHIHISHA kwa CCM ni kazi nzito sana na yenye gharama kubwa sana sasa hivi. Kama huko ndani ya chama kuna kundi hili la kutaka kujisahihisha, itabidi wafanye kazi kubwa sana ya ziada. Huko kwenye uongozi wa juu wa chama sioni mtu mwenye sifa za kuongoza kazi ya "KUJISAHIHISHA".