Hawezi kufutwa ubunge, kwasababu Gwajima ni jeuri kuliko Mwenyekiti wa CCM na pia ametumwa na hao hao CCM kumtingisha Rais SSH ili wamweke kwenye tisini asigombee 2025.
Kifupi, Gwajima anatimiza agizo la wana CCM wenye uchu wa madaraka ya urais (Mwigulu Nchemba & Co Ltd In Collaboration With Sukuma Gang) kumfanyia hujuma, figisu na fitina Rais SSH.
Simple logical theory wanayotumia Mwigulu Nchemba & Co Ltd; Rais SSH anatakiwa atingishwe kisawasawa,
1) Afitinishwe na wananchi kwa kupandisha kodi/tozo kwa wanyonge (Miamala Ya Simu, Wakulima, Wavuvi). Hapa ametumika Mwigulu Nchemba.
2) Afitinishwe na vyombo vya Usalama. Hapa ametumika Gwajima.
3) Afitinishwe na dunia nzima kwa kuwapa viongozi wa upinzani kesi za Ugaidi. Hapa vimetumika vyombo vya Police.
4) Akose kuungwa mkono na CCM wenyewe ndani kwa ndani kwa kuona hana msimamo thabit. Hapa itatumika CCM yenyewe kwenye vikao vya NEC taif.
Rais SSH cha ajabu bado hajaona sinema hii, akiendelea kuwalea hao viumbe hachomoki kwenye kikaango cha CCM wenye uchu wa madaraka, ndio kwanza 2021 mpaka 2025 ni mwendo masafa marefu na Rais SSH ajiandae kwa kuvaa viatu vizuri tu.