SIO kweli mkuu.
Kaskazini inachangia pato kubwa sana kupitia Utalii na wafanyabiashara wakubwa.
Mpaka leo Kaskazini na Tanga ni eneo linaloweza kuwa nchi na lisitegemee mkoa Mwingine wowote.
Shule na Taasisi za Binafsi Kwa ukanda Huo zilianza Kwa kiwango kikubwa zilikengwa na Wananchi wenyewe Kwa nguvu zao.
Hivi Sehemu yenye wasomi wengi kama Ukererewe inapokosa maendeleo utasemaje kuwa rasilimali zao zimepelekwa kaskazini kama SIO ukichaa na upunguani.
Madini ya dhahabu Kwa ukanda Wa Maziwa makuu yameanza kuchimbwa na wawekezaji miaka ya 2000. Nyuma ya Hapo mgodi ulikua mmoja tu Wa Williamson kule Mwadui. Amboa kimsingi huwezi kulinganisha na pato la watalii na mabepari waliokuwa wanamiliki mashamba ya shayiri ,ngano,maharagwe,ngano ,mkonge na Tanzanite , migodi mikubwa kule kararani Tanga ambayo Nyerere aliifunga Kwa kuogopa mzungu aliyeiweka nchi mfukoni kwake. Mgodi uliokufa mpaka leo. Tanga Ina Vito vingi sana Vya thamani,Tanga ndiyo manuspaa ya kwanza Tanzania ,ikiwa na viwanda vingi sana Lakini vilihujumiwa na kufa na kuwaacha wazawa wakiwa maskini. Arusha na Kilimanjaro palikua na mabilionea tangu ukoloni wakanyanganywa Mali zao na Nyerere na pia MAGUFULI.
Hakuna msukuma aliyenyanganywa n'gombe na kufanywa za Taifa ila watu Wa kaskazini walinyanganywa Mali na majumba na mashamba na kuwa ya umma na kufilisiwa.