Unajua baada ya kufariki magufuli kosa kubwa Sana lilifanyika ndani ya ccm wenyewe kwa kuanzisha mashambulizi ya wazi kabisa kwenye media kwa kumtukana magufuli,kubagadha, kumkejeli marehemu,Mara eti wazuri hawafi na kuanzisha majina ya ajabu eti SUKUMA GANG,hadharani bila ya ccm kukemeana wenyewe ndani ya chama Mambo haya yaliwauma mno wasukuma,Sasa matusi na kejeli hizo ziliwaamsha Sana wasukuma na kuwaleta pamoja,matusi na slogani hizo zilijidhihirisha zaidi pale alipofariki membe ,ambapo nao walikejeli "kumbe na wazuri nao wanakufa!" Haijachukua muda Sasa mnataka kura zao mnafanyaje,wahenga walinena mchimba kisima huingia mwenyewe,Mimi niseme ni ushamba wa siasa za ccm wa kuropoka matusi mazito Kama hayo bila kupima athari zake mbeleni,Ina maana chama na serikali vilikosa watu wenye busara wa kuonya na kukemea kuwa Mambo hayo ya kutukana marehemu Yana impact Hadi kwa chama na serikali mbeleni???? CCM wamelichonga dude hili la ukanda lazima liwatafune Sana,hasa akitokea mpinzani mwenye influence Kama alivyokuwa lowasa itakuwa ni hatari hasa kwa ccm