CCM wamenasa kwenye mtego wa Wasukuma, hawatoki tena

Watanzania wanataka kiongozi mwenye falsafa ya magufuli!!!!!!!! kumbe! baaaaaaaasi mnaotaka uongozi anze kuigiza falsafa hiyo kazi kwenu
 
Mkuu kavulata , usemayo ni kweli kabisa, Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!
Hivyo Kanda ya Ziwa ndio kanda determinant kwa urais wa JMT na ndipo roho ya CCM ilipolalia!. Ikitokea CCM ikachokwa Kanda ya Ziwa kama Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi! then huu mbuyu chali!.

Kufuatia umuhimu wa Kanda hii, JPM aliipatia preferential treatment kama Pongezi kwa Rais Magufuli kusitisha Bomoa Bomoa kwa kuongeza kigezo cha "Human Face". He's so Human!
na Naunga mkono Uwanja wa Ndege wa Chato. Una justification, utakuwa kama Ggabolite au Yamoussoukro. Watalii watamiminika!

Ila pia Wasukuma ni wachapa kazi na majembe kazi ya ukweli Kiukweli nimeguswa sana na uchapakazi wa Rais Magufuli!. Je, kuna uhusiano kati ya kabila la mtu, na uchapakazi wake?. Je, 2020 kuna haja ya... just imagine usiku watu huwa wako bize na yale ya usiku, Mwamba yule yuko na ma file mpaka chumbani!.

Wasukuma Oyeee!.
P
 
Hoja zenye mtazamo wa ukabila na ukanda siyo za wakati huu.
Huwezi kuwatenganisha wasukuma na makabila mengine wakiwepo wachaga, hivyo habari za ukanda wa ziwa na ukaskazini ni ujinga wa kisiasa kwa ajili ya wabinafsi wachache kutumia ujinga wa wananchi kuwaghilibu.
Maendeleo ya kweli yatatokana na wananchi wenyewe kwa kuhakikisha rasilimali na jasho lao vinagawanywa kwa haki na siyo ubinafsi na ufisadi wa viongozi kulimbikiza mapato ya taifa nyumbani kwao.
Wasukuma kwa asili ni wachapakazi, siyo wabinafsi wala roho mbaya na uovu kama wanasiasa wachache waovu na wakatili wanavyotaka kuaminisha jamii na taifa.
 

1. Hakuna kabila jamii au kanda iliyopendelewa na mkoloni.

2. Mkoloni alijenga miundombinu kwenda ktk maeneo mbalimbali ili kufuata RASILIMALI na sio kwasababu aliyapenda makabila ya maeneo hayo.

3. Dhana kwamba kabila fulani jamii au kanda iliyopendelewa sio sahihi. Kila jamii hapa nchini ilinyonywa na kunyanyaswa na wakoloni.

4. Maeneo mengine ukiacha kanda ya ziwa nayo yana utajiri wa rasilimali, mazao ya biashara, ardhi yenye rutuba, na watu wanaochapa kazi.

Kwa mfano kanda ya kaskazini kuna KAHAWA ambayo kwa miongo kadhaa ilikuwa na bei kubwa ktk soko la kimataifa na zao tegemewa kwa kuiingizia hazina yetu mapato. Pia kuna utalii, na madini, mfano Tanzanite.

5. Wamisionari walijenga mashule ili waweze kuwabadili wenyeji kiimani. Huo haikuwa upendeleo bali ni hila ya kuzitawala na kuzinyonya jamii hizo. Sio sahihi kusema jamii au kanda fulani hapa Tanganyika ilipendelewa na wakoloni.

6. Serikali ya baada ya uhuru ilikandamiza maeneo yote hakuna jamii iliyoachwa salama. Kwa mfano, VYAMA VYA USHIRIKA vilivunjwa nchi nzima. Nyanza cooperative ilipovunjwa, vyama vingine vya ushirika navyo vilivunjwa nchi nzima

7. Tatizo la kanda ya ziwa ni kuwa na viongozi WABINAFSI wasiosimamia maslahi ya wananchi wao.

8. Jamii mbalimbali hapa nchini zinapaswa kuiga mfano mzuri wa WAKINGA. Ni namna gani Wakinga wamepats maendeleo makubwa bila kutegemea au kulilia kubebwa na wakubwa serikalini.
 
Unajichanganya
 
Watapambana na Tribal Profiling ambayo imenyamazisha Wajaluo Kenya na Tz na pia Hutu na Twa Rwanda na sasa Acholi Uganda.

Ila Wasukuma, Maasai na Datooga wana mkakati wa hatari sana ambao wasomi wameshindwa kuudhibiti; wa kusambaa kila kona ya Jamhuri.

Huko wanakwepa intermarriage wana maintain purity kwa kuoa makabila yao tu kama Boers, Wadachi, Wayahudi, Wahindi, Wachina wanavyofanya.

Wakija kufikia akidi wataendesha na kuamua mustakabali wa nchi jinsi watakavyo hata kama watakuwa hawana rais na elimu.

Naona akili za kifugaji zinaenda kudhibiti akili kubwa za wasomi e.g. Wachaga, Wapare, Wanyakyusa, Wahaya, Wajaluo and sundries.

Asomaye na afahamu maneno ya unabii huu.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
8. Jamii mbalimbali hapa nchini zinapaswa kuiga mfano mzuri wa WAKINGA. Ni namna gani Wakinga wamepats maendeleo makubwa bila kutegemea au kulilia kubebwa na wakubwa serikalini.
Wakinga wanapata maendeleo kwa kutumia kinga!.
Wambeya ni ajili ya umbea!.
Wahaya ni kwa kukosa haya!.
Wachagga wamepata maendeleo kwa ku chaga!.
Wasukuma wao ni wanasukuma tuu!.
Wasambaa wanasambaa!
Wapare wana pare!
Waarusha wana rusha!
Wamakonde wana konde!.
Wasandawe wana sanda!
Wanyiramba wana ramba!
Wanyaturu wana turu!
Wanyamwezi wana mwezi!.
Wagogo wana gogo!
Wahangaza wana angaza!
etc.
P
 
Utajiri mkubwa kuliko wote ni wananchi wenye uelewa na akili nzuri.
Hata hivyo, hii ni hatari kwa wanasiasa wetu, ambao hutegemea ujinga wa wananchi kama mtaji wao.
Msingi wa umasikini wa Afrika umejengeka kwenye ujinga wa wananchi walio wengi, na unaendelea kuimarishwa na wanasiasa wanaotumia umasikini huo kama mtaji wao.
Wanasiasa wengi ni wajinga pia, kwa sababu wanatokana na wananchi wajinga na hivyo kusababisha ujinga wa halaiki.
 
Aise umeamua kuongea ukweli uliojificha muda mrefu πŸ˜† πŸ˜†
 
Wasukuma kosa lao lilikuwa ni kuzubaa

Labda wachangamke huko mbeleni
 
Msijidanganye, ccm mkigoma kuwapigia, wao watapiga kwa niaba yenu...bao la mkono
 
Kuwaita sukuma gang kunawaunganisha zaidi na kuwafanya wajione wana jukumu la kumuunga mkono sukuma gang mwenzao regardless anafaa au hafai. Suluhisho la hili ni kuacha kugeneralize matendo ya mtu mmoja mmoja na kabila.
 
Nimependa tu hiyo no. 7.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Zile siasa za kishamba za dhalimu lazima zitaendelea kuwa ni athari hasi, na alikuwa anafumbiwa macho. Niliwahi kusema anaweza kuua upinzani kinyume kabisa na utashi wa wananchi, lakini kutaanza kujitokeza upinzani usio na afya wa kikabila. Na sasa tunaelekea huko kwa kasi. Ngoja tuone hatima yake.
 
Wewe ni mkabila wahed.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…