Walnut Creek
JF-Expert Member
- Mar 17, 2009
- 5,830
- 6,315
Siyo kıla mtu ana kipawa cha uongozi, jambo ambalo CCM na wapinzani wengine hawataki kuelewa.Kwanini hauwi kiongozi ili tupate kiongozi mwenye "maono"?
Akili kubwa vs Akili ndogoWamedhamiria kuuza bandari zetu. Najua kamati hiyo ya CCM walio wengi hawaafiki, wanaogopa na kutetea matumbo yao.
Suluhisho pekee ni nguvu ya wananchi. Tunafanyaje ? Mapendekezo:
1. Waandikie DP World na dunia nzima kwa ujumla kuwa watanzania wamekataa upuuzi wao, na hawatakaribishwa.
2. Watakutana na physical confrontation
3. Polisi na majeshi nanyi teteeni nchi yenu Tanganyika na vizazi vyenu vijavyo. Msikubali kuwaumiza watanganyika kwa faida ya wazazibari na matumbo ya watu wachache.
😆😆😆toto limekua kubwa na zito, bado linadeka halitaki kuteremka mgongoni
Ndio utaelewa kwanini wanaofanya vibaya darasani wasio na akili kabisa ndio wanachukuliwa na watawala wakatumike kwenye majeshi na vyombo vya usalama kama majibwa ya kuwalinda watawala3. Polisi na majeshi nanyi teteeni nchi yenu Tanganyika na vizazi vyenu vijavyo. Msikubali kuwaumiza watanganyika kwa faida ya wazazibari na matumbo ya watu wachache.
Itafika siku mbaya adui watafika, watashambulia mwili hata roho, laiti ungelijua amaniLuka 19:41-42
Alipofika karibu aliuona mji akaulilia alisema Laiti ungelijua yapasayo Laiti ungelijua Amani!
Hoja hujibiwa kwa hojaInauma lakini maendeleo inabidi yafanyike.
Pole sana.
Kama hauna "kipawa" cha uongozi utaujuwaje "uongozi" mpaka uweze kusema wenzako hawawezi?Siyo kıla mtu ana kipawa cha uongozi, jambo ambalo CCM na wapinzani wengine hawataki kuelewa.
Hulka yangu ni biashara na kutembea dunia siyo kubeba majukumu ya kulinda, kutetea na kuwasaidia wananchi.
Hoja ipi unaiongelea?Hoja hujibiwa kwa hoja
Hizo trillion ni ngapi? Ina maana kila mwaka bandari itakuwa inauzwa? Sijitoi ufahamu ni kwamba hueleweki au huo mkataba hujauona unatupigia tu kelele hapa?Unajitoa ufahamu sio??? jumlisha hizo trillions zitakazoingia kila mwaka kwa muda usiojulikana, wewe vipi???
Mimi sijaona huo mkataba wenye hela ndio nimeomba hapa mniambie nyie mliouna umeandikwa shilingi ngapi?Kwani mkataba uliosainiwa na serikali unasemaje tutapata shilingi ngapi?.
Acha matusi hizi ni dalili za kushindwa hoja mbona unataka kuwa kama Tundu LissuOna hili senge
Uliwakopesha sh. Ngapi bwasheee?Kikwete na Samia rudisheni pesa zangu.
Hawajaenda shule.Mnadai kuwa tupewe elimu. Juu ya nini? Walichochambua wanazuoni mlitakiwa mkijibu kisheria sio kutoa majibu ya juu juu tu.View attachment 2683517
Kweli chama hichi ni chama cha majambaziHamashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana katika kikao chake cha kawaida makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo Jumapili, Julai 9, 2023, chini ya Uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine imejadili mkabata wa makubaliano ya uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.
Mkataba huo ni baina ya Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya Dubai Port World ambao tayari Bunge la Tanzania limeridhia ushirikiano huo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amewaambia waandishi wa habari kuwa, Halmashauri Kuu imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari na kuazimia ifuatavyo; uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.
Uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, ibara ya 59, ukurasa wa 92. Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari,” amesema Mjema.
=====
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai wakibariki mchakato huo.
Katika kikao chake kilichoketi makao makuu ya CCM, jijini Dodoma leo Jumapili Julai 9, 2023 chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kikao hicho kimesema uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.
Taarifa fupi iliyosomwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema mbele ya waandishi wa habari ilesema uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, Ibara ya 59, ukurasa wa 92.
Hata hivyo, Mjema amesema kikao kimekubaliana kuwa, Serikali iendelee kutoa elimu kwa kwa wananchi katika jambo hilo.
"Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari," amesema Mjema.
Halmashauri hiyo ilifanyika baada ya kutanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ambapo pia imezipongeza Serikali zote mbili za Chama Cha Mapinduzi, Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.
Katika mkutano huo na waandishi, Mjema amesema siyo siku ya kujibu maswali kwani yeye amesoma kile ambacho wamekubaliana na Halmashauri na mambo mengine yasubiri wakati wake.
Pia soma: Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World
DOKEZO - Malalamiko ya mkataba wa DP World yapelekwe CCM, Rais Samia hana makosa sababu anatekeleza sera za chama chake
Hili ni sikio la kufa.Mnadai kuwa tupewe elimu. Juu ya nini? Walichochambua wanazuoni mlitakiwa mkijibu kisheria sio kutoa majibu ya juu juu tu.View attachment 2683517
Maswali ya hovyoHoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?