CDC Africa: Vipimo vya Corona Virus vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vizuri


Hii mbaya mazee especially coming from you. Hakuna madaktari ambao ni TISS? Au unajuaje kwenye hiyo hiyo maabara hakuna informants wa TISS??


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hiyo tume ikiwa Kama bunge watatia mguu wenye.hapo tutegemee waliosimamishwa na wengine wawe kafala,hatuwezi kusema mtambo feki maana wenye brand pia watatua kutuumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pimbi kaumbuka kweli kwa uongo wake wa mchana kweupe kitu Cha njombe noma.
 
Return Of Undertaker,

Kama kuna taasisi ambayo ni dhaifu sana kwenye kusimamia PanAfricanism ni AU.

Bahati mbaya wengi wa viongozi AU ni waoga hasa kama wametoka makoloni ya Ufaransa.

Huyu mkuu wa CDC Africa, Dr. John Nkengasong ni raia wa Cameroun; sote tunakumbuka Cameroun ilikuwa koloni la Ufaransa.

Kuna syndicate pale AU jambo likitoka kwa Anglophone lazima Francphone walipige chini. JPM angetoa Francphone, si ajabu wangeunga mkono kwa haraka.

Mwaka jana 2019 Dr. Arikana Chihombori-Quao akiwa Balozi wa AU Marekani, AU Commission chini ya Mkiti wake raia wa Chad (nae ni Francphone) Moussa Faki Mahamat walimtimua kazi Dr. Arakana kwa sababu ambazo hazina mashiko sana kwa maslahi ya Afrika.

Kiufupi, AU ni teethless dog na ina watu ambao wako so corrupt.


JPM kaja na scientific proof kuthibitisha udhaifu wa equipments ambazo China katengeneza. Ni nchi nyingi kit za kupimia zilikuwa zinaonesha kutokuwa accurate. Kitendo cha kuonesha majibu yenye udhaifu hata kwa mbuzi au papaya kuwa na Corona; huo ni ushindi mkubwa ambao hata ngozi nyeupe hawakuwa na majibu.

JPM is such a confident leader to challenge the norms.
 
Yaan watanzania bhana, ulitegemea kila nchi au chombo kitasupport hii issue??...kumbuka Ethiopia ndo alikuwa supplier wa hivi vifaa, unategea atakubali kuchafuliwa kuwa alikuwa supplier wa vifaa fake?, reputation yake ingekuwa destroyed, assume ndo ingekuwa MSD ndo amepata hii tenda ya kussuply unafikiri angekubali tu achafuliwe??.

Kuna baadhi ya vitu sio vya kushangilia, hili sio la JPM bali ni la kwetu wote, Nchi nyingi zimelalamikia hili swala la vifaa ila kwa Tanzania ndo imekuwa Nchi ya kwanza Afrika kutoka hadharan na kusema ukweli huu ili wananchi wake wapate kuelewa na kupata ahueni.

JPM amefanya hichi kwa ajili yetu na familia zetu, kuna vitu vya kushangilia na kumdhihaki ila kwa hili HAPANA.




Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Virusi vya corona: Vipimo vinavyotumika kupima corona Tanzania havina hitilafu

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (CDC) kimesema kwamba vifaa vya kupimia virusi vya corona nchini Tanzania havina shida yeyote. Leo Alhamisi, Mkuu wa Afrika CDC amewaambia waandishi wa habari kuwa ofisi yake inavijua vilivyo vipimo hivyo.

"Vipimo ambavyo Tanzania inatumia tunajua kwamba vinafanyakazi vizuri," Dkt. John Nkengasong amesema hivyo katika mkutano na wanahabari wa njia ya mtandao.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Africa CDC, inapingana na kauli ya rais wa Tanzania ambaye alisema huenda vipimo hivyo vikawa na matatizo.

Kituo hicho cha Africa CDC pamoja na wakfu wa Jack Ma, Shirika la msaada la bilionea wa China, lilisambaza vifaa hivyo, Nkengasong amesema na kuongeza kwamba vilidhinishwa na wanachojua ni kwamba vinafanya vizuri.

Kituo hicho kiko chini ya Umoja wa Afrika kina majukumu ya kuratibu mapambano dhidi ya mlipuko wa mangonjwa barani Afrika.

WHO inasema nini?
Kwa upande wake Shirika la Afya Duniani kupitia Mkuu wake wa bara la Afrika Dkt Matshidiso Moeti limesema halikubaliani na kauli ya Rais Magufuli kuwa vifaa vya kufanyia vipimo vya corona vina maambukizi ya virusi.

''Tunaamini kwamba vifaa vya kufanyia vipimo vilivyotolewa vinazingatia ubora wa kimataifa na zimenunuliwa kupitia WHO na zile zilizotolewa kama msaada na WHO Jack Ma hazijaingiwa na virusi'' alisema Dkt. Moeti

Aliongeza kusema, '' Samahani sikubaliani na kauli ya [Rais wa Tanzania] kwamba vifaa vya kufanyia vipimo vilivyopo vina maambukizi ya virusi. Kwa kweli hatukubaliani na kauli hiyo.Rais Magufuli atilia mashaka ufanisi wa maabara, uchunguzi kufanyika.

Siku ya Jumapili, rais Magufuli alikihutubia taifa alitilia mashaka ufanisi wa vifaa vya kupima corona katika maabara kuu ya nchi hiyo.

Magufuli alieleza kuwa aliagiza sampuli za Wanyama na matunda kupewa majina ya binadamu na umri kisha kupelekwa ili zipimwe bila wataalamu wa maabara hiyo kujua na matokeo yakarudi kuwa baadhi ya sampuli hizo zimekutwa na maambukizi ya corona.

"…Lazima ugundue kuna mambo ya ajabu yanafanyika nchi hii. Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, ama hawana utaalamu jambo ambalo si kweli kwa kuwa maabara hii imetumika sana katika magonjwa mengine. Ama zile sampuli zinazoletwa maana vifaa vyote vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa," alisema Magufuli.

Magufuli amesema kutokana na taarifa hizo anaamini kuna watu ambao walipewa majibu yasiyo sahihi.

"Lazima kuna watu wameambiwa positive lakini si wagonjwa wa corona, na inawezekana wengine wakafa kwa hofu."

Jambo hili linaweza kuwa ni moja ya sababu kuu ya kutotolewa kwa takwimu mpya kufikia sasa.


My Take
Hii ni aibu tunavuna baada ya Rais kukimbilia kwenye media wakati wangeweza kufanya consultation na wataalamu wakajiridhisha na kuja na hitimisho lisilo na shaka. Kwenye orodha ya wanaopata aibu mnitoe
 
Wredawazimu tu hao kwani wao ndio walivipokea hivyo vifaa? Wanavijuaaje kama bora au la? Wajinga hao
Utadhani wao ndiyo walivitengeneza. Hivi vifaa vyetu havijulikani hata aina yake wao wanasemaje kwamba havifai??
 
Punguzeni ujinga..sina chama lakini haakuna Rais makini Afrika hii kama JPM, tumieni akili zenu kufikiri badala ya kubeba maneno ya washenzi walio karibisha mkono wa mkaburu ndani yao
JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…