Chad: Rais Idriss Déby afariki dunia saa chache baada ya kutangazwa mshindi wa Urais kwa muhula wa sita

Chad: Rais Idriss Déby afariki dunia saa chache baada ya kutangazwa mshindi wa Urais kwa muhula wa sita

Hakuna hiyo siku. Huo ndio ukweli mchungu.
Madikteta wanazidi kuongezeka duniani.
Marekani iliponea chupuchupu kutumbukia kwenye udikteta mwaka huu.
Ila kwakuwa kifo kipo basi uhuru hautakoma
 
Afrika hapa shida sana, wewe umekaa mihula 5..si uacheee..kama miaka 30 umetawala hujaridhika na hujabadili kitu miaka 5 inatosha nini??
Hii ni hulka aliyonayo mwanadamu,hata siku ya kufa mtu muovu ataomba angalau apate dakika chache angalau akatoe swadaqa ingawaje ameishi duniani miaka 30 lakin hamkufanya hilo!
 
Madikteta wameamua kwenda frontline kwenye vita, na wanaishia huko.

Mzee na uzee wake akajitia u Van Damme badala ya kutoa hotuba ya ushindi baada ya kuulawiti uchaguzi. Si ajabu hiyo ni assassination. Wadau walimchoka kwa kuwasotesha msituni kwa manufaa yake.

Jiwe naye aliamua kujiweka frontline kwenye vita ya corona aliyoiita vita ya kiuchumi. Mwanzo alionekana kuishinda ikaenda kujipanga, ilivyorudi hajachukua raundi.

Mungu kaamua mapinduzi mwenyewe kunusuru watu wake, anawachanganya madikteta wanajipeleka wenyewe midomoni mwa chatu. Halafu lawama zote kwa mabeberu.

Salamu kwa madikteta wote waliobaki.
 
God is helping Afrika, by killing dictators. And what I fore see this will continue.enough is enough.
 
Rais wa Chad Iddriss Deby ambaye amekuwa madarakani kwa takriban miaka 30 toka aingie madarakani mwaka 1990, ambaye jana usiku alitangazwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kwa kushinda uchaguzi kwa awamu ya sita ameuawa.

Taarifa zinasema alikwenda kwenye battle ground kuwatembelea wanajeshi, na kupigwa risasi na waasi.
 
Habari za kifo chake haziko wazi, ila ni kama amekufa kwa majeraha ya risasi, na mtoto wake anayejulikana kwa jina la Kaka ametangazwa kuwa rais wa mpito.
Hyo mtoto wake nae inabidi wapite nae coz ataleta utawala ule ule wa kishenzi wa mshua wake.
 
Mwanae kapewa Urais wa mpito!!

Africa ni Africa tu naye wahesabu miaka 30 mingine
Jeshi ndio linaongoza nchi kupitia baraza la kijeshi katika kipindi hiki cha mpito cha miezi 18, otherwise useme mkuu wa baraza la lijeshi ni mwanae vinginevyo acha upotoshaji.
 
Ngoja nione umati utaojitokeza kumuaga kisha nifanye comparison.

Pia nataka nione namna legacy yake itavyojailiwa.
 
Raisi anakufaje kwenye uwanja wa vita? Kwani alikuwa frontline? Nahisi wanajeshi wake walimchoka na wamemuua.
 
Nakwambia mwaka huu Mungu hatanii.

Wewe ukijifanya tu jeuri, kibri, mjivuni, mjuvi, mpenda sifa, mbabe (sio m-mbabe, there's a difference).... kichwa kinaliwa!

Kuna kichwa kililiwa mwezi March nimesahau jina lake, lakini kuna kichwa kingine jeuri (Mourinho) kimeliwa hapa jana tu dadeki.
 
Back
Top Bottom