#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

Hivi CHADEMA wanaelewa kwamba kabla ya chanjo kuna fomu ya kusaini kukubali kuchanjwa?

Wanaelewa kwamba kuna issue nzima ya consent katika maadili ya kitabibu?

Wanaelewa kwamba kulazimisha watu wasiotaka chanjo wachanjwe ni kuvunja haki zao za kibinadamu?

Hawana ajenda kwa sasa, wanarukia kila kitu! Ajenda yao ya ufisadi waliipoteza 2015! Kwa sasa wamebaki kushikilia katiba mpya ambayo kwa 90% ya watanzania haina mashiko, ina mashiko kwa wasomi wachache
 
Chanjo za COVID19 ni jambo la hiari duniani kote. Serikali haiwezi lazimisha wananchi kuchomwa chanjo kama hawataki. Wakifanya hivyo watakuwa wanakiuka na kuvunja haki za binadamu na dunia nzima itawageukia. Huyu ni mshauri mbaya na haufai.
 
Nchi hii kuna ufala mwingi sana, ukichunguza vizuri wanaopinga chanjo chanzo ni Gwajima alipoanza kuipinga mwaka jana, mbona chanjo zote tulizochanjwa ni za wazungu?

Kwanini tusiachane nazo?

Hebu pingeni chanjo kwa hoja za kisayansi ili tuwaunge mkono basi?
Hakuna aliyekukataza kuchanja, wewe chanja ila sisi wengine hatuchanji ng'o.

Kila mtu ana maamuzi yake tuheshimiane.
 
Hii habari ya kulazimisha watu wote wapatiwe chanjo ya corona imemweka mbowe ktk mazingira magumu sana. Katiba kwa sasa haijadiliwi, kinachojadiliwa sasa ni kauli yake ambayo imeleta taharuki kubwa kwa watanzania.
Kaenda Mwanza kwa mbwembwe then kapiga bonge la boko! Kasahaulisha watu tozo
 
Hawana ajenda kwa sasa, wanarukia kila kitu! Ajenda yao ya ufisadi waliipoteza 2015! Kwa sasa wamebaki kushikilia katiba mpya ambayo kwa 90% ya watanzania haina mashiko, ina mashiko kwa wasomi wachache
Tuangalie wenzetu waliotutangulia katika demokrasia wanasemaje, naangalia demokrasia kwa sababu CHADEMA ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Demokrasia ipo katika jina la chama.

Mimi nakaa Marekani kuna demokrasia mpaka inakuwa fujo.

Katika majimbo yote 50 ya Marekani hakuna jimbo linalolazimisha chanjo.Yani wanaweza kukubana ukitaka kufanya kazi hii ni lazima upigwe chanjo, ukitaka kusoma shule hapa ni lazima upigwe chanjo. Hivi vitu vilikuwepo kabla ya Covid.Mimi nilivyosoma chuo hapa ilikuwa huwezi kuanza chuo kabla ya kuonesha ushahidi wa chanjo ya MMR (Measles,Mumps and Rubella). Lakini hakuna sehemu serikali ya Federal au State wanaposema ni lazima watu wote wapigwe chanjo.

Na siku serikali itakapolazimisha chanjo ndipo baadhi ya watu watu watachukua bunduki zao kuingia mtaani kuandamana.

Mimi napenda chanjo, nimechanja chanjo zote mbili za Pfizer, naona watu wanaokataa chanjo kuwa ni tatizo kubwa sana, kwa sababu wao ndio wanaosababisha mlipuko wa ugonjwa uendelee. Sasa hivi Marekani watu wanaolazwa mahospitalini kwa Covid na wanaokufa karibu wote ni wale waliokataa chanjo. 9 Covid deaths out of 10 in the US are for people who are unvaccinated.

See here
Lakini sitaki waingiliwe katika haki yao ya kukataa chanjo.

In fact hiyo inaweza kuwa a special case ya Darwinian evolution kuua watu wajinga na kuacha dunia iendelee na watu wenye maarifa.

Sasa mimi siku zote nimekuwa natetea haki binafsi za watu, kama mtu kachoka maisha anataka kufa kifo cha "suicide by Covid" mimi nina haki gani ya kumkatalia?

NPR wameripoti kwamba sasa hivi Marekani vifo vya Covid vinaongezeka, na 90% ya wanaokufa ni watu waliokataa chanjo.

Sasa mtu akitaka kufa mwenyewe mimi ni nani nimkatalie?

 
Huyu jamaa atakuwa ana matatizo ya akili ama ameshushia ile soda yake ya faru john.
 
Chanjo zote duniani hi hiari. Umewahi kuona wapi watu wanalazimishwa tiba? Kwenye medical ethics tunaongozwa na Principle of Autonomy; kwamba, kila mtu mwenye akili timamu, ana haki ya kuchagua Aina ya matibabu/Kinga anayotakiwa kupata baada ya kupewa Elimu ya kutosha juu ya faida na hasara za matibabu hayo. Na haapo ndipo tunapoona umuhimu wa Informed Consent.

Sasa ndugu yenu Mbowe, anataka kuleta siasa kwenye professional za watu. Mwambieni apambane na Katiba, haya atuachie. Hakuna sehemu WHO walisema Chanjo ni lazima. Hata marekani ambao ni wadhamin wakuu wa WHO, majority ya raia wao, hawajapata Chanjo na Kuna wengi tuu wamegomesha na serikali haiwafanyi kitu.
Acheni uongo wakati mwingine unaogeuzwa kisiasa,hivi mgonjwa wa kipindupindu useme anahiari ya kupatatiba au akatae,nini kitatokea.
 
Nasikia pia madhara ya chanjo ni pamoja na kupunguza namna ya kufikri sawasawa, ubongo unapumbazika

Naanza kuamini hii kitu, Anayeleta hii agenda ya kulazimisha watu wote kuchanjwa tayari kesha kula dozi???

Kama tayari, basi madhara yake yashaanza mapeeemaa,!!
 
Mi nadhani hujaielewa hii post inasema nini na kama umeielewa huwezi kulinganisha marekani na afrika katika mlipuko huu wa ugonjwa wa corona huku shughuli zinaendelea bila lockdown watu wamesongamana bila barakoa na bado hakuna maafa kama waliyotabiri hao mabosi zako.
 
Nchi hii kuna ufala mwingi sana, ukichunguza vizuri wanaopinga chanjo chanzo ni Gwajima alipoanza kuipinga mwaka jana, mbona chanjo zote tulizochanjwa ni za wazungu?

Kwanini tusiachane nazo?

Hebu pingeni chanjo kwa hoja za kisayansi ili tuwaunge mkono basi?
Hizi chanjo ni salama. Watanzania wengi wanazipinga kwa sababu ya ulimbukeni. Ila isiwe lazima kwa watu kuchanja. Iwe ni hiari. Cha muhumu elimu itolewe ili watu waondoa hofu waliyopandikizwa na wajinga kama kina Gwajima na marehemu. Ila kusema iwe ni lazima big NO!
 
Hizi chanjo ni salama. Watanzania wengi wanazipinga kwa sababu ya ulimbukeni. Ila isiwe lazima kwa watu kuchanja. Iwe ni hiari. Cha muhumu elimu itolewe ili watu waondoa hofu waliyopandikizwa na wajinga kama kina Gwajima na marehemu. Ila kusema iwe ni lazima big NO!
Mdogo mdogo watazikubali tu, mtu akiwa na safari hapa hawezi kukwepa
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeomba huduma ya utoaji chanjo ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19), iwe ya lazima badala ya hiari kama ilivyotangazwa na Serikali....
Hapo Msee umeyumba sana ww n upepo wakati mwingine
 
Back
Top Bottom