CHADEMA hii ya Lissu na Heche ichangiwe kwa moyo mweupe. Fedha zipo salama hii sio ile SACCOS ya Mbowe.

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
7,748
Reaction score
10,288
Natoa wito kwa Watanganyika wote na Wazinzabari kuichangia Chadema hii maana ipo kwa ajili ya ukombozi wa taifa letu.

Kutoa ni moyo. Watu wachangie bila kuwa na hofu . Pesa na michango ipo salama tofauti na zama za Mbowe.

Propaganda mfu za wanaCCM waliokosa sera zisisikilizwe.

Mimi binafsi nimeshachangia elfu hamsini.
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU (The Ultimatum)
Kutoka Jumuia ya madola


Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:
  • Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.
  • Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.
  • Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.
  • Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.
Je selikali itafanyaje kwa muda iliyopewa?

MWISHO WA UBAYA AIBU.
 
Ni kweli ,tuchange tuchange ,pesa zipo salama ,propaganda za kina ANKO T wa mbutu zisiturudishe nyuma.
 
Ni makosa makubwa mno kumkejeli Freeman Aikael Mbowe ambaye bila yeye CHADEMA ingekuwa kama UDP, DP, NLD, CHAUSTA, PONA na wengineo! Kumbuka Mbowe alivunjwa mguu na alisota jela miaka mingi na kufilisiwa mali zake nyingi akipigania demokrasia leo unamsema vibaya hivi?!
 
Unakabia kwa juu hadi vimbwenerehi wa CCM are deprived of air!
 
Napingana na wewe mbowe alikuwa anatufanyia amaigizo tu, kachangia pakubwa sana kudhohofisha harakani nchi hiii!
 
Napingana na wewe mbowe alikuwa anatufanyia amaigizo tu, kachangia pakubwa sana kudhohofisha harakani nchi hiii!
Sijui nani amefanikiwa kuwadanganya watanzania kiasi hiki! Naamini sio Lissu.
 
CCM wanatamani wasingemnanga Mbowe kwani sasa ndiyo wamebaini kuwa waliruka mkojo wakakanyaga mavi, this time around ndipo wanadai kuwa Mbowe hakuwa gaidi bali mwanasiasa safi.
 
Hii Jumuia ni ya Mabeberu?
 
Mbowe mliyemuita gaidi sasa hivi mnamsifia, akitokea mwingine yoyote akasaliti mapambano pia mtamsifia. Hakuna mwenye hati miliki ya CHADEMA, politicians will come and go lakini chama kitaendela kuwepo. If Mbowe was compromised regardless mazuri yote aliyoyafanya anastahili kusemwa tu, kama ulilea watoto vizuri baadaye ukawasaliti unastahili kusemwa na kusakamwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…