CHADEMA inapokea ruzuku kama kawaida, hawajaigomea

CHADEMA inapokea ruzuku kama kawaida, hawajaigomea

HAKI NA WAJIBU. Nazani wanapoendelea kudai haki yao ni wajibu wao pia kuendelea kupokea fedha maana ni zao kisheria.
 
Ule usemi wa kuwa boss hanuniwi unaendelea kudhihirika ndani ya Chadema. Ambao walisema hawautambui uchaguzi hivyo chochote wanachopata kutokana na uchaguzi huo hawatakipokea.

Lakini kwenye pesa imekuwa tofauti kwani hivi sasa wanawinda 109M kila mwezi toka November na hawajazikataa.

View attachment 1677814
Nimegundua kuwa hii nchi ina wajinga wengi sana. Na tatizo kubwa ni watu kuyachukua mambo kama yalivyo, yaani hakuna hata kujiuliza walau kwa sekunde moja.

Nikusaidie tu kwamba, ruzuku ya chama chochote cha siasa, ni takwa la kisheria, halina uhusiano wowote na matokeo ya uchaguzi au kauli za chama baada ya uchaguzi. Ruzuku sio hisani, ni sharti la kisheria na fedha inatoka mfuko mkuu wa taifa, ambao hauhodhiwi na chama chochote cha siasa, ikiwamo kilichoshinda uchaguzi. Leo hii hata wanachadema wotw wangeondoka chadema na kumuacha Mbowe pekeake, bado ruzuku ingelipwa chadema kwa kuwa tu chadema ilishiriki uchaguzi na kushika nafasi ya pili. Anayewalipa chadema sio aliyeshinda uchaguzi, ni watanzania wote ukiwamo wewe usiyeelewa hata majukumu yako. Usipoelewa na hapa, basi nenda kwa mganga.
 
Mleta hoja umeileta kishambenga sana. Kadiri ya matokeo ya kura za urais na ubunge walizopata wanastahili kupewa hiyo PESA. Sio hisani
Mbona unakuwa mgumu kuelewa? Kinachosemwa ni kwamba kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2020 uliotangazwa na NEC chama cha chadema kinapewa:
1. Viti 19 vya ubunge wa viti maalum
2. Tsh 109 million kila mwezi

Sasa chadema wamekataa katakata matokeo hayo kama alivyokataa Trump. Tena chadema wameenda mbali zaidi ya Trump hadi ku file kesi mahakama ya ICC.
Chadema wamekataa kupokea hivyo viti 19 maalum na hata hiko kimoja cha jimbo na vile vya udiwani wamevikataa lakini ile pesa ya Tsh 109 million kila mwezi wameikubali kwa mikono miwili wakati nayo ni matokeo ya huo wanaouita uchafuzi. Sasa watanzania wawaeleweje hawa jamaa?
 
Nyumbu vigeugeu, hawaeleweki msimamo wao NI upi, Jambo wanakataa leo kesho wanakomaa ni Haki yao.
Nyumbu hovyo kabisa.
 
Ule usemi wa kuwa boss hanuniwi unaendelea kudhihirika ndani ya Chadema. Ambao walisema hawautambui uchaguzi hivyo chochote wanachopata kutokana na uchaguzi huo hawatakipokea.

Lakini kwenye pesa imekuwa tofauti kwani hivi sasa wanawinda 109M kila mwezi toka November na hawajazikataa.
===
Miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, vyama sita vyenye sifa ya kupata ruzuku vimeanza kuneemeka baada ya kuingiziwa mgawo wa fedha na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Vyama ambavyo vimevuna fedha hizo za mgao wa ruzuku hiyo unaotokana na idadi ya wabunge, madiwani na kura za urais ni pamoja na CCM, Chadema, ACT-Wazalendo, CUF, NCCR-Mageuzi na kile cha Democratic Party.

Kwa mujibu taarifa ambazo gazeti hili linazo, chama kinachoongoza kwa kuzoa ruzuku hiyo ni CCM yenye wabunge 354 ambacho kimepata zaidi ya Sh1.33 bilioni, Chadema ‘inayohesabiwa’ kuwa na wabunge 20 imepata Sh109.68 milioni, ACT Wazalendo yenye wanne kimepata Sh14 milioni na CUF yenye mbunge mmoja ikipata Sh5.7 milioni.

Vyama vingine vinavyopata ruzuku kwa idadi ya kura za madiwani ni pamoja na NCCR Mageuzi kilichoambulia Sh316,937, huku DP ikiambulia Sh63,387.

View attachment 1677814
Baniani mbaya kiatu chake dawa.
 
Kwani wewe ukipewa hela na aliyekulamba makofi siku nyingi utaikataaaa??,, ndo mana ikaitwa hela, fedha, pesa, hundi, nk🤣🤣🤣🤣
 
Kuna wajinga huwa hawasikii hata ukiwaponda na marungu wanabaki hivyo hivyo, huu uzi ni mfano wa vibuyu wasiopenda kueleweshwa, wao ni ushabiki tu.
 
Nimegundua kuwa hii nchi ina wajinga wengi sana. Na tatizo kubwa ni watu kuyachukua mambo kama yalivyo, yaani hakuna hata kujiuliza walau kwa sekunde moja.

Nikusaidie tu kwamba, ruzuku ya chama chochote cha siasa, ni takwa la kisheria, halina uhusiano wowote na matokeo ya uchaguzi au kauli za chama baada ya uchaguzi. Ruzuku sio hisani, ni sharti la kisheria na fedha inatoka mfuko mkuu wa taifa, ambao hauhodhiwi na chama chochote cha siasa, ikiwamo kilichoshinda uchaguzi. Leo hii hata wanachadema wotw wangeondoka chadema na kumuacha Mbowe pekeake, bado ruzuku ingelipwa chadema kwa kuwa tu chadema ilishiriki uchaguzi na kushika nafasi ya pili. Anayewalipa chadema sio aliyeshinda uchaguzi, ni watanzania wote ukiwamo wewe usiyeelewa hata majukumu yako. Usipoelewa na hapa, basi nenda kwa mganga.
Hata Viti maalum ni takwa la kisheria.
 
Siasa ni zaidi ya ujuavyooooo. kulikuwa na vijana machachari/machalari sanaaaaa leo hii wapo kimyaaa, maisha yanaendelea

Wao wanakula kuku kwa mirija sie wapiga kura twabaki kubwata bwata tu
Ndiyo maana ni upumbavu mwananchi kushiriki maandamano yanayolenga kulinda au kutetea maslahi ya wanasiasa kwa kivuli cha kuonea huruma wananchi.
 
Wabunge 19 viti maalumu hawana mchango wowote kwenye ruzuku!Muwe mnajielimisha kabla ya kuandika!Ruzuku hutokana na makundi haya
1.Kura za urais
2.Wabunge wa kuchaguliwa
3.Baraza la madiwani!

So unaposema Halima Mdee na wenzake wamewezesha uzuku,unakuwa unapotosha kwa kujua au kutokujua!
Hata leo akina Halima Mdee wakifukuzwa Ubunge,Hizo factor 3 hapo juu haziwezi kubadilika hivyo ruzuku itabaki ileile!
Mbunge wa kuchaguliwa ndiye anayeweza kuathiri Ruzuku!
Kwa maana hiyo Gazeti la Mwananchi wameripoti uongo "Kwa mujibu taarifa ambazo gazeti hili linazo, chama kinachoongoza kwa kuzoa ruzuku hiyo ni CCM yenye wabunge 354 ambacho kimepata zaidi ya Sh1.33 bilioni, Chadema ‘inayohesabiwa’ kuwa na wabunge 20 imepata Sh109.68 milioni, ACT Wazalendo yenye wanne kimepata Sh14 milioni na CUF yenye mbunge mmoja ikipata Sh5.7 milioni."
 
Vigezo ni hivyo!Wabunge wa viti maalum hawana mchango kwenye ruzuku!Kilichosababisha CDM ipate ruzuku nyingi kuliko hivyo vyama vingine ni kura za urais!
CDM ilinalijua hilo ndio maana iliwafukuza viti maalum!
 
Mwambie mbowe atangaze kuwa ame pokea na wakina halima mdee wame mwongezea ruzuku la sivyo angepata ml 5 kwa mbunge mmoja
 
Hiyo haki wanaidai wapi?
Heheheh hvi ipo chama gani cku hzi! Naona toka Matiko akufute rasmi kwenye ulimwengu wa siasa basi ww ni kupambana na CHADEMA tu.

Huko ACT nako vp ulikimbia ama umerudi NCCR? Anyway kwenye hiko kijarida hakuna mahali popote wamencofirm CHADEMA kupokea ruzuku zaidi ya kuproject kuwa ITAPATA...... Not IMEPOKEA!!

So till then hakuna hta senti 5 yenu iliyoguswa.... Maana haiwezekani wakubali pesa alafu wakatae wabunge 20 ambao wakichanga 15% ya mapato yao kila mwezi chama kingepata zaidi 40M kwa mwezi pamoja na platform ya kumwaga sera.

It's madness
 
Mwambie mbowe atangaze kuwa ame pokea na wakina halima mdee wame mwongezea ruzuku la sivyo angepata ml 5 kwa mbunge mmoja
Kuna miaka CHADEMA ilikua na wabunge 3 tu na bado ilirusha helikopta kampeni zote za Urais mpka udiwani.

Chama hakitegemei ruzuku tu but kuna wadhamini, ada za wanachama, miradi ya kisiri ya chama, ndio maana 400M ilipatikana ndani ya saa 72 tu walipofungwa viongozi wote wakuu
 
Wamepokea au wamewekewa? Unakataaje pesa iliyodumbukizwa kwenye account yako? Unajuaje kama wanafanya mpango wa kuwarudishia waliowawekea? Au una hakika gani kuwa wamezitumia?
Kitu cha kujiuliza ni kama hao "wabunge" wanachangia chama " chao" kulingana na muongozo wa chama " chao" ? Na chama kinapokea?

Amandla...
 
Yani Mbowe arudishe hela? Unaota wewe!
 
Kuna miaka CHADEMA ilikua na wabunge 3 tu na bado ilirusha helikopta kampeni zote za Urais mpka udiwani.

Chama hakitegemei ruzuku tu but kuna wadhamini, ada za wanachama, miradi ya kisiri ya chama, ndio maana 400M ilipatikana ndani ya saa 72 tu walipofungwa viongozi wote wakuu
Mlichanga milioni 400 huku bilioni 8 zilizokusanywa chadema kwa miaka 5 zikiwa hazijulikani zilipo
 
Back
Top Bottom