CHADEMA kukataa mualiko wa NEC wakati wanasubiri mualiko wa Rais Samia ni kichekesho

Uwezo huu wa uchambuzi ungekuwa unatumika na uongozi wa Chadema, chama kinge kuwa mbali.

Ninazo evidences nyingi ambazo uongozi wa Chadema haufanyi kabisa au hata kusikiliza synthesis analysis ya major events ili kupata critical path analysis huwa hilo halipo kabisa .

Na ukitaka wafuate uchambuzi wa kitaalamu wa kila jambo, watakwambia toa usomi wako hapa. Wataalamu ambao wanaweza kusikilizwa Chadema ni Wana sheria tuu, na sababu uongozi unafanya ya kuishi kisiasa kwa kuvunja sheria.

Ndio maana si shangai vilaza kuwa uongozi wote wa juu kabisa wa Chadema,
 
Bwashee, hata huko kwa rais wameshaghairi asipokutana nao peke yao. Akiwaweka kwenye kundi la vyama vyote basi hawaendi!
Ujinga uliomo chadema sasa hivi hata kwa fimbo hatuwezi kuutoa.
Uzuri mmoja tozo haziangalii huyu ni mataga or huyu ni chadema 🤣🤣🤣
 
Kuna wakati tunafanya propaganda isiyo na mashiko. Vyama vyote vilivyokataa kushiki hafla ya Jana wapo sahihi
Maana waliikata mimba hivyoawana sababu kushiriki kwenye ubatizo wa mtoto.

Nchi lazima iwe na mkuu wake bila kujalishha amepatikana vipi. Majadiliano yafanywe kupata mwafaka.
Hivyo tu
 
Ni chama kipi kina hizo sifa ulizozitaja?
 
Kwa walio andikwa hapa na hakika mimi sijaona bado ninavyotakiwa kuongea. Hiyo Chadema wewe huifahamu kama ninayo ifahamu mimi.

Nimejiunga nayo nipo chuo, mwaka wa pili tuu baada ya kuanzishwa.
Rais Mwinyi alitufukuza na kufunga chuo 1994, tukapoteza
Mwaka, na bado niliendelea kuwa Chadema. Wazazi wakanipeleka nje kusoma zaidi, ili pia nipate nafasi ya kuachana na Chadema, niliporudi bado nikawa Chadema.

Ila nilihama 2015 moja kwa moja, labda kwenye social justices tuu ndio nakuwa sympathiser.

Huku kwa wazazi Lyamungo Sinde, Machame. Chadema ni maisha ya kila siku.
Kama hivi sasa hapa tupo Msibani kwa mama Mtei na Bi mkubwa wangu na Mwenyekiti wako hayapo.

Sisi ndio wale tukitaka kuibomoa Chadema utalia na kubadilisha Chama siku hiyo hiyo.

Ninachu shukuru sana hapa Jimbo lá Hai Chadema tumeisafisha, tumeijeruhi sana kiasi inaelekea kufa tumeisafisha na kuipiga deki kwa Machine na

KIJANA WETU MHESHIMIWA MNO LENGAI OLE SABAYA

kamaliza wizi wa kutumia silaha na mtandao wake,
Wizi wa magari na mtandao mzima.
maisha ya dhulma kwishney Ubabe usio na mpango keishney.

Bi mkubwa mama Grace unaweza kulala bila kufunga milango na sio lazima gari aiingize parking ya ndani ya nyumba. Hata akiziacha kwenye lawn tuu siku hizi inatosha.

Wazawa wasio na ardhi, aibu hiyo imekwisha, jimbo letu Wakristo ni wengi. Lakini ndilo lenye idadi kubwa ya Waislamu wazawa katika majimbo ya Kilimanjaro wanafuatiwa na Mwanga. Vitu vyote vilivyo kuwa karaha kwa Waislamu wame sawazishiwa, kama shule zao, maeneo yao ya misikiti, ardhi za Jumuiya zao.

These are long-standing social injustices we have been living with in Hai District for ages.

Madonda ndugu ya Hai CCM IMEYAPONESHA. .
 
Well said
 
Ukiangalia kwa haraka nikuwa NEC inaendelea kujitangaza kuwa haikubaliki, na haiaminiki na watu wowote zaidi ya wale walio nufaika nao.
Hapa kuna ushirika wa NEC na wanufaika nao yaani CCM and Allies.
Kukataliwa huku kunaionyesha dunia tatizo letu la kikatiba lilivyo. Ila kwa watawala, hawaoni wala kusikia mana mlo umepofusha macho.
Ninacho shukuru ni kuona mambo hayahaya yanaamsha watu walio lala. Ingawa hawatapinga kwa mapigano, ila wanaandaliwa kuwa tayati kuunga mkono mtu atakae jitolea kupinga kwa mapigano.
 
Ningewashangaa sana Chadema kama wangelikwenda huko wakati anayewaalika ndiye anamshikilia Mwenyekiti Mbowe!
 
Nimekunyoosha, nimeongea na ma'am yako atakupigia Sasa hivi akwambie baba yako ni Nani maana huyo unayejidai naye Ni wa kufikia

Nimekunyoosha, nimeongea na ma'am yako atakupigia Sasa hivi akwambie baba yako ni Nani maana huyo unayejidai naye Ni wa kufikia
Retired, mbona leo umejaa matusi hivyo? Tena haziko proportional na hoja. Unazimwaga tu.
 
Kwa hiyo unalazimisha chadema wakae pamoja na cuf au vile vyama pandikizi vinavyojiita ni vyama vya upinzani kumbe mlango wa nyuma ni ccm???Unaelewa maana ya upinzani wewe??Kama mtu umekubali kuwa mpinzani unatakiwa uwe na maono yako kufuatana na falsafa ya chama husika.
 
Unasemaje kuhusu ACT-Wazalendo, CUF, NCCR-Mageuzi ambao pia walikataa kwa sababu hiyo hiyo? Ama mimba yako hiyo mtoto hujigeuza tu pale anapotajwa CHADEMA?
 
Samia si katokana na huo uchaguzi batili? Hiyo ina maana urais wake ni batili pia, then why mnataka kuonana na Rais batili?
Kuonana naye ni lazima pamoja na ubatili wa kuwepo kwenye kiti kile ili kuweka mambo sawa,kukataa kukutana na Samia ni kushindwa kutimiza wajibu na haki ya kisiasa katika kudai madai halali,pia Samiah ni mwanadamu pengine anadanganywa sana na watu wa kariba yako lakini atakapokutana na viongozi wa Chadema ana kwa ana kuna maswala yaliyojificha chini ya pazia yataibuliwa na atayafanyia kazi.
Vilevile Chadema kama chama kikuu cha upinzani wana madhaifu yao ambayo Rais Samiah anayajua pamoja na watu wengine kama wewe,atawaambia wasasahishe sehemu fulani ili mambo yaende sawa.Hivyo lengo la kukutana si ushabiki bali ni maridhiano kwa usalama wetu na usalama wa nchi yetu.
 
Ni kwa mwenye ufinyu wa akili tu ndiyo anaweza kuandika hivi. Mpaka hapo nchi itakapoingia kwenye machafuko ya kutisha kwa UCHAFUZI wa uchaguzi ndiyo mtatia akili kichwani.

Machafuko hayata muathiri mmoja, hata wewe unayeombea Taifa liingie kwenye machafuko hutakwepa athari za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja.
 
Safi sana.
Kitu ambacho hujui, hata ukipindua nchi na ukaweza bado utaitwa rais, CHADEMA wapo sahihi kabisa, Samia hata angekuwa amefanya mapinduzi bado angekuwa ni rais japo hatakuwa amepatikana na njia ya kidemokrasia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…