Pre GE2025 CHADEMA kutoshiriki uchaguzi mkuu 2025 litakuwa ni pigo kubwa sana kwa Rais Samia Suluhu Hassan na serikali ya CCM kidiplomasia na kiutawala

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tanzania ina vyama Vya siasa zaidi ya 12 na vitashiriki uchaguzi sasa chama kimoja cha siasa ndo kinaathiri nini??

Msijipe umuhimu msiokua nao uchaguzi utafanyika na maisha yataendelea punguzeni utoto.
Tofautisha kati ya vyama na magenge ya machawa yanayofadhiliwa na yule msagaji
 
Hakuna hanayejipa umuhimu, ngoja uchaguzi ufanyike na CHADEMA wasishiriki, baada ya hapo taswira ya Tanzania kimataifa itakuwa na sura mpya na ngumu sana, vile vile hii itamtia doa hata Rais Samia.
CCM haiogopi tena hicho kinacho itwa kutiwa doa wamesha zoea
 
Sidhani kama unajua athari alizoziacha mwenda zake ktk utawala wake ni msifu kwa kiasi fulani Mama samia kwa juhudi alizo fanya za kuifungua nchi ila tulikuwa tunaelekea kubaya sana hata zimbabwe kingekuwa cha mtoto sidhani kama Mama angependa turudi huko, hivi sasa Tanzania inaaminiwa kwa sababu ya alivyo fanya Mama samia, kama atakuwa amesahau hali ilivyokuwa, ashupaze shingo, nakwambia atakuwa na hali ngumu sana kwenye awamu yake. Mimi nimuombe Raisi asiwasikilize wachumia tumbo tu aangalie na mstakabali wa serikali yake. Asije akairudisha nchi nyuma, tunamwamini, tunampenda na bado tunamuitaji. Ata kwa unafiki tu awasikilize wapinzani la sivyo, mambo yataharibika sana na uchumi wetu kwavsasa umesimama pazuri, utaporomoka kama chaguzi zitakuwa za magumashi kama miaka mingine yote. Chondechonde Raisi wetu usizibe masikio na kusikiliza watu wapande mmoja tu utakaye kuja kupata shida ni wewe,.
 
Watu mkiitwa wapumbaf mnasema mnatukanwa, hivi yaliyotokea 2019,2020 na mwaka jana 2024 unaweza kuita ni uchaguzi? Mwaka jana Rais alitamka mwenyewe kuwa uchaguzi huu wa serikali za mitaa 2024 mambo ya 2019 na 2020 hayatajirudia kamwe lakini yakawa vilevile.
Sasa jitu jinga linatoka huko na kusema eti "wana tamaa ya madaraka hao"!
Upuuzi mtupu, sasa Chadema wamesema NO REFORM NO ELECTION mnaogopa nini kufanya hizo reform?
Eti vipo vyama vingine 12! Sisi sio wajinga, vyama gani visivyo hata na mwenyekiti wa mtaa? Vina wakilisha wananchi wepi?
Wajinga ni watu wasio tumia hekima, kisha nchi zao zikija geuka Sudan au Congo wanalia lia eh Mungu tunusuru na wakati huo hawa wanao wasapoti washaiba rasilimali zenu na wanaishi Dubai na Honolulu.
Kweli wajinga ndio Waliwao
 
Tanzania ina vyama Vya siasa zaidi ya 12 na vitashiriki uchaguzi sasa chama kimoja cha siasa ndo kinaathiri nini??

Msijipe umuhimu msiokua nao uchaguzi utafanyika na maisha yataendelea punguzeni utoto.
unaijua CHADEMA wewe?
 
Hakuna cha pigo wala, misitake kujipa umuhimu msiokua nao.
Msiposhiriki wengine watashiriki na kwa kua CCM itakua imeshafanya utafiti wake wa kujua itashinda kwa kiwango gani kura zilizokua ziende CHADOMO zitasambazwa kwa vyama vyengine vitakavyoshiriki.
Labda CHADOMO wajitoe siku hiyo hiyo ya uchanguzi ndio mnaweza kuwaendesha ovyo CCM.
 
Kwa nini ccm hawataki kusikia mabadiliko ila muda utaongea mabadiliko ya kimfumo yapo kiubeba ccm
Tuache kushupaza shingo ccm wenyewe wanamjua hili
 
Sasa hapo pigo ni lipi? 😂😂
 
Huyu Mama Kizimkazi ana kazi kubwa sana mwaka huu
 
Tanzania ina vyama Vya siasa zaidi ya 12 na vitashiriki uchaguzi sasa chama kimoja cha siasa ndo kinaathiri nini??

Msijipe umuhimu msiokua nao uchaguzi utafanyika na maisha yataendelea punguzeni utoto.
Tofauti na chadema vilivyobaki sio vyama vya Upinzani ni matawi ya CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…