Chadema na ACT wanatakiwa kujua kuwa watanzania sio wapumbavu kiasi hicho kwamba waende barabarani kuandamana kwasababu ya kutetea ulaji wa wanasiasa.
Miaka yote chaguzi zinapo fanyika wapinzani hulalamika kuibiwa Kura lakini kwa kuwa walikuwa wanashinda ubunge na kuwa na uhakika na shibe ya matumbo yao walikuwa hawaoni umuhimu wa kuandamana na kudai haki.
Uchaguzi wa 2020 umekuwa tofauti kwao baada ya watanzania kuwanyima nafasi za kuingia bungeni kunufaika na Kodi zetu huku wakishinda kutwa kutukana na kususia vikao vya bunge na wakiti mwingine wakijifunga midomo ili wasichangie chochote bungeni ama kuanzisha fujo kwa makusudi(mkasahau kuwa wananchi ndio waajiri wenu). Leo ndio mmeona umuhimu wa kuandamana baada ya kukosa ajira?
Ukweli ni kwamba watanzania hatuta andamana na hatuto tii amri zenu zozote.
Kumbukeni jinsi tulivyo kataa amri yenu ya kukaa kwenye vituo kulinda Kura basi mjue kuwa hata hili la kuandamana halito fanikiwa pia.
Kesho tutakwenda kwenye shughuli zetu za kutafuta ugali kwaajili ya watoto wetu na si kupigania ulaji wenu huku mkijificha kwenye kivuli Cha Demokrasia.
Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya wapiga kura, hiyo Demokrasia mnayo itaka nyinyi ya lazima upinzani washinde kamwe haiwezi kukubalika kwetu.
Mwisho niseme tu kuwa tunawapuuza Kama tulivyopuuza agizo la kulinda Kura .
Andamaneni wenyewe na familia zenu zinazonufaika na mishara yenu ya kibunge Ila sisi msituhusishe.
Mwlm Nyerere alikuwa sahihi alipo sema hutuwezi kuwapa nchi CHADEMA