Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nov 2, 2020 kupinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nov 2, 2020 kupinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu

Ndugu yangu posho za ubunge ufaidi na familia yako, baada ya kukosa uniingize mimi barabarani nikale mkong'oto wa polisi . Chukua familia yako itangulize mbele. Mi najua uchaguzi umeisha kifuatacho ni kuchapa kazi.
Tutaenda tunaojitambua
 
Ndugu yangu posho za ubunge ufaidi na familia yako, baada ya kukosa uniingize mimi barabarani nikale mkong'oto wa polisi . Chukua familia yako itangulize mbele. Mi najua uchaguzi umeisha kifuatacho ni kuchapa kazi.
usha ogopa wewe na ukiogopa haki zako ume zizika na umoja ninguvu sikuzote ata mkoloni aliondoka kwa umoja wetu sasa tuta andamana kwasababu ni kwafaida yetu🙏🙏🙏
 
Chadema na ACT wanatakiwa kujua kuwa watanzania sio wapumbavu kiasi hicho kwamba waende barabarani kuandamana kwasababu ya kutetea ulaji wa wanasiasa.

Miaka yote chaguzi zinapo fanyika wapinzani hulalamika kuibiwa Kura lakini kwa kuwa walikuwa wanashinda ubunge na kuwa na uhakika na shibe ya matumbo yao walikuwa hawaoni umuhimu wa kuandamana na kudai haki.

Uchaguzi wa 2020 umekuwa tofauti kwao baada ya watanzania kuwanyima nafasi za kuingia bungeni kunufaika na Kodi zetu huku wakishinda kutwa kutukana na kususia vikao vya bunge na wakiti mwingine wakijifunga midomo ili wasichangie chochote bungeni ama kuanzisha fujo kwa makusudi(mkasahau kuwa wananchi ndio waajiri wenu). Leo ndio mmeona umuhimu wa kuandamana baada ya kukosa ajira?

Ukweli ni kwamba watanzania hatuta andamana na hatuto tii amri zenu zozote.
Kumbukeni jinsi tulivyo kataa amri yenu ya kukaa kwenye vituo kulinda Kura basi mjue kuwa hata hili la kuandamana halito fanikiwa pia.

Kesho tutakwenda kwenye shughuli zetu za kutafuta ugali kwaajili ya watoto wetu na si kupigania ulaji wenu huku mkijificha kwenye kivuli Cha Demokrasia.

Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya wapiga kura, hiyo Demokrasia mnayo itaka nyinyi ya lazima upinzani washinde kamwe haiwezi kukubalika kwetu.

Mwisho niseme tu kuwa tunawapuuza Kama tulivyopuuza agizo la kulinda Kura .

Andamaneni wenyewe na familia zenu zinazonufaika na mishara yenu ya kibunge Ila sisi msituhusishe.

Mwlm Nyerere alikuwa sahihi alipo sema hutuwezi kuwapa nchi CHADEMA
 
Maandamano ya mtandaoni labda.

Watanzania wanataka amani ndio maana wameipigia CCM
ZZK anaongea kukwepa aibu. Anaonyesha kura zilipigwa kabla lakini hapeleki zionekani zilipigwa wapi na nani. Wenzale wamezichoma moto kuogopa kushtakiwa kwa sababu walizitengeneza wenyewe. Watanzania HATUDANGANYIKI. Zito pole sana. Wote tunasapoti polisi kuhakikisha tuko salama na vikundi ulivyoandaa tumesharipoti wakijaribi kesho andaa mazishi yao japo wewe hutashiriki.
 
Naona hapa kuna mtu anatafuta risasi 32 maana zile 16 ni za kuonja.
 
usha ogopa wewe na ukiogopa haki zako ume zizika na umoja ninguvu sikuzote ata mkoloni aliondoka kwa umoja wetu sasa tuta andamana kwasababu ni kwafaida yetu🙏🙏🙏

Sawa, me ntakuwa na mishe zangu we nenda boss
 
Maandamano ya mtandaoni labda.

Watanzania wanataka amani ndio maana wameipigia CCM
Nani akipe kura chama kinacho vunja Sheria za utumishi wa imma?
Nani akupe kura chama ambacho hanitaki kutoa haki za watumishi?

#YNWA
 
Nimekusoma kwa mara ya kwanza tokea...; pole rafiki!
japo nipo siku zote , uchaguzi huu ulikuwa tayari na matokeo dunia yote inajua na mimi ninao ushahidi , kwahiyo hakuna haja ya kupeana pole
 
Back
Top Bottom