Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nov 2, 2020 kupinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nov 2, 2020 kupinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu

japo nipo siku zote , uchaguzi huu ulikuwa tayari na matokeo dunia yote inajua na mimi ninao ushahidi
Nafurahi kusikia ushahidi upo, na ni matumaini yangu makubwa kwamba utatumika barabara wakati utakapohitajika.
Kuhusu hili la "... uchaguzi huu ulikuwa tayari na matokeo...", swali ni kwa nini mliruhusu uchafuzi huo uendelee huku mkiwa mnajua ulikuwa umeandaliwa?

Huoni kwamba fursa nzuri ilikuwa ni kuuzuia uchafuzi huo mara moja huko huko kwenye vituo vya kupigia kura? Ingekuwa rahisi zaidi na salama zaidi kama zoezi zima la kupiga kura lingesitishwa wakati mawakala wenu wanazuiwa kufanya kazi mliyowatuma waifanye.

Na hata hiyo mikoba ya kura zilizoingizwa, hapo hapo ndipo zingeonyeshwa kwa wananchi nchi nzima.

Kwa nini mlikubali uchaguzi uendelee? Hilo ndilo swali.
 
Safi sana, bado hasira za kushindwa vibaya zipo lkn kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo zinavyozidi kupungua, hata matusi yanazidi kupungua siyo kama siku kwanza hapa JF, rhetoric zimebadilika kuelekea kukubali hali kama ilivyo, time heals all wounds wanasema Wazungu, hivyo wataandamana kesho, kesho kutwa ikifika Ijumaa wamechoka, mwishowe watakubaliana na hali na maisha kurudia kawaida, ...
Mchawi tu wewe, hayo manukta na makoma yasiyo na mpangilio peleka kwa wapuuzi wenzio wa Lumumba
 
Yani mtu kanyang'anywa Jimbo Kigoma, wengine Kilimanjaro, Arusha, Musoma na kwingineko, alafu maandamano unakuja kuyafanyia dar na mitandaoni, kwakua umeiona dar ndo shamba la bibi?

Hizo posho za ubunge ulikuwa unagawana na hao wananchi unaotaka wakaandamane? Achana na swala la watu kuuliwa, wakivunjwa hata miguu na mikono utagharamia matibabu yao?

Pumbavu zenu. Zitto wewe ni mjinga.
 
Acheni unafki. Walivyoangushwa wenzenu wasio na majina Seikali za mitaa,hamkuitisha maandamano. Leo mibuyu imekatwa ndo mnataka maandamano just because mmeguswa.
Acheni Tamaa. Sasa tulieni muungane mfanye siasa za kweli na si za maslahi yenu binafsi.
Victorie mama huwa sikuelewi kabisa unasimama upande gani? Ila kwa hili la maandamano tuko pamoja hawa viongozi baada ya kuona hawatopata posho za bunge wanadai haki, binafsi ningependa kesho wawe pamoja na watoto na wake zao barabarani tofouti na hapo waache sinema za ajabu kwa watanzania...

Jana mchana nimekutana na viongozi hawa maeneo ya Rose Garden, sugu a.k.a jongwe kachoka naona haamini kama hatokalia kiti chekundu
 
Madhumuni ya maandamano ni kudai Uchaguzi chini ya Tume huru ya Uchaguzi OK.

Yani maana yake tume hii ya sasa sio huru?
Then kwanini mlikubali kuingia kwenye uchaguzi ambao mnajua tume sio huru?

Kwanini msifanye hayo maandamano kutaka tume huru kabla ya uchaguzi?

Mngeshinda uchaguzi mngesema tuandamane kudai tumehuru?

Acheni kufanya watu kama wajinga kaandamane mwenyewe na familia yako.
 
Uchaguzi ulishaisha sasa tuijenge nchi...

Kwenu vijana wenzangu epukeni kutumika na wanasiasa ambao wanataka kuona mkipata shida ili wao wapate political mileage wahenga walisema "za kuambiwa changanya na zako" na " mchuma janga hulia na wa kwao"..

OTHERWISE
Hongera Magufuli,Hongera Mwinyi,Hongera CCM
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Msisahau kuwaalika wake zenu, watoto wenu, waume zenu, shangazi zenu, wajomba zenu na ndugu zenu maana kesho sisi tutakuwa tunashirikiana na JWTZ kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu
 
Ongera kwa kutoa ratiba
Wale jamaa waliomkanyaga Jussa kule Zanzibar kesho watakuwepo ubungo na buguruni
hatutaki mtu akimbie
Makamanda mnatakiwa mkomae hata ukila buti la shingo komaa hivyo hivyo ili ufe shahidi
Tayari vijana wa Asterdam watakuwepo katika hayo maandamano watabeba makamera makubwa ili picha za mnato na za video zichukuliwe kama ushahidi
Kule Zanzibar kipondo walikipata mbaka viongozi wale vihere here tunasubiri na hapa tuone
Mm nitakuwepo youtube nikishuhudia hayo maandamano makubwa kuwai kutokea africa
 
Ongera kwa kutoa ratiba
Wale jamaa waliomkanyaga Jussa kule Zanzibar kesho watakuwepo ubungo na buguruni
hatutaki mtu akimbie
Makamanda mnatakiwa mkomae hata ukila buti la shingo komaa hivyo hivyo ili ufe shahidi
Tayari vijana wa Asterdam watakuwepo katika hayo maandamano watabeba makamera makubwa ili picha za mnato na za video zichukuliwe kama ushahidi
Kule Zanzibar kipondo walikipata mbaka viongozi wale vihere here tunasubiri na hapa tuone
Mm nitakuwepo youtube nikishuhudia hayo maandamano makubwa kuwai kutokea africa
Ni upuuzi kushabikia raia wasio na hatia wakipigwa kisa kudai haki zao.

Mbona Lissu alipotua Dar watu walifanya maandamano ya amani na hakuna vurugu ilitokea? Kwani mkiacha waandamanaji wakusanyike kwa amani mnakosa nini?

Hili bara kweli lina laana
 
Back
Top Bottom