CHADEMA: Polisi wenye silaha za moto wazuia msafara wa Makamu M/kiti wetu, Tundu Lissu ukielekea Kibaha

CHADEMA: Polisi wenye silaha za moto wazuia msafara wa Makamu M/kiti wetu, Tundu Lissu ukielekea Kibaha

Ukiona hilo Jeshi la Polisi linatumia nguvu hivyo kumdhibiti huyo Tundu Lissu, ujue hao watawala wa CCM weshaona maji yako shingoni!

Hilo Jeshi la Polisi, kwa kujua au kutojua, wanampaisha mno huyo Tundu Lissu.......

Ukombozi kamili tayari ushakaribia mno.......

Tarehe 28/10/2020 twende tukamalize kazi..........

Watanzania wana jambo lao kwenye sanduku la kura
Ushindi unakaribia
 
Hao polisi walikuwa kwenye msafara wa waziri mkuu sasa kama mtu wenu anataka kuvuruga basi lazima athibitiwe vilivyo!
 
Tatizo la CCM na vyombo vyake ni wazito wa kuelewa au wanajifanya hawaelewi! Kwasasa Lissu ana kofia mbili , ni mgombea urais na pia ni Makamu mwenyekiti! Hata Mbowe ameshalifafanua hili, kwa hiyo kwasasa anafanya kazi za chama kama Makamu mwenyekiti, CHADEMA imeweka wagombea nchi nzima hivyo uongozi hauwezi kubaki kukaa tu pale ofisini bila kufanya shughuli za kimkakati!

Mbona waziri mkuu Khasim Majaliwa sio mgombea wa nafasi ya kitaifa lakini anazunguka huku na huko akitumia kofia ya mjumbe halmashauri kuu ya taifa ya ccm kufanya kampeni tena ambazo hata ratiba yake haitambuliwi na NEC?

Hazuiliwi na wala hapigwi mabomu na hata tume haitoi kauli yoyote ilihali hata mwananchi wa kawaida tu anaona wazi jambo hilo sio halali!
 
Umefanya fujo barabarani?

Tumemtuma sisi wafanyakazi, sisi wafanyabiashara tuliofilisiwa, wakulima wa ufuta, mbaazi na korosho, sisi tunaokatwa 15% HESLB n.k
Mzito kuelewa ni yule anayetoa rushwa ya uchaguzi hadharani
Jamani jamani Magufuli kaumiza watu. Haisemeki kiwango cha maumivu kilichopitiwa. Kaumiza watu jamani jamani jamani. Hivi ni kuwa watu hawaelewi au wamelipwa waje kumfanyia kampeni?
 
Back
Top Bottom