CHADEMA: Polisi wenye silaha za moto wazuia msafara wa Makamu M/kiti wetu, Tundu Lissu ukielekea Kibaha

Kwahiyo Lisu alikuwa anaenda kufanya nini sasa? Ana bidhaa anauza pale?

Kila anayeenda sokoni ana bidhaa anazouza? Mkuu sioni kama una jipya kwenye huu mjadala. Naona ni upuuzi tu tunajadili hapa wa mtu kwenda au kutokwenda sokoni. Iko siku ataenda uwanjani kuangalia mpira utasema kuwa anaenda kuangalia mpira kwani ni mchezaji?
 
Mkuu kwa hadhi ya Lisu sokoni alikuwa anaenda kufanya nini? Alitumwa kununua nyanya ama kitu gani?
 

Nyie propangandists wa CCM mnapata taabu Sana Uchaguzi wa mwaka huu! Hakika Tundu Antipas Lissu amembana Magufuli mpaka ameamua kutumia Mapolisi na Tume Chaguzi isiyo Huru.
Hapo Ni hakuna Cha Prevention is better than Cure wala intelijensia zaidi ya UHUNI!
 
Matendo yanayotendwa na vyombo vya Ulinzi dhidi ya wapinzani ni uonevu Ambao Tanzania tulipinga wakati Waafrika wananyanyaswa na Makaburu. Askari wetu kutenda matendo haya ni sawa na kulidhalilisha Taifa letu ambalo lilikuwa mstari wa mbele kupinga vitendo hivi viovu.

Matendo haya maovu hayawezi kuleta afya njema ya Taifa letu.​

 
Yaan hii nchi jamani Lissu ndio tishio kiasi hiki jamani
 
Kwa mujibu wa RPC Lissu alitakiwa kuomba kibali polisi masaa 48 kabla ya kufanya mikutano yake kwa jeuri hakuomba hicho kibali
wakati sheria anajua wazi kuwa alihitaji kibali cha polisi kufanya hiyo mikutano na kupewa ulinzi.

Lissu in tatizo hivi hata hajui kuwa huwezi weka mikutano bila kibali cha polisi sababu yeye kwa sasa sio mgombea ni kiongozi wa kawaida wa chama anayewajibika kuomba kibali cha mikutano yake.
 
Mkuu kwa hadhi ya Lisu sokoni alikuwa anaenda kufanya nini? Alitumwa kununua nyanya ama kitu gani?

Kwako wewe kwenda sokoni ni mpaka uwe huna hadhi? Mkuu kwangu kujadili jambo dogo hivi ni kuishiwa hoja.
 
Nani kakuambia mikutano ya siasa inahitaji kibali cha policcm?
Ya kampeni haihitajiki sababu tume ilishatoa ratiba na copy kupewa Polisi ya kawaida lazima upate kibali cha polisi ili wawepo kulinda usalama wa raia na Mali zao.
 
Kwako wewe kwenda sokoni ni mpaka uwe huna hadhi? Mkuu kwangu kujadili jambo dogo hivi ni kuishiwa hoja.
Twambie basi akikuwa anaenda hapo sokoni kufanya nini?
 
Kwani Lissu alisema anafanya kampeni Leo?
Ya kampeni haihitajiki sababu tume ilishayoa ratiba na copy kupewa Polisi ya kawaida lazima upate kibali cha polisi ili wawepo kulinda usalama wa raia na Mali zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…