CHADEMA wamesema hawatoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe

CHADEMA wamesema hawatoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe

Chama cha CHADEMA kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Muhambwe lililopo wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma.

Jimbo la Muhambwe liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge Atashasta Nditiye kufariki dunia Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari iliyotokea Februari 10, 2021 eneo la Nane Nane, mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Benson Kigaila amesema baada ya kikao cha kamati kuu kilichofanyika Machi 31, 2021 kwa njia ya mtandao wameazimia kutoshiriki uchaguzi huo kutokana na mazingira ya tume ya uchaguzi kutotenda haki.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshatangaza kuwa uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika Mei 2, 2021.

Tayari Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Florence Samizi kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Chanzo: Mwananchi
Kususia uchaguzi ni upumbavu.
Kama kweli kuna nia ya dhati ya kuboresha demokrasia yetu, vyama vya upinzani vina nafasi ya kufanya hivyo kwa kushiriki fursa zilizopo kwani kwa kushiriki ndipo wanapoweza kuona penye changamoto na kupendekeza maboresho.
Shiriki uchaguzi, ukishindwa kwa sababu ya irregularities nenda mahakamani, zikithibitika utapata haki yako na hizo kasoro zitarekebishwa.
Mnaposusa uchaguzi mnasababisha demokrasia yetu izidi kudumaa.
 
Sure mkuu, tunataka kupata viongonzi waliochaguliwa na wananchi katika mfumo ulio bora wa kiuchaguzi, leo GHANA imekua kinara wa democrasia Afrika, na Mambo yanaenda vizuri ,sisi tz tunaogopa nini,? Tz yetu wote yeyote aliekubaliwa KWA kura za kutosha, kupitia tume huru,na mfumo huru, awe m/mtaa,diwani, mbunge,rais, bila kujali dini,ukabila,chama,so far ni mwananchi mwenye sifa kutoka katika jamuhur ya muungano wa tz atakua kiongozi wetu, hapa shida nini,kuwa na tume huru,na katiba mpya ,
Sahihi maana kutegemea huruma ya mtu kwa sasa ni kujiingiza kibra kisiasa
 
Kususia uchaguzi ni upumbavu.
Kama kweli kuna nia ya dhati ya kuboresha demokrasia yetu, vyama vya upinzani vina nafasi ya kufanya hivyo kwa kushiriki fursa zilizopo kwani kwa kushiriki ndipo wanapoweza kuona penye changamoto na kupendekeza maboresho.
Shiriki uchaguzi, ukishindwa kwa sababu ya irregularities nenda mahakamani, zikithibitika utapata haki yako na hizo kasoro zitarekebishwa.
Mnaposusa uchaguzi mnasababisha demokrasia yetu izidi kudumaa.
Usijtoe ufaham KWA kutukana, TZ tangu kuwepo mfumo wa vyama vingi,changamoto zimekuwepo ,na zipo wazi moja kubwa ni tume ya uchaguzi, wenda wewe na majuzi, hata chaguzi zetu jinsi zilikuwa zaendeshwa hujui,
Vinginevyo usingekuja na maneno ya maajabu ,jf sio facebook
 
Dalili zipi zitaonyesha kuwa sasa Tume ya uchaguzi ni huru?
 
Tume ya Uchaguzi ndio inatakiwa kubadilishwa vinginevyo hakuna uchaguzi. Wateue tu aende bungeni hela za kampeni wapeleke vituo vya kulelea watu wenye mahutaji maalum.
 
Exactly hakuna haja ya kushiriki maigizo .
Screenshot_20210326-224030.png
Screenshot_20210401-125515.png
 
Chama cha Demokrasia na maendeleo kimesema hakitashiriki kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma.

Hali hii imeleta sintofahamu kwa watanzania wapenda demokrasia nchini kama hiki chama kweli kinapigania kushika dola.

Ikumbukwe makamu mwenyekiti wa chadema Tundu Lisu licha ya jana kuwa live kwenye TV hakuzungumzia kabisa maendeleo ya chadema na jinsi ya kushiriki uchaguzi huo na badala yake akatumia muda wote kuwabagaza na kuwatukana watanzania wenzake wa Chato.
Screenshot_20210401-212242.jpg
 
Hawana hela, wanasingizia tume ya uchaguzi siyo huru. Pia wanajua hawatashinda kwa kuwa wananchi sasa hivi ni CCM tu na maendeleo
 
Chama cha Demokrasia na maendeleo kimesema hakitashiriki kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma.

Hali hii imeleta sintofahamu kwa watanzania wapenda demokrasia nchini kama hiki chama kweli kinapigania kushika dola.

Ikumbukwe makamu mwenyekiti wa chadema Tundu Lisu licha ya jana kuwa live kwenye TV hakuzungumzia kabisa maendeleo ya chadema na jinsi ya kushiriki uchaguzi huo na badala yake akatumia muda wote kuwabagaza na kuwatukana watanzania wenzake wa Chato.View attachment 1740700
Kinuju umeandika kachumbari
Umetuhumu
Umebeza
Umeripoti
Umekejeli
 
Nadhani ni muda muafaka sasa kila mtu kupaza sauti juu ya katiba mpya.
Kama vyama vyote vya upinzani vitasusia hizi chaguzi pia wananchi tukasusia chaguzi zote zisizo haki naimani hiyo ni njia moja wapo itakahotupeleka kwenye katiba mpya
 
Tanzania toka Magufuli alipoingia madarakani alifuta kabisa mambo ya uchaguzi, hakuna uchaguzi huko wanaenda kupiga pesa tu.

Mbunge tayari akina Mahera wanaye. Nchi imekuwa ya hovyo sana hii, wananchi hawaruhusiwi tena kuchagua viongozi wao wanabambikiwa na dola. Chadema kama wameliona hilo basi wana akili sana.
 
Utakula katiba mpya? Nenda ukafanye kazi
 
Nadhani ni muda muafaka sasa kila mtu kupaza sauti juu ya katiba mpya.
Kama vyama vyote vya upinzani vitasusia hizi chaguzi pia wananchi tukasusia chaguzi zote zisizo haki naimani hiyo ni njia moja wapo itakahotupeleka kwenye katiba mpya
Samia alisema tusahau kabisa, weiti ini 2040,aiwilu bi a Presidenti nitawaletea
 
Hawana hela, wanasingizia tume ya uchaguzi siyo huru. Pia wanajua hawatashinda kwa kuwa wananchi sasa hivi ni ccm tu na maendeleo
Kule Zanzibar walikochagua ACT, hawakuyaona maendeleo ya ziziem
 
Tanzania toka Magufuli alipoingia madarakani alifuta kabisa mambo ya uchaguzi, hakuna uchaguzi huko wanaenda kupiga pesa tu.

Mbunge tayari akina Mahera wanaye. Nchi imekuwa ya hovyo sana hii, wananchi hawaruhusiwi tena kuchagua viongozi wao wanabambikiwa na dola. Chadema kama wameliona hilo basi wana akili sana.
Kwa hiyo Magufuli aliwagaragaza akiwa hai na sasa anaendelea kuwagaragaza akiwa kaburini?
 
Back
Top Bottom