CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Kumbuka ni marufuku kwa watoto wa kambo kushiriki mchezo wa "kombolela" sasa watachezaje na wenzao?
 
Kalamu1,
Unadhani hili linawezekana? Umesahau mbunge anatakiwa kufanya siasa kwenye eneo lake? Sasa tunaelekea kwenye kila Mwenyekiti wa Kitongoji, Mtaa na kijiji kufanya siasa kwenye eneo lake!!!
 
Ulikuwa ni upumbavu kushiriki uchaguzi wa kipumbavu uliondaliwa na watu wapumbavu kuja kuleta matokeo ya kipumbavu!
Toka awali tukiwahimiza fisiemu kufuta vyama vyote ili wabaki peke yao kuepuka kuharibu rasilimali na muda wa watanzania kusaka mkate wao katika mambo yasiyo na tija.
 
Tanzania inahitaji upinzani ili kuleta changamoto kwa chama tawala kwa ajili ya maendeleo.

Pindi hawa wana CCM wanaogeuza siasa kama michezo watakapogundua kuwa upinzani umemalizwa na hawana tena cha kushangilia basi watajikuta wanashindana kushangilia vitu vya kijinga tu kama vile jinsi mfalme alivyovaa suti na kumpendeza, eventually wenye akili kati yao watagundua na kujilaumu kwa kubariki uuaji wa upinzani nchini.
Mwenzao Nyerere alyaona haya miaka 50 baada na yeye kudhani mfumo wa chama kimoja ndiyo sahihi, lakini alipokuwa nje ya utawala akagundua hypocricy iliyopo ndani ya chama kimoja, yaani watu kushangilia lolote ilimradi wapate shibe badala ya kuumizwa kichwa na mambo ya wananchi!
Anguko kubwa litafichua rasmi unafiki na yale yanayodhaniwa ndiyo na kumbe siyo...
 
Figisu na ubabaishaji katika uchaguzi serikali za mitaa ulifanywa ili kuwapitisha bila kupingwa wagombea wa CCM. Ajabu ni kuwa Chadema imejitoa ili wajitangaze washindi wa kishindo, lakini ghafla wao tena ndio wananyong'onyea na kulalama?
Vyama vingine vikiamua kuunga mkono Chadema kwenye uchaguzi litakuwa pigo kubwa kwao.
Malofa wapumbavu hawakujifunza kwenye zoezi la uandikishwaji wakazi sasa watahaha zaidi kwenye upigaji kura
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

----
WAZIRI JAFO AWASHANGAA
Baada ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.


Pia soma

NI UAMUZI BORA KABISA. VIVA CHADEMA, VIVA MBOWE.
 
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba -" Sijawahi kuona uchaguzi wa kihuni ktk nchi hii toka uhuru wa Tanganyika upatikane". Mwisho wa kumnukuu Mwenyekiti wa chama cha siasa cha CUF.

Prof. Lipumba aufananisha uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji unaoratibiwa wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iliyo chini ya Ofisi ya Rais kuwa kinachoendelea ni uchafuzi wa amani na siyo uchaguzi.

Mwenyekiti wa CUF alisema badala ya kupoteza kuandaa uchaguzi huu batili ni bora serikali ya CCM ingepeleka muswada wa mwendokasi Bungeni ili bunge hilo lenye wingi wa wabunge toka CCM wabadili sheria ya vyama vingi, nchi iwe ya chama kimoja tu kuokoa fedha za walipa kodi kujenga shule na vituo vya afya badala ya kufanya vituko vya namna hii kuviita uchaguzi wa serikali za mitaa Tanganyika.


Source: DARMPYA TV
 
DJ kanyooka anamgwaya meko balaa, yani kiufupi kaufyata sasa anawauza wenzie awamu ya pili

Awamu ya kwanza kawauza kwa EDO
Awamu ya pili anawauza kususia uchaguzi eti hatutawatambua viongozi ambao watachaguliwa yani utoto utoto tu hivi hawa si walisema hawatamtambua meko wakasusia mpaka kikao siku anahutubia bunge je leo bado hawamtambui

DJ kawauza wenzake tena CDM imernda na Dr slaa.
 
Mbowe wewe ni kiongozi wa chama cha siasa.
Lengo kuu la chama chochote ni kushika dola.

Unatakiwa kutambua kususia uchaguzi maana yake ni kuwadhulumu wananchi.
Sio kila mtaa majina yamekatwa, sasa madudu mliyofanya huko kwenu Hai unataka tuumie na tusiousika.

Hiki chama sio cha viongozi, maana ya maamuzi yenu ni kuua chama, serikali inaanzia mtaani, kama mnaona hamtendewi haki mbona ubunge mnaendelea?

Mbowe ni jipu litumbuliwe.
kama baba yako alivyo kirusi kwenye familia yako
 
Hicho chama unachosema kinajifia ndicho pia kilimtoa jasho huyo mtukufu wenu akawakusanya watendaji nchi nzima na kuwapa maagizo ambayo hata huyo Jafo anayajua.
Haki ilishapotea kabla hata ya zoezi la kuchukua fomu halijaanza.
Hahaha, CCM ndio husema ni chama kinachojifia, mimi nimechagiza tu. Soma tena utaelewa tu.
 
Hawakutaka cdm wajitoe ili wauhadae umma na dunia kuwa kuna demokrasia lakini washinde kihuni. Sasa wanajua fika umma na dunia utawajua kuwa wanabaka demokrasia, na itadhibitika kuwa nchi inaendeshwa na dictator. Wanajua fika kuwa nchi inazidi kujipaka matope kuwa haiheshimu utawala wa sheria, na madai ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi yanazidi kupata nguvu, jambo ambalo rais Magufuli halitaki kwani hana uwezo wa kushindana kisiasa. Kikubwa wanaogopa mbinyo wa kimataifa.
 
Back
Top Bottom