CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Kiuhalisia hili haliwezekani ni rahisi zaidi kutokushirikiana na diwani,mbunge au Rais kuliko hawa wenyeviti wa mitaa.

Mfumo uliopo unakulazimisha si tu uwatambue bali ushirikiane nao.

Ukienda bank kufungua account watahitaji barua ya utambulisho wa makazi.

Ukitaka kumiliki silaha kihalali lazima hao wenyeviti wahusike.

Baadhi ajira kama ulinzi.na kwa wasiowaajiriwa microfinance hazikopeshi hadi barua ya utambulisho wa makazi.

Mauziano ya viwanja na mashamba pia etc

You need a new approach,hili lipo kinadharia mno.
 
Acha kuleta mafunza yako kwenye hili jukwaa wewe!;Kichwa fuata bendera.
Upepo upi hapa tunaongea ukweli mtumishi wa bwana ukweli ni kwamba DJ kawauza wenzie

Tunaishi kwa historia

Lipumba yupi wapi
Malim sefu yupo wapi
Slaaa yupo wapi
Siasa ya tz wapinzani wanaangalia matumbo yao so mpinzani akiona kabanwa sana anaunga mkono juhudi za chama
 
Hiyo Ndio demokrasia

Kama hujajipanga unajiandaa kwa wakati mwingine

TLP itatoa ushindani Sasa
 
Safi Mbowe kacheza Kama Mchezaji wa zamani wa Moira Pele.

Seif sharrif Hamadi aliwabwaga CUF Zanzibar kwa kususa uchaguzi Zanzibar Hadi Leo hakuna mbunge Wala mjumbe wa Baraza la wawakilishi hata mmoja baada ya Seif kuifungia goli CCM

Mbowe naye kacheza mpira Safi kaifungia goli CCM la viongozi wa serikali za mitaa,vijiji na Vitongoji..Kama Seif Sharrif Hamad alivyocheza kwa niaba ya CCM na Mbowe kacheza vile vile
Mbona mnaumia nyinyi badala ya waliosusia?

Ushindani wako kiusawa ni upi kama kweli Ushindani?

Faida ya kutokupokea fomu za upinzani nini?

Nini kilichowafanya kufunga ofice ili fomu za upinzani zisipokelewe?
 
Mitaani wanachadema wanapiga kelele za faulo kuwa Kamati kuu ya chadema imeuza mechi kwa CCM .

Hivi wanamaanisha Nini?
 
Mitaani wanachadema wanapiga kelele za faulo kuwa Kamati kuu ya chadema imeuza mechi kwa CCM .

Hivi wanamaanisha Nini?
Mbona mnaumia sana ccm, chadema kujitoa badala ya kuumia wao?
 
Uko sahihi! Wanataka tuwe mishukule yao. Tuwapiganie ili wakale kuku kwa mrija huku wakijidai kuwa wanatutetea...hamna lolote!
OOOh, Yeah! Haya mambo ya kujiliza liza na kusema CCM wanatumia nguvu, halafu unajiondoa, hayafai. Unataka nani akusaidie hiyo kazi yako ya siasa? Mimi ni mkulima mbona jua likiwaka natafuta mbinu mwenyewe bila kuwalilia wanasiasa?

Wanasiasa wanataka tuwe mateka wa kazi yao. CHADEMA, ACT, pambana na CCM. Wakitoa virungu nanyi toeni virungu. hiyo ni kazi yenu!
 
Wanapenda sana kushindana ila
Wasingevuta subira, nina hakika ungepinga pia, au wengine wangepinga. Hata mimi ningejiunga katika kundi hilo kama wangejitoa mapema.
Baada ya wagombea wao kukataliwa, wamepata sababu ya kujitoa ambayo hata wewe nina hakika unaiona ipo wazi kabisa, au sio?
Hapana mkuu,kama umenisoma humu tangu siku nyingi sana napingana na CHADEMA na vyama vyote vya upinzani kushiriki chaguzi hizi ambazo kila mteule anajitahidi kuwatumia kupanda chati.

Itakuwa ni usaliti mkubwa kwa chama chochote kinachojiita cha upinzani kukubali kutumika kama mhuri.
 
NAONA WAMEWEKA MPIRA KWAPANI BAADA YA KUONA MECHI NGUMU KWAO
mechi rahisi sana shida refa yuko upande mmoja dk ya 6 kadi nyekundu 5 bado njano kibao haahahaha ila anataka mpira uendelee hahahaha
 
Mathayo 26: 31

..."Nitampiga Mchungaji na kondoo watatawanyika"

pamoja na yote yaliyotokea, mara zote nasema, Mbowe na baadhi ya viongozi wa upinzani wananufaika sana binafsi wakiwa upinzani. Kwa ufupi ajira ya Mbowe iko pale pale.
 
Moderator
Tafadharini hizi propaganda kwenye maswala muhimu kwa ustawi wa nchi.

Nadhani ifike mahala Moderators waone umuhimu wa Nidham kwa jukwaa hili tukufu

Pasiachwe watu kutupotosha kwenye mambo muhimu ya kitaifa

Pasiachwe watu kutufedhehesha kama taifa kwa threads za hovyohovyokwa katika mambo ya msingi

Mambo ya mzaha yaonekane ya mzaha. Lakini kwenyemambo muhimu Moderators lazima walinde heshima, weledi na utu wa mtanzania hapa jukwaani.
 
Mmewanyanyasa,mmewatenda isivyo sawa na haki,wameamua kuwaachia kila kitu bado mmnalalamika,kwani ninyi ni watu wa aina gani?

Mnapenda kushindana,kushindwa hamtaki.
 
Itakuwa hawana hela za kusimamia kampeni.

Hata uchaguzi mkuu itakuwa hivi. Note me!
 
Watu wa kaskazini wameanza kukatakata mahindi shambani, baadaye viongozi wakituhamasisha civil disobedience ndiyo wataanza kuuona mchezo vizuri
 
Back
Top Bottom