CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Uwezo huo hawana. Tatizo ambalo limesumbua sana upinzani kwa muda mrefu ni kuwa wanasiasa ndio wana mikakati wa upinzani. Matokeo yake haya unayoyaona mtalaumu Magufuli bure. Hawakuwa na mbinu nyingine yeyote wakati wa JK; unafikiri watapata sasa? Upinzani hauitaji mbinu nyingine tu; unahitaji uongozi mpya kabisa. Kama wangeniuliza mimi. Hapa mtazungushana hadi hawa wengine watazeeka huku mkiwaangalia; angalieni ya kina Besigye... na yaliyowakuta kina Tshikedi..
Yawezekana ni kweli kuna matatizo katika uongozi wa vyama vya upinzani lakini tatizo lao ni dogo. Kubwa kuliko yote, tuna utawala usio na hekima wala maono, uliokosa busara na weledi. Ni utawala unaofurahia ushetani, unaotaka kulieleeza Taifa gizani.

Taifa linataka mwanga, linataka utawala wa kulipeleka mbele katika nyanja zote, na siyo kuliingiza shimoni. Wenye hekima wote na wenye dhamira njema, inukeni, jiwekeni wazi na wala msijishikamanishe na uovu kwa maana baba wa uovu ni shetani.
 
Alianza Britanicca, akaja nani sijui yule, sasa kaja TumainiE, mtalialia sana mwaka huu. Na bado hamjalipa gharama ya damu za watu.

No sympathy.
Hata johnthebaptist wa Maendeleo Hayana Vyama anashangaa sababu za Wagombea wa Upinzani kukatwa.
 
hivi wewe mkuu hata kama kwa mahaba ya chama chako, yaliyofanyika unaona ni sawa? kwamba hao wapinzani tu ndo waliwekewa pingamizi, ndo hawajui kujaza fomu, ccm nchi nzima hakuna mgombea hata mmoja aliyekosea, unaona ni haki?
Mitaani wanachadema wanapiga kelele za faulo kuwa Kamati kuu ya chadema imeuza mechi kwa CCM .

Hivi wanamaanisha Nini?
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

----
WAZIRI JAFO AWASHANGAA
Baada ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.


Pia soma
KUNA POST
NILIWEKA HAPAA KUULIZA.CHADM WALIGOMA VIPI HII YA SERKL.ZA.MTAA WANASHIRIKI

HOPE SASA MMENIELEWA NAPITA TU
DOH NASIKIA.MJOMBA WANGU ALIKUWA MWN SERKL ZA MITAA.MAKA.MITANO NAE HAJUI KUANDKKA ...
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
CCM WANALALAMIKA.

unafiki wa kiwango cha juu zaidi
 
Yani Mbowe ni mbaya sana uyu jamaa ataki watu wahoji yy anapenda tuu kusitishs uchaguzi ila ubunge aachi
 
mwenyekiti wenu anataka ccm itawale milele.
Sawaa mmepewa ruhusa ya kutawala bado mnalalamika.
SASA MNATAKA NINI CCM?
 
Nakubaliana na wewe kabisa mkuu, ndio maana nikasema wenye mamlaka walishajua wakimbana yeye wanachama watatawanyika na kukosa uelekeo.

Tukirudi kwenye hili la jana, huo ndio ulikua uamuzi pekee wa kufanya? Wamekua wakifanya hivi mara kadhaa lakini madhambi na hujuma za dola dhidi yao hazitakoma.

Ni wakati nasisitiza amekitoa chama Mbali na hilo tunalithamini lakini nafikiri mawazo na mitazamo mipya inahitajika.
Wapinzani wa hapa Tanzania wanapenda na wanaweza kufanya siasa 'kivulini'. Wakibanwa kidogo hawana mbinu nyingine zaidi ya kuridi kwa wananchi kueleza changamoto na malalamiko.
 
[emoji30][emoji30][emoji30][emoji30] View attachment 1257249
Na nini matokeo ya mwisho huku mitaani au ndio tutakuwa na wenyeviti miungu watu wenye viburi visivyomithilika? au ndio wananchi hawatashirikiana na wenyeviti wao ama kinyume chake? Je mashirikiano kijamii yatakuwa kama awali pasi kujali uvyama? Je chuki hizi za kisiasa zitatupeleka wapi?
Naona giza...
Naona tunatumbukizwa shimoni...
 
Mwanakijiji hata ukibadilisha mwekiti mbowe usiyempenda huyo atakayekuja ndio atawrza kuihua mbinu Mpya ambayo Leo haipo. Hata ukibadili uongozi ujue wote watakuwa hao unaowaona hapo chadema.
Usijifoche kwenye hicho kivuli km means ipo wape uone kama hawataitrkeleza
 
Safi Mbowe kacheza Kama Mchezaji wa zamani wa Moira Pele.

Seif sharrif Hamadi aliwabwaga CUF Zanzibar kwa kususa uchaguzi Zanzibar Hadi Leo hakuna mbunge Wala mjumbe wa Baraza la wawakilishi hata mmoja baada ya Seif kuifungia goli CCM

Mbowe naye kacheza mpira Safi kaifungia goli CCM la viongozi wa serikali za mitaa,vijiji na Vitongoji..Kama Seif Sharrif Hamad alivyocheza kwa niaba ya CCM na Mbowe kacheza vile vile
Sasa c ujinga anafanya uwo ye aoni
 
Eti kwann asusiii
Wagombea wa CHADEMA wameharibu form kwa Sababu walikuwa kama mbuzi wasio na mchunga ili takiwa wapate sample ya hizo form kwanza kisha ndio wajaze ni makosa ya uongozi mbovu ambae ni Mbowe
Pia sina kumbukumbu kama Mbowe alishawahi kususia uchaguzi wa wabungu na yeye mwenyewe akiwa ni mgombea
 
Mbowe wewe ni kiongozi wa chama cha siasa.
Lengo kuu la chama chochote ni kushika dola.

Unatakiwa kutambua kususia uchaguzi maana yake ni kuwadhulumu wananchi.
Sio kila mtaa majina yamekatwa, sasa madudu mliyofanya huko kwenu Hai unataka tuumie na tusiousika.

Hiki chama sio cha viongozi, maana ya maamuzi yenu ni kuua chama, serikali inaanzia mtaani, kama mnaona hamtendewi haki mbona ubunge mnaendelea?

Mbowe ni jipu litumbuliwe.
Wewe ni intarehamwe?
Umemfunga selo, makesi kibao na umenyima fomu za uchaguzi, kirusi kiko kwako hujijui tu.
 
Ukiona waliokuwa wanatetea wameanza kuona tofauti ujue kuna shida, pole sana COMRADE, vita yako na wajibu wako uliutekeleza sana, lakini hawa jamaa hawabebeki tena.

Nikumbuka kauli ya kiongozi mmoja kwamba Vyama vinavyodai Uhuru baada ya miaka 50 ya Uhuru hugeuka vyama vya KIGAIDI
 
Mazingira yaliyopo kwasasa

1. Hakuna tofauti kati ya ccm na Dola
-Polisi, usalama wa taifa, jeshi nk wote ni ccm
-Mahakama hususan pale juu ni ccm wote
-Bunge linajiendesha kiccm 100%

2. Viongozi wa upinzani kwa ngazi tofauti
-Wanakesi za kizushi wala hazina Mashiko
-wapo Walio magerezani
-wapo waliofilisiwa biashara na Mali zao
-wapo waliopotezwa, kuuwawa, kupigwa risasi nk

3. Hakuna ushindani wa kikatiba wala kiimani, ccm Inapora chochote itakacho au kulazimisha maamuzi yoyote kwa faida yake

Mzee Mwanakijiji mkakati au mbinu zipi unazotaka wapinzani wafanye kwenye mazingira haya? Ambako, mahakama, vyombo vya dola, bunge na hata msajili wote wainaimba wimbo wakuitukuza ccm bila kuzingatia matakwa ya katiba?
Kwa ujumla tusipepese macho. Bado kidogo kila mmoja atajua na kushuhudia kuwa tumepata hasara, na bila shaka tupo katika hali kuliko kipindi chochote.

Watu wanadanganywa na rangi nzuri ya nyoka wakisahau kuwa rangi nzuri ya nyoka huashiria sumu nzuri ya nyoka, na sumu nzuri ya nyoka ni ile ya maangamizi makubwa.

Hakuna mtawala mbaya aliyeingia bila ya kusifiwa sana, hata Amini alishangiliwa sana, na waganda wakasema kwa mara ya kwanza wamepata mtawala mzuri kuliko wote waliotangulia. Wakati uliwafundisha na kuwapa alama za ufaulu katika fikra zao.

Kitu kibaya au kizuri utakijua kwa ishara za mwanzoni. Haya ya sasa yanaashiria hulka ya yale yanayojengeka.

Tumwombe Mungu atuondoe kwa amani katika njia ya uovu ambayo tumewekwa bila kujitambua, na kwa sauti kubwa tunaimba na kujisifu kuwa tupo katika usahihi.
 
Political is a game of Chance, wacha CCM na Vyama vingine vitumie hiyo kama Fursa..
Mbowe wewe ni kiongozi wa chama cha siasa.
Lengo kuu la chama chochote ni kushika dola.

Unatakiwa kutambua kususia uchaguzi maana yake ni kuwadhulumu wananchi.
Sio kila mtaa majina yamekatwa, sasa madudu mliyofanya huko kwenu Hai unataka tuumie na tusiousika.

Hiki chama sio cha viongozi, maana ya maamuzi yenu ni kuua chama, serikali inaanzia mtaani, kama mnaona hamtendewi haki mbona ubunge mnaendelea?

Mbowe ni jipu litumbuliwe.
 
mechi rahisi sana shida refa yuko upande mmoja dk ya 6 kadi nyekundu 5 bado njano kibao haahahaha ila anataka mpira uendelee hahahaha
SI HAMJUI KUCHEZA MPIRA VIZURI ACHA MLE KADI ZA KUTOSHA
 
Back
Top Bottom