Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Yawezekana ni kweli kuna matatizo katika uongozi wa vyama vya upinzani lakini tatizo lao ni dogo. Kubwa kuliko yote, tuna utawala usio na hekima wala maono, uliokosa busara na weledi. Ni utawala unaofurahia ushetani, unaotaka kulieleeza Taifa gizani.Uwezo huo hawana. Tatizo ambalo limesumbua sana upinzani kwa muda mrefu ni kuwa wanasiasa ndio wana mikakati wa upinzani. Matokeo yake haya unayoyaona mtalaumu Magufuli bure. Hawakuwa na mbinu nyingine yeyote wakati wa JK; unafikiri watapata sasa? Upinzani hauitaji mbinu nyingine tu; unahitaji uongozi mpya kabisa. Kama wangeniuliza mimi. Hapa mtazungushana hadi hawa wengine watazeeka huku mkiwaangalia; angalieni ya kina Besigye... na yaliyowakuta kina Tshikedi..
Taifa linataka mwanga, linataka utawala wa kulipeleka mbele katika nyanja zote, na siyo kuliingiza shimoni. Wenye hekima wote na wenye dhamira njema, inukeni, jiwekeni wazi na wala msijishikamanishe na uovu kwa maana baba wa uovu ni shetani.