CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Wapinzani wa hapa Tanzania wanapenda na wanaweza kufanya siasa 'kivulini'. Wakibanwa kidogo hawana mbinu nyingine zaidi ya kuridi kwa wananchi kueleza changamoto na malalamiko.


Na kwakuwa hicho hakihatarishi kibarua chao, wanaona sawa tu. Ndio msingi hasa wa nilichokisema kuwa, kuna baadhi ya viongozi wananufaika zaidi wao binafsi kwa kuendelea kuwa wapinzani. Nia yao sio kushika dola. Upinzani ni ajira bora zaidi kwao.
 
hivi wewe mkuu hata kama kwa mahaba ya chama chako, yaliyofanyika unaona ni sawa? kwamba hao wapinzani tu ndo waliwekewa pingamizi, ndo hawajui kujaza fomu, ccm nchi nzima hakuna mgombea hata mmoja aliyekosea, unaona ni haki?
Kujaza fomu sio mtihani kuwa kila.mmoja anajaza chumba Cha mtihani peke yake kiasi kuwa useme Kama upinzani walikosea na CCM lazima wakosee.

Fomu mtu alikuwa hajazii hapo hapo ofisini alikuwa anapewa aondoke nayo akale nayo siku za kutosha lengo.likiwa awe na muda wa kujaza kwa usahihi.Kama kina kitu haelewi arudi hata kuuliza au aombe msaada kwa Wana Chama wenzie wamwelekeze au hata ndugu zake hata mawakili wamsaidie kumwelewesha.Hawakufanya.

CCM ilifanya semina elekezi za kujaza hizo fomu na ikawataka viongozi wa mataei wadimamie ujazaji.hizo fomu kujakikisha haikosewi hata nukta kujaza.

Kwa hiyo.mtu alikuwa akichukua fomu anaenda kwenye tawi.lake viongozi wa CCM wanamzunguka wakiwa wamekaa naye kuhakikisha anajaza vizuri bila kukosea.Sababu CCM ilionya fomu yeyote itakayojazwa vibaya uongozi wa tawi wote utachukuliwa hatua.

Upande wa upinzani.mtu alikuwa akichukua fomu anaenda kujijazia anavyojua mwenyewe wnarudisha.Hawakupewa semina elekezi Wala usaidizi.Zao zikarudi na mikosa kibao za CCM zote safi
 
Roving Journalist,
HIVI HIKI CHAMA BADO KIPO

Maana nasoma hidaya za msajili hakijafanya Uchaguzi Mkuu unaotakiwa huko kwingine wanajua wenyewe. Mh ..rudi tu ukaungane na CCM hakuna jinsi. Sasa chama kila siku kinakimbia uchaguzi kinasubiri ruzuku tu ooh no msajili embu fuatilien na hizi rizuku
 
Wakati muafaka sasa kuangalia na upande wa hizi ruzuku za Vyama vya Upinzani. Kama kila chaguzi wanakimbia je, wanastahili kuendelea kupewa ruzuku?

Sidhani
 
Iko hivi. Hawa jamaa baada ya kuona kasi ya Rais Magufuli kwenye maendeleo ya nchi na watu wake haikamatiki basi wao wakaja na mkakati wa values za kiliberali ambazo hakika kwa nchi yetu sio kipaumbele kama kuboresha na kuendeleza hali ya kiuchumi na kijamii ya watu.

Wanajidai wanapigania uhuru wa kutoa maoni na kujieleza wakati ni kisingizio waweze kufanya uchochezi dhidi ya serikali wanapinga wazi sera za ujenzi wa nchi za kupambana na unyonyaji wa ndani na nje kwa kufadhiliwa na hao mabeberu. Bahati nzuri wananchi wameliona hilo wanaunga mkono kwa asilimia kubwa na CHADEMA ila kufanya usanii jinsi ia mitini bila kuabika kwenye uchaguzi
 
Hiyo Ndio demokrasia

Kama hujajipanga unajiandaa kwa wakati mwingine

TLP itatoa ushindani Sasa
 
WAKATI.MUAFAKA SASA KUANGALIA NA UPANDE WA HIZI RUZUKU ZA VYAMA VYA UPINZANI

KAMA.KILA CHAGUZI WANAKIMBIA JE WANASTAHILI KUENDELEA KUPEWA RUZUKU

SIDHAN
Kama play field haiko level,hata wewe ungekimbia.
 
Kaka! Uko serious kweli? Mshindani mwenzako akipe nafasi sawa yakushindana nae? Haya ni mapambano, ukiingia ulingoni na mtizamo kwamba adui sometimes atakuwa anakupa offer nawewe upige moja kwakuwa amekupiga tatu mfululizo....ni hakili za ajabu mno! Siasa ni ujanja, ubunifu etc. Unategwa na kitu kidogo sana KANUNI! Na unaingia mwenyewe! UBUNIFU HUO.
Kuelewa ndio shida...unajua maana ya haki sawa.. ndio maana hata mabondia wanapimwa uzito..hata timu za mpira zina idadi ya wachezaji sawa..usiandike kwakua una bando!!!
 
Mzunguko mrefu akili kubwa ya mbowe imefanikiwa tatizo ni pesa chama hakina pesa jamani kikitangaza hakuna pesa kitazua ya kuzua na kuanzisha tafrani ni bora hii akili iliyotumiwa..
 
CCM, hii nchi mnakoipeleka, haitorudi tena, hata Sierra Leone walianza hivi hivi Kisha kikanuka.
⚠️⚠️⚠️
 
Hakuna mkakati wa aina hii bali wanapambana na mbinu za medani za kisiasa kutoka CCM zinazoitwa suffocating tactics
 
Back
Top Bottom