Kuna siku unazo acha akili zako nyumbani na kuna siku unatembea na akili zako.Leo umetembea na akili zakoKuna makada wengine wa CCM siyo kwamba wanakurupuka bali hawafikirii sawasawa wakati wa kufanya maamuzi.
Mbona bendera za Yanga na Simba zimezagaa kila kona katika manispaa ya ubungo na hatujasikia katazo lolote.
Binafsi nitamuona DED wa ubungo kidume kama atazishusha bendera za Yanga.......za Simba najua ataweza maana ni wahindi wala dengu wale.
Maendeleo hayana vyama!
Zinamkera Mwenyekiti hivo anaogopa utumbuzi.Angeweka na kifungu cha sheria cha kuzitoa
Mwambieni akatafute solution barabara hazipitiki aache siasa za kipumbavu kwa muda huu
CCM ni chama dolla, kimepoteza mvuto hakina tena ushawishi wa kuwatongoza/shawishi/enfluence wanachama wapya chenyewe kinategemea dolla ili kiweze kujinufaisha. kama unaogopa mpaka bendera za chama ambachokila siku mnasema kinakufa 2020 huo ni nini kama sio ujuha
Inajenga picha kuwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasiaHilo ni eneo la kibiashara lisigeuzwe la kisiasa
Watu kutoka mataifa mbali mbali wanafika pale
Je itajenga picha gani kwa Nchi yetu?
Tuache siasa
Wewe hujui kuwa MM anatafuta uteuzi toka kwa Jiwe??Halafu ndi linasimama jitu moja linasifia kuwa JOGOO LA SHAMBA limewika mjini.....upumbavu mtupu
Ifike mahala watanzania tuache kupinga pinga kila kitu.
Mkurugenzi yupo sahihi kabisa, hizo bendera za CHADEMA ndiyo zimesababisha hizi mvua na mafuriko haya Dar.
Ni mvua hizo zilizosababishwa na hizo Bendera zimesababisha Mkurugenzi aache kutembelea maeneo na wahanga na kuongelea uharibifu uliosababishwa, badala yake wamesababisha aende maeneo zilipowekwa hizo bendera na kurudi kukaa ofisini kuwaandikia barua za maelekezo CHADEMA kwa tabia zao.
Kama ndio hivi basi aliyetakiwa kutoa tangazo la kuzishusha ni hao wahusika uliowataja, wote hao (Tanroad na Tarura) hawako chini ya DEDWana kibaki Cha kuzifunga kwa wamiliki wa nguzo na miti? Kwani nguzo na barabarani wanamoweka Ni Mali yao?
Barabara ni.mali ya Tanroads na Tarura wamepata kibali?