CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

Kuna makada wengine wa CCM siyo kwamba wanakurupuka bali hawafikirii sawasawa wakati wa kufanya maamuzi.

Mbona bendera za Yanga na Simba zimezagaa kila kona katika manispaa ya ubungo na hatujasikia katazo lolote.

Binafsi nitamuona DED wa ubungo kidume kama atazishusha bendera za Yanga.......za Simba najua ataweza maana ni wahindi wala dengu wale.

Maendeleo hayana vyama!
Kuna siku unazo acha akili zako nyumbani na kuna siku unatembea na akili zako.Leo umetembea na akili zako
 
Hichi Kilevi ni Balaa ,CCM wame lewa chakari na kuona Nchi ni yao kiasi wanawaza kuitia Mfukoni.
IMG-20191009-WA0009.jpg
 
Wamelipia? Isotoshe wanaweza kwenda Mahakamani kama wameonewa, mimi nakereka kuwaona hivyo wanaingilia uhuru wangu wa kuangalia, chadema OUT of Town!
 
Kawe Alumni,
Hizo bendera zinawazuia hao wageni kupata huduma zao? Kwani hao wageni hawawezi kuuliza na kuambiwa kuna shughuli maalum? Ingekuwa ni shughuli ya kuhatarisha amani, au hizi bendera zinaashiria vita hapo sawa. Ni hivi, awamu hivi ya tano inalazimisha kuiua cdm, lakini CHADEMA imeishaingia kwenye akili za watu haifi kwa kufanyiwa hujuma na taasisi za kimamlaka.
 
Mwambieni akatafute solution barabara hazipitiki aache siasa za kipumbavu kwa muda huu

Mambo muhimu hawawezi hawa labda yahusuyo wapinzani. Anashindwa shughulika na kero anasumbuliwa na bendera
 
Ni kweli wanatakiwa waziondoe maana zinaweza zikaibwa na wakora kwa jinsi zinavyopendeza
 
Tatizo sio kwa mujibu wa sheria, tatizo ni kujua SHERIA IPI? Nina uhakika Madam Mkurugenzi hajakurupuka.
 
Ifike mahala watanzania tuache kupinga pinga kila kitu.
Mkurugenzi yupo sahihi kabisa, hizo bendera za CHADEMA ndiyo zimesababisha hizi mvua na mafuriko haya Dar.
Ni mvua hizo zilizosababishwa na hizo Bendera zimesababisha Mkurugenzi aache kutembelea maeneo na wahanga na kuongelea uharibifu uliosababishwa, badala yake wamesababisha aende maeneo zilipowekwa hizo bendera na kurudi kukaa ofisini kuwaandikia barua za maelekezo CHADEMA kwa tabia zao.

Una Hoja ya Msingi sana Mkuu。
 
Wana kibaki Cha kuzifunga kwa wamiliki wa nguzo na miti? Kwani nguzo na barabarani wanamoweka Ni Mali yao?
Barabara ni.mali ya Tanroads na Tarura wamepata kibali?
Kama ndio hivi basi aliyetakiwa kutoa tangazo la kuzishusha ni hao wahusika uliowataja, wote hao (Tanroad na Tarura) hawako chini ya DED
 
Wakuu nimepita hapa mlimani City muda huu naona Polisi na wanachama wa CHADEMA wanazozana ila naona kimtindo bendera zinashushwa na hao hao Polisi.

#Wenyeviti wa CCM wajao baada ya kustaafu ukamanda.
IMG_20191217_192148.jpg
 
Back
Top Bottom