CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

Niliwahi kusema muda sana na nimekuwa nikisema, jiwe anawaonea wivu cdm kwa jinsi wanavyokubalika na wananchi, na ndio sababu hasa amepiga marufuku vyama vya siasa kufanya kazi za siasa nchi nzima kwani anajua fika cdm wanakubalika, na hilo linamuumiza sana roho yake. Alitamani jinsi cdm inavyokubalika ndio iwe yeye na ccm. Namna pekee ameami kutumia nguvu kubwa na uonevu wa wazi dhidi ya cdm, akidhani akiiua cdm basi automatically watu wataipenda ccm, kitu ambacho hakiwezekani.

Imagine CHADEMA ingekuwa iko huru kufanya kazi zake kama katiba ya nchi isemavyo, mizengwe na chuki zidi yake zisingekuwepo jee ccm na Magufuli wangekuwepo katika siasa kweli?
Ni wazi ingesha jiishia na yeye pengine angeachia ngazi kwa shinikizo la afya kwani mchaka mchaka huo asinge uweza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zimeanza bendera kuwekewa ribiti na Halmashauri ya Ubungo, na kwa vile mkoa nao haujaingilia kati kama wakati wa marufuku ya Sophia Mjema na ibada za kila siku basi mkoa umeridhia kuwa bendera za Chadema ni tishio kupepea kwa tashwishwi eneo lote la Mlimani.
Hizo ndio figisu za utawala dhidi ya Chadema, lakini figisu hizo ndizo zinaipaisha Chadema kila siku.
Nawaomba wakae chonjo, kwa figisu za namna hiyo wasije kushangaa kesho kuwakuta Polisi wametapakaa eneo la Mlimani city na maagizo kuwa wakachukue fedha zao maana ukumbi umepata shughuli zingine.
Waandae kabisa plan B iwapo hilo litatokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watahamia ukumbi wa Mbezi beach high school
 
View attachment 1295323

Huyu Mheshimiwa anaitwa Beatrice Dominic , ameingia kwenye rada zetu baada ya kufanya kituko cha kuamuru kushusha bendera za Chadema zilizowekwa kwenye maeneo ya Mlimani City kunakofanyika Mkutano mkubwa wa uchaguzi wa chama hicho , kama walivyo watumishi wengine wa Umma tunapaswa kuufahamu wasifu wake , ni wapi aliposoma , alisoma shule gani , alisomea nini , mahali pengine alipofanya kazi , alikuwa na cheo gani , uaminifu wake pote alipopita na mengine mengi ambayo mtumishi wa umma anapaswa kuwa nayo .

Lengo kuu la kutaka kumfahamu ni kuweka kumbukumbu sawa kwa ajili ya vizazi vijavyo
Me nafamu kuwa anajua kusoma na kuandika na mwanachama wa mtiifu wa ccm.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka wasifu wa nini, mbali ya kujua kwamba huyo ndie atakayesimamia uchaguzi. Hapo mna kitu kweli?

Wakati huu mngekuwa mnajenga hoja kwa ushahidi kama huu ulio wazi kukataa kabisa hawa watu wasimamie uchaguzi.
Hiyo mahakama imekwisha wapiga chini, mnazo mbinu gani zaidi ya hapo?

Utaingiaje kwenye uchaguzi ukijua wazi huna utakachoambulia kwa sababu ya uwepo wa watu kama hawa?

Erythro haya ndiyo maswali yanayohitaji kufanyiwa kazi mara tu baada ya kuwapata viongozi wenu wapya.
Kesho Mkutano Mkuu , tumealika mabeberu wote .
 
Yuko sahihi!! Tusipige kelele bila kujiuliza sheria za matangazo mitaani zinasema nini. Huwezi weka matangazo bila kibali na huenda hata kulipia. sasa wao waliweka kwa kulipia? Kwa muda gani?
 
Back
Top Bottom