CHADEMA yapoteza ushawishi mitaani. Sare zake hazivaliki

Huo ushawishi umeupimaje wakati serikali inazuia mikutano ya hadhara!?
Uungwaji mkono wa CCm kutoka kwa vijana Ni mkubwa Sana kuanzia kuongezeka kwa wanachama wanao chukua kadi za CCM katika ofisi za chama na hamasa ya vijana Katika chaguzi za ndani ya chama
 
inakuwaje mwanaume kama kweli wewe ni rijali kabisa, unapoteza muda wako kuandika vijembe vya kipuuzi namna hii ilhali unajua vyama vingine vyote vya siasa vimezuia kufanya shughuli za siasa? Kichwa chako kiko sawa kweli wewe?
 
Katika suala la mazingira Ni wajibu wetu sote kuyatunza na kuyalinda, lakini pia suala la ushawishi Ni ukweli ulio wazi kuwa CCM Ina ushawishi mkubwa Sana kwa vijana
Pamoja na wajibu wa mwannchi ktk mazingira, ni WAJIBU MKUBWA SANA wa serikali kuweka sera na mipango mizuri ya kumwongoza huyu mwanchi, na Ndiyo maana ikawepo serikali ili kuratibu.

Lakini pia jibu swali Je wewe kama kada hauoni kuwa mtwara tuliumizwa na kupewa vilema bure mkituaminisha kuwa gesi yetu itakuwa mkombozi kwa taifa letu? Je matokeo yake yako wapi? Tupe majibu kada wewe.

Kama gesi ingeratibiwa ktk sera nzuri leo hii tusingekuwa tunakata miti ovyo kwa matumizi ya nishati na hapa ndipo ccm
mlipochangia Sana ktk kuharibu mazingira.

Kuhusu ushawishi unazungumza maneno matupu, onesha mifano ya ushawishi ulioleta tija unaofanywa na uvccm mahali popote, zaidi tu utawakuta uvccm kazi yao ni kuandaa matamko ya kusifia matukio yanayo fanywa na viongozi wa serikali.

Nimekupa mfano hai wa viongozi wengi waliogombea ngazi za kata, hiyo ndiyo picha inayotoa mtazamo wa chama kama kweli kina mvuto au laa!
 
Ipo siku utajikuta umechanganyikiwa na Chadema, ongopa Sana chama ambacho tiyari kimekua imani ndani ya nyoyo za watu, level hii haitaji kuvaa sare n.k, nakupatia siri hii,
 
Ipo siku utajikuta umechanganyikiwa na Chadema, ongopa Sana chama ambacho tiyari kimekua imani ndani ya nyoyo za watu, level hii haitaji kuvaa sare n.k, nakupatia siri hii,
Chadema haipo katika mioyo ya watanzania kwa Sasa ndio maana unaona haiungwi mkono katika azimio lolote lile au tamko lolote lile inalolitoa kwa watanzania
 
mbona baba yako anavaa sare za Chadema?
 
mbona baba yako anavaa sare za Chadema?
Hakuna mwenye Akili Timamu anayeweza kuvaa masare ya Chadema kwa Sasa , maana unakuwa unajiaibisha tu kwa kuonekana tapeli tapeli tu, si unaona pesa za michango zinavyotafunwa na viongozi wa chadema, Kama huamini tupe hesabu na kiasi kilichokusanywa kupitia join the chain, tuambie hela hizo zipo wapi kwa Sasa, Tuambie pesa za akina Sabodo Nani alizitafuna
 
inakuwaje mwanaume kama kweli wewe ni rijali kabisa, unapoteza muda wako kuandika vijembe vya kipuuzi namna hii ilhali unajua vyama vingine vyote vya siasa vimezuia kufanya shughuli za siasa? Kichwa chako kiko sawa kweli wewe?
Nataka unijibu Kama ulishaona Marekani wakishamaliza uchaguzi wao wale walioshindwa wanaanza kuzurula zurula mitaani Kama nyinyi chadema mnavyofanya hapa nyumbani,
 
Mwalimu vipi umeshindwa kuona hoja zote hizo, nimezungumzia habari za Sera, ajenda,hoja ambazo chadema haina na kupelekea kukosa dira na muelekeo,
Mbona unakwepa kujibu hoja zingine, nimekuuliza uje hapa kutupa majibu ya sera mbovu za mazingira pamoja na gesi ya mtwara.

Je ni wapi mtaani unaona ccm wamevaa sare kama siyo kwenye mikutano yao, chaguzi au mapokezi ya viongozi?

Kama vyama vingine vingekuwa vinaruhusiwa kufanya siasa kama sheria inavyotaka ungeziona sare za vyama hivyo maana sare za siasa huvaliwa ktk siasa.

Hii kazi unayojipa bado hauwezi màana wewe inaonekana ni miongoni mwa wale viongozi wa kata wasio na weledi wa masuala ya kijamii na siasa kwa ujumla.
 
Nataka unijibu Kama ulishaona Marekani wakishamaliza uchaguzi wao wale walioshindwa wanaanza kuzurula zurula mitaani Kama nyinyi chadema mnavyofanya hapa nyumbani,
umethibitisha nilichoandika. marekani inaingiaje kwa kile ulichoandika? Sikukosea, hauko sawa kichwani.
 
umethibitisha nilichoandika. marekani inaingiaje kwa kile ulichoandika? Sikukosea, hauko sawa kichwani.
Kwani nani kakwambia kuwa Tanzania Ni kisiwa? Hufahamu hata sheria au baadhi ya vitu huwa tunabeba kutoka kwa wenzetu pale tunapoona vinaweza kuleta manufaa na faida kwa Taifa letu? Au unafikiri Taifa letu lipo katika sayari yake ya kujitegemea?
 
Ya ngoswe muachie ngoswe..wewe komaa na ccm yako bro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…