CHADEMA yatangaza kumwaga mishahara kwa watendaji wake wote kuanzia ngazi ya chini Kabisa

CHADEMA yatangaza kumwaga mishahara kwa watendaji wake wote kuanzia ngazi ya chini Kabisa

Kauli hii ya kishujaa imetolewa na Mwamba Mwenyewe Freeman Mbowe alipokuwa anahitimisha mpango wa Operesheni Haki Mkoani Morogoro .

Mbowe ambaye sasa anaitwa Mtemi Isike , baada ya kusimikwa huko Tabora , amesema kwamba Chama chake sasa kinataka viongozi wake wafanye kazi moja tu ambayo ni kusuka chama kwa kukusanya wanachama wapya na kuhudumia wanachama wake 24/7 , hivyo ni lazima wapewe vitita vizito kila mwezi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi .

Kwa kadri ya kumbukumbu zangu CHADEMA yaweza kuwa ndio Chama cha kwanza cha kisiasa nchini Tanzania kuwalipa wafanyakazi wake wote hadi wa ngazi ya chini kabisa Mshahara , vyama vingine watendaji wake wengi huishi kwa kutegemea RUSHWA ZA WAGOMBEA WAKATI WA CHAGUZI za ndani au Uchaguzi Mkuu .
Mungu ibariki CHADEMA
 
Mbowe hatasamehewa na watanzania kwa kitendo chake cha kuangushwa na konyagi alafu akaitangazia dunia amepigwa na wasiojulikana ili kumchafua mwendazake.

Uongo uongo tu
Mkuu, wanaita Faru Joni.
 
Kama tulishindwa kutoa mishahara kipind kile tukipata ruzuku kubwa tutaweza Sasa kweli na je zoez litadumu kwa mda gani?

Chama changu nakipenda Sana lakn kwa hili mh?
Wafadhili hawakosekanagi ukiwataka.
 
Chadema wanapata wapi hizo hela?
Swali la kizalendo hili naamini.
 
Wafadhili hawakosekanagi ukiwataka.
Wafadhili ni kweli hawakosekani hasa Ulaya ambako wanaamini Afrika iliyostaarabika inaweza kuwa makazi yao au paradiso yao hapo baadae.
Wanafadhili kwaajili yao wenyewe,, sisi waafrika tungeacha ubinafsi tungeweza kutumia hizi fursa vizuri na kujenga nguvu zetu za kiuchumi.
Lakini tunanunulia madem zetu magari mazuri, tunawapangishia nyumba za bei kubwa.
Ubinafsi unatumaliza Afrika.
 
Dogo huwezi kusema humkubali Lowasa wakati huo huo unamsujudia Mbowe aliyemleta
Tafuta popote nilipowahi kumsifia Lowassa akiwa Ccm kisha kwenda cdm na kurudi ccm, kama kuna mahali popote niliwahi kulisifia lile zee tapeli la kisiasa. Ukiona popote nilipowahi kumsifia Lowassa, au takataka yoyote toka ccm akiwepo Sumaye, Nyalandu nk nipigwe ban ya mwaka mzima. Unanichukulia poa nini?
 
Misukule ya Mbowe, ina kazi sana, yaani Mbowe akitamka kitu, basi hata kuwaza kidogo tu hamuwezi, is it possible? Wenyewe sbb ni misukule basi kazi kuamini tu na kuchapisha mitandaoni.. Mbowe wakati anapata ruzuku kwa miaka anakula yeye na hakuna wa kumuuliza na alishindwa kulipa mishahara, leo hana ruzuku ndio alipe mishahara? Hivi nyie Chadema ni kuwa akili hakuna hata kidogo, mmefanywa misukule kabisa na Form 6 div 0 kweli?
 
Huu ni uongo mwwupe kbs - atuambie analipa kiasi gani kwa viongozi wa matawi, kata, wilaya, mkoa, kanda na taifa. Aseme ana matawi mangapi, kata na wilaya ngapi pia

CDM hawakuwahi kuishiwa vioja
 
Hizi taasisi za kisisasa za kipuuzi sana.

Classmate wangu alijitoa sana kwa chadema, alitumia pesa zake mpaka pikipiki yake kwaajili ya chadema kilichomtokea mpaka leo jamaa amekua mlevi mbwa.

Miaka zaidi ya mitatu tangu wamharibie maisha eti leo kuna tangazo la kuanza kulipana mishahara halafu huyu mwingine analileta kwa mbwembwe zote.

Manina.
Ulevi wa rafiki yako chadema wanahusika?
 
Naona tunaleta mbwembwe kama za abunuasi.

Yaani kulipa mishara watendaji wa chama na kuimarisha chama?

Kama hata ofisi tu tumeshindwa ndio tutaweza kufanya haya?

View attachment 1815280

View attachment 1815307
Chadema hajengi chama kwa kufuata mfano wa ccm ambao wao wanaamini kujenga chama ni kua na ofsi zenye majengo maxuri chadema inajenga chama kwenye mioyo ya watu na ndio maana mwanachadrma ambae hakutoka chama kingine ni ngumu kumubadilisha mawaxo na huumia chama chake kikisemwa vinaya
 
Mwaka 2010-2015 Ruzuku ya CHADEMA ilikuwa inasoma zaidi ya milioni 300 kwa mwezi lakini hakukuwa na mishahara na iliishia DAR.

Mwaka 2015-2020 ikapanda mpaka milioni 450 kwa mwezi na hali ikawa vile vile.

Leo hawana Ruzuku ndio watoe mishahara 🙄🤣

Anyway, itakuwa ni mbinu ya kuwapush viongozi wa chini ili wajitume kuandikisha wanachama kwenye kadi zao ili pesa ipatikane.

Ndio maana wanasema mpaka ukiandikisha mtu na wewe unapata 500. Sasa hivi ni pesa mbele kwa mbele.

Kwa 2,500 wakipata wanachama 2M tayari hiyo ni billion kadhaa.
 
Huu ni mwanzo mzuri.. kwasababu sisiM ikiongozwa na Jiwe ilifanya jitihada kubwa kuwek chama kushika madaraka kwenye nafasi za ubunge na udiwani.. Bunge limetawala Kijani tu Lakini kama hawa wabunge hawatakuwa makini 2025 tunaweza tusiwaone kwenye viti vyekundu pale Dodoma! sisi wananchi tuna ona yote yanayofanyika pale
 
Kauli hii ya kishujaa imetolewa na Mwamba Mwenyewe Freeman Mbowe alipokuwa anahitimisha mpango wa Operesheni Haki Mkoani Morogoro.

Mbowe ambaye sasa anaitwa Mtemi Isike, baada ya kusimikwa huko Tabora , amesema kwamba Chama chake sasa kinataka viongozi wake wafanye kazi moja tu ambayo ni kusuka chama kwa kukusanya wanachama wapya na kuhudumia wanachama wake 24/7 , hivyo ni lazima wapewe vitita vizito kila mwezi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Kwa kadri ya kumbukumbu zangu CHADEMA yaweza kuwa ndio Chama cha kwanza cha kisiasa nchini Tanzania kuwalipa wafanyakazi wake wote hadi wa ngazi ya chini kabisa Mshahara, vyama vingine watendaji wake wengi huishi kwa kutegemea RUSHWA ZA WAGOMBEA WAKATI WA CHAGUZI za ndani au Uchaguzi Mkuu.
Huko CCM hata mwenyekiti wa CCM mkoa,wilaya,Kata,na vijiji hawalipwi mshahara hata Senti tano.sijui wanaishi vipi na wanakula wapi na wanatunzaje familia zao. Ni fedhea na aibu kubwa kubwa kwa chama kilichozaliwa mwaka 1977 na ndicho chenye Dola. Mabalizi hawalipwi,wajumbe wote hawalipwi. Mwenyekiti wa CCM Taifa Naye halipwi mshahara ndani ya chama Wala wakuu wa jumuia zake wote hawalipwi. Hii ni aibu kubwa tena kubwa. Kuna uwezekano viongozi hao wanaishi kwa njia ya Rushwa na kwa kigezo hicho Rushwa nchini haitakaa iishe kamwe.
 
Back
Top Bottom