Kauli hii ya kishujaa imetolewa na Mwamba Mwenyewe Freeman Mbowe alipokuwa anahitimisha mpango wa Operesheni Haki Mkoani Morogoro .
Mbowe ambaye sasa anaitwa Mtemi Isike , baada ya kusimikwa huko Tabora , amesema kwamba Chama chake sasa kinataka viongozi wake wafanye kazi moja tu ambayo ni kusuka chama kwa kukusanya wanachama wapya na kuhudumia wanachama wake 24/7 , hivyo ni lazima wapewe vitita vizito kila mwezi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi .
Kwa kadri ya kumbukumbu zangu CHADEMA yaweza kuwa ndio Chama cha kwanza cha kisiasa nchini Tanzania kuwalipa wafanyakazi wake wote hadi wa ngazi ya chini kabisa Mshahara , vyama vingine watendaji wake wengi huishi kwa kutegemea RUSHWA ZA WAGOMBEA WAKATI WA CHAGUZI za ndani au Uchaguzi Mkuu .