Chakula au vitu gani huwezi kuacha kula hata kama ukiwa Bilionea?

Chakula au vitu gani huwezi kuacha kula hata kama ukiwa Bilionea?

Ha ha ha ha ha ha ha

Mimi ugali kwa majani ya maboga yaliyowekwa karanga au unga wa mbegu za maboga au majani ya maharage yaliyowekwa karanga sitaweza acha kula kabisa.
Majani ya maboga huku Tabora tunayaita msusa acha kabisa kwa karanga yananoga sana
 
Vyakula vya kiafrika uchafu mtupu. Ugali maharage sijui na mlenda ukimpa nguruwe wa US hali.
 
Ugali na mlenda.

Mtori na chapati 1

Ugali na dagaa rosted ukimix na tubamia, kakiazi na vinyanya chungu.

Wali maharage na kachumbari
mtori na chapa rohoo 1

chapa rohoo zikiwa 2 unasusa kula😅
 
Back
Top Bottom