Changamoto katika ujenzi: Mafundi uchwara wanavyoharibu kazi

Mkuu nahisi nimedhulumiaa nifanyaje?
 
Dawa ni kwenda mwenyewe kichwa kichwa kuhemea vifaa na usimshirikishe.

Kazi yake yeye ni kutaja vifaa vinavyohitajika, halafu mahemezi unazama dukani mwenyewe.
 
Lakini nimiwa na wale jamaa zako wa kilingeni sii wanaweza nilindia nyaya zangu bila kuwepo mtu
Utapigwa halafu utapigwa tena😂 vilinge vya siku hizi havina totauti na lile joka la kibisa
 
Hapo ndiyo dawa yao vinginevyo lazima wapige cha juu.
Hilo waweza kulidhibiti, lakini katika ujenzi kuna wizi wa kila aina usipokuwa makini.

Je unajua kuwa mota(tope)la saruji iliyochanganywa na mchanga tayari kwa ujenzi kuwa inauzwa na mafundi?

Je waelewa marundo ya mchanga kwenye site yako ni store ya kuhifadhia saruji na vifaa vingine vilivyoibwa vinavyosubirishwa kuondoshwa?

Je wajua kuwa vipande vya tofari pamoja na misumari iliyododoka katika kupaua inatafutwa kama sukari?

Je wajua kuwa saruji iliyokwisha kufumuliwa kwenye mifuko huuzwa kwa kupima kama chumvi?

Je wajua vipande vya mabati vinavyoonekana kutofaa kwa kazi yoyote hapo kwenye ujenzi wako kuwa ni pesa ya chap chap?

Je wajua pia kuwa siku ya kupaua ndiyo siku ya kukuibia bati zako utake usitake: Bati zilizopangwa kuvushwa hushikizwa ndani ya paa ya dari hata ukichungulia ni ngumu kubaini, usiku mafundi hurejea na kuzihamisha?

Mkuu, unapoanza ujenzi jitoe hasa kusimamia mwenyewe, usitume mtu kusimamia kwa niaba yako, hata mkeo hapana maana kuna ujanja mwingi sana wa wizi na upotoshaji wa manunuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…