MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
NATO wamecheza mchazo mkali sana wa kisiasa dhidi ya MRUSI.
Mosi, wameanzisha mtafaruku Lebanon kwa kumtumia mshirika wao mkubwa Israel, jambo ambalo limepelekea vikosi vingi vya Hizbullah kuondolewa nchini Syria na kurudishwa Lebanon kuzuia uvamizi wa Israel. Jambo hili limechangia kwa kiasi kikubwa Syria kukosa ulinzi katika eneo la Aleppo.
Pili, NATO kutumia mwanachama wake Turkey wamefanya shambulio zito dhidi ya Syria kwa kutumia mgongo wa makundi ya waasi na makundi mengina ya kigaidi. Jambo hili limewaweka Warusi na Wairani njia panda kwasababu kwasasa Iran anasaidia washirika wake Hizbullah kupambana nchini Lebanon, hivyo ni ngumu kurudisha au kuvigawanya vikosi vya Hizbullah baina Syria na Lebanon kama ilivyokuwa mwaka 2015 ambapo vikosi vya Hizbullah vilijazana nchini Syria.
Tatu, Urusi ndiye aliyetoa mchango mkubwa kwa Syria mwaka 2015 ili Assad asipinduliwe. Kipindi hiki yuko kwenye wakati mgumu kwasababu hawezi kutuma vikosi vyake ilhali yuko anapambana na Ukraine na NATO kule Donbass. Mwaka 2015 alitumia vikosi vyenye wanajeshi wasiopungua 60,000 hadi kukamilisha ile vita dhidi ya waasi na magaidi. Kipindi hiki kupeleka wanajeshi 60,000 siyo jambo rahisi.
Nne, NATO na EU wameanzisha chokochoko nyingine nchini Georgia kama zile za Maidan nchini Ukraine mwaka 2014 ambazo ndiyo chanzo kikubwa cha uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Serikali iliyopo Georgia ina mahaba na Moscow, EU, Ukraine na NATO hawataki hili litokee kabisa. Upande mwingine Urusi hataki kabisa Georgia igeuke Ukraine nyingine. Hivyo kama mambo yakiwa mabaya na serikali ikapinduliwa itabidi avamie kijeshi. Mwaka 2008 alivyovamia Georgia alitumia vikosi vyenye wanajeshi 75,000. Kipindi hiki sidhani kama itakuwa rahisi.
Tano, NATO wanamtumia Turkey kwasababu wanafahamu fika kwamba, ili Urusi afanye oparesheni zake za kijeshi za anga ni lazima atumie anga la Turkey. Lakini pia, Turkey ni nchi jirani na Georgia, hivyo Urusi akivutana Turkey ina maana NATO wataitumia nchi hiyo kama njia ya kufanya vurugu dhidi ya Urusi kupitia Georgia.
Kubwa zaidi na hatari, ili manowari za kijeshi za Urusi zitoke Black Sea na kufika kwenye kambi ya kijeshi ya Urusi iliyoko Syria, ni lazima wapite nchini Uturuki kwenye mfereji wa The Bosphorous. Wakivutana Urusi atazuiwa kupita kama ambavyo mwaka 2015 nchi ya Malta ilizikataa manowari za Urusi kupita kwenye mipaka yake. Kazi ngumu.
Sita, kama Iran ataingilia moja kwa moja basi lazima Israel na Turkey wataingia kwenye vita dhidi ya Syria moja kwa moja kwasababu nchi zote hizi hazimpendi Iran. Israel na Turkey wakiungana madhara makubwa sana yatatokea nchini Syria na Israel hasahasa ukizingatia uwezo wa kijeshi ambao Iran kauonesha hivi karibuni.
Saba, Urusi na Iran wanaweza kutumia mgambo wa Houthis, japo hili nalo ni changamoto kwasababu tayari baadhi ya mgambo wako Urusi wanapambana kule Donbass, lakini pia Houthis wamekabwa koo hivi karibuni baada ya UK, USA na ISRAEL kuongeza nguvu ya mashambulizi dhidi yao kuvisaidia vikosi vya serikali.
MRUSI ATAFANYA NINI SASA ????
Anaweza kuhusika moja kwa moja kwa kupeleka vikosi vyake, japo hili ni jambo la hatari mno hata kama mpaka sasa ana vikosi vya wanajeshi milioni 1.15 (Active Personnel), hili litasababisha nguvu zake kule Ulaya kupungua.
Mchezo kama huu USSR alichezewa mwaka 1969 na NATO, baada ya kuona vikosi vyake vizito viko Eastern Europe, waliamua kuitumia China kuvamia mpaka wa kusini wa USSR ambao haukuwa na wanajeshi wengi. Ilikuwa ngumu kwa USSR kupeleka vikosi mpaka wa kusini kupambana na CHINA ndani ya usiku mmoja ilhali kule Ulaya kuna vikosi vizito vya NATO.
AU, Mrusi anaweza kufanya jambo la hatari zaidi ambalo wazungu hawawezi kulipenda. Kukodi maelfu ya mamluki kutoka Asia na Afrika wajazane Ulaya kuua maelfu ya Wazungu, jambo ambalo litakuwa ni hatari mno kwa bara la Ulaya.
Ila kubwa zaidi ni kwamba vita ikiendelea basi, UE itaendelea kupokea wimbi kubwa mno la wakimbizi kama ilivyokuwa 2011-2016, jambo ambalo litakuwa siyo zuri hasa kwa kipindi hiki ambacho uchumi wa mataifa ya UE umegubikwa na mfumuko mkubwa wa bei.
ENDAPO MATAIFA YATAHUSIKA MOJA KWA MOJA: Mfano Iran aende Syria basi lazima The Persian Gulf yote itahusika kwasababu hakuna taifa linaloweza kupambana na Iran bila kutumia korido za nchi kama Qatar, Saudi Arabia na Bahrain. Nchi hizi ambazo zina kambi za jeshi za Marekani zikitumika kuishambulia Iran, lazima nazo zitashambuliwa vibaya.
NB: Mpaka sasa, kwenye huu mchezo mwenye THE UPPER HAND ni Benjamin Netanyahu na Israel yake. Akizichanga karata zake vizuri (Jambo ambalo sidhani kama ataweza) basi anaweza kupata suluhu kubwa kabisa ya kidiplomasia hasa kule GAZA na WEST BANK, lakini pia kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kumtenga IRAN kutoka Lebanon na Syria.
SWALI: Je, Mrusi anaweza kukubali kupoteza kambi zake muhimu za kijeshi kule Tartus na kukubali maslahi yake mengine ya kiusalama yapotee kwa kukubali kuachia serikali ya Assad ianguke ???