Changamoto za kufanya kazi na Mtu anayekaribia kustaafu kwa heshima



Wivu tu, anataka abaki hapo, muangalieni huyo msije toka naye.
 
Umenichekesha sana 😂😂
Mimi nilishajaribu hayo makitu aisee naona sielewi. Yanavutia lakini vitoto vidogo vitaalamu vilikua vinanikanda nikaona ni kuaibishwa huku.
Mkuu chakufanya wewe unajaza tu games alafu unaanza kucheza moja moja hadi utapata unalolipenda, game raha sana.

Mfano game za racing unanunua hadi consule zake wewe ni kukaa sebuleni ni kuburudika tu, uzuri sahivi unanunua hadi uskani kabisa ni wewe tu.
 
Lijinga hilo hakujipanga kabla.

Anastress za ataishije baada ya kumaliza kazi.
 
Lijinga hilo hakujipanga kabla.

Anastress za ataishije baada ya kumaliza kazi.

Vijana walio kwenye ajira wanamtukana mzee kwamba hakujipanga ila nawaambia kama una tubiashara twako tunafanya vizuri usidhani ukistaafu tutaendelea kufanya vizuri, vinafanya vema kwa sababu

1. kuna mahali unapata pesa kutoka kwenye kazi unaboost tuendelee mbele
2.wanakupa heshima kwasababu wanajua upo sehemu flani ili siku wakiwa na shida wanakuona
3. mnapiga dili kwa sababi upo serikalini, ukitoka huna jipya wanahamia kwa wengine
4. Pesa inaisha haiongezeki
5.unaitwa "Mstaafu" huna dili tena hata simu hutaziona

OGOPA SANA KUSTAAFU NDUGU ZANGU, Ukifika Miaka 50 utashangaa tu 58 imefika bila kujua
 
😎😎😎 Jiandae
 
😎😎😎 Jiandae
kustaafu hakuna kujiandaa kwa watumishi wa serikali wa kawaida, ambao wakistaafu mishahara inakata, Unaziona "STK, STL, DFP" unaumia roho balaa hata kama upo ndani ya Nissan Murano.

wenye raha ni wale wanaolipwa 80% baada ya kustaafu, wengine ni Mungu asaidie tu
 
Inawezekana ana stress za nyumbani. Tafuta siku umtembelee nyumbani kwake unaweza kijua sababu na ukamshauri. Ila Mimi sijawahi pata kazi ya kusubili pension, nielimu ili nimejiajili. Sina uzoefu na hao ila hayo ni mawazo yangu. [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Vipi anaangukia kwenye kile kikokotoo cha 33%? Kama anaangukia happ, basi mfikishie salamu zangu za pole.

Maana ni wastaafu wachache sana ndiyo wamekielewa hicho kikokotoo cha hovyo.
Mkuu emb nitoe kiwi cha macho maana mimi nshastaafu "miaka".
Nasikia kitita cha kiinua mgongo kinapunguzwa, ila "take home" ya kila mwezi ya pensheni inakuwa kubwa?
 
Kuna tabu za uzeeni kawaida mi nafanya kazi na wazee wanakaribia kustaafu na mmoja tulimuaga mwaka Jana mwanzoni.

wako peace sana na mpaka raha ila kiuchumi wapo mbali kuna mwengine ana gorofa na miradi kibao .
Basi hii mambo inaendana na hali ya Uchumi.
Kama hujajipanga vizuri, kustaafu inakuwa mateso kidogo
 
Mkuu emb nitoe kiwi cha macho maana mimi nshastaafu "miaka".
Nasikia kitita cha kiinua mgongo kinapunguzwa, ila "take home" ya kila mwezi ya pensheni inakuwa kubwa?
Hicho kikokotoo ni cha kibabaishaji sana. Mstaafu hupewa kwa mkupuo 33% pekee ya mafao yake. Mfano kama ulitakiwa kupata milioni 100, basi utapewa milioni 33 tu!

Halafu hela nyingine inayobakia unalipwa kama mshahara kwa miaka 12 tu, then wanasikitisha. Na ikatokea ukondoka duniani kabla ya hiyo miaka 12, basi hiyo hela inakuwa ni mali ya serikali.

Wastaafu wengi wanalalamikia hicho kikokotoo. Maana hiyo 33% wanayopewa, huwa haiwasaidii kututatua changamoto zote wanazo kumbana nazo baada ya kustaafu.
 
Muda wa kustaafu umefika ila hakujiandaa namna ya kuishi baada ya kustaafu na naona kachelewa kufanya hivyo, ndio maana anaonekana kupanic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…