Wakuu Vipi hili suala la kuomba pande zote Wizara ya Afya na TAMISEMI
SUALA hili nimeliwekea uzi Ila naona Mods Siyo kipaumbele chao.
Ajira ni ushindani!
Ukipata huku unaweza kukosa kule na kinyume chake.
Ukipata kote unachagua pa kwenda, iko hivo siku zote na wengine watafill hiyo nafasi!
Kwa nini tunawafundisha Watu kuchangamkia fursa? Kila Siku Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu akiongea anawasihi vijana kukaba Halafu Fursa zikija tunaweka mibano isiyokua na maana.
Sasa wizara ya Afya inakuwekea limitations hata kama unazo sifa!
Nawashukuru OR-TAMISEMI wameupuuza msimamo huo wa katibu mkuu wa Afya.
Naamini hizi ni taasisi mbili tofauti na ndiyo maana Wizara afya wamesisitiza kuhakiki vyeti mahakamani huku TAMISEMI siyo muhimu na mambo mengine mengi wanayopishana
Kama huu ungekua msimamo wa Mh Rais na Serikali kwa ujumla kwenye hizi ajira basi hili katazo lingeonekana Kwenye Tangazo la OR TAMISEMI pia!
Nawasihi vijana Ombeni kotekote huwezi jua bahati yako iko wapi, Tuwapuuze wasomi wenzetu wachoyo wa ridhiki kama huyu Katibu mkuu Afya.
Haya lazima ni maoni yake binafsi.
View attachment 2206222
Makubi huyu?