Unatarajia matokeo yapi zaidi ya yale yanayoelezwa na vyombo husika kama vile WHO na CDC?! Na kama ndo hayo, tutoe mara ngapi?!Mimi nafikiri sayansi ni mabishano ya hoja ktk kutafuta ukweli. Sasa mtu akija na hoja za kupotosha ajibiwe kisayansi. Apewe hayo matokeo ya utafiti yanayoharalisha mawazo yako
Unajua mijadala kama hii ingekuwa ngumu sana zamani kupata taarifa lakini sio zama hizi za Internet ambazo mtu anaweza tu kuingia Google na ku-search "How Effective is COVID-19 Vaccines" na huko atapata taarifa nyingi tu kutoka vyanzo vya kitaalamuna sio kutoka kwa Conspiracy Theorists !!
Mtu aki-Google "How was it possible for COVID-19 Vaccines to be developed so fast" atakutana na majibu ya kitaalamu bila tatizo lolote!!
The problem, watu ni wavivu wa kutafuta taarifa! Na wakizitafuta wanashindwa kuchuja taarifa kwa sababu sio wote wenye uwezo wa kutambua credible source ni ipi!! But on top of that, watu wanapenda sana conspiracy theories!!!
Tangu nikiwa mdogo, nimekuwa nikisikia conspiracy theories za Wazungu kutuletea hiki na kile ili tuzizaane, mara ili tuwe mahanisi, mara hivi... ndo hapo nisipochoka kujiuliza "what's so special tulichonacho cha kuwafanya hao Wazungu watamani kutufuta kiasi hicho"!!