#COVID19 Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?
Wasabato wengine hawanywi Chai, pepsi au Coca Cola
 
Wasabato wanaamini kusali jumapili ni alama ya mnyama
 
serikali ya awamu ya tano ilituaminisha kuwa korona haipo na iliisha kwa maombi, madaktari, maprofesa,mawaziri wote hata huyu kidamba wa afya naye alituaminsha hivyo hivyo...
Umeandika porojo tu hapa. ww huna scientific means ya kusema corona iliondoka 100% kwa maombi. nani kasema iliondoka?
hakuna cha kuhongwa hakuna cha behind the scene..

tatizo la serikal yetu haina scope.. yaani msimamo kiasi kwamba kila rais anaekuja akisema tuende kushoto wanaenda huko.. tuende kulia wanaenda huko. hakuna wa kupinga.
 
Peleka huko ujinga wako , chanjo ya CORONA ni hiari, kama wewe hutaki acha usiende kuchanja.
 
serikali ya awamu ya tano ilituaminisha kuwa korona haipo na iliisha kwa maombi, madaktari, maprofesa,mawaziri wote hata huyu kidamba wa afya naye alituaminsha hivyo hivyo...
Mpuuzi mwingine huyu

Akili ndogo siku zote huwa hamuwazii chochote zaidi ya majungu, fitna, Tuhuma na chuki

rais mzima aweke nchi nzima regain Kwa kuhongwa?

she is 62 years old akishahongwa hiyo Pesa atapeleka wapi?

apokee Pesa gani kuangamiza watu milioni 60??
Hivi hamuwezi kuja na scientific evidence against vaccines hadi mje na majungu?

sayansi imeongea inabidi tuifuate
Nawaza sana mtu kama wewe unatumia dawa, simu, magari, mbolea, nguo, mafuta ya mwili na ulitumia chanjo za hao hao - vipi waasisi wa taifa walihongwa?

mtaji wa madhalimu wote duniani ni watu masikini, wavivu na maamuma…. Usinufaishe watu mkuu

Gwajima hajawahi kuwa na permanent agenda, ndio maana hata kanisa lake Bado ni Hema , he is purely temporarily getting good hits Kwa kutumia watu kama wewe
 
Kijana mdogo mwenye muonekano wa afya njema hata akipata Corona mwili wake unanafasi kubwa ya kushinda mpambano lakini anakauka koo kushawishi watu including the vulnerables wasipate chanjo. Ole wao wanaotumia jina la Mungu kiholela kwa hisia zao.

Angalizo: Kila binadamu ameumbwa ili aishi kutimiza mpango wa Mungu. Hivyo kuweka mazingira hili binadamu asiishi kutimiza huo mpango wa Mungu ni kutimiza mpango wa Shetani. Tukumbuke hilo pia.
 
Nchi yetu inapitia kipindi kigumu cha maamuzi kuhusu afya za Watanzania.Kila mtu amekuwa mtaaalamu,kila Blog hivi Sasa ni Chanzo Cha Taarifa za Kisayansi! Ukiingia TikTalk ,Insta,Tweeter,kote kumejaa wanasayansi wakiungaa mkono au kuping chanjo!

Vyombo vilivyotegemewa vitoe mwongozo ni kama vimezidiwa nguvu na Hisia!

Wataalam nao hawaaminiki kwa Asiliamia 100!

Ni vurugu!
Tumefikaje hapa....jibu ni rahisi saana...Ubovu wa Katiba yetu,inayompa madaraka makubwa mtu mmoja!

Magufuli na Timu yake walifanikiwa kwa kiwango kikubwa kueneza 'Injili yao kuhusu COVID!

Cha kusikitisha Magufuli hayupo,lakini Vyombo vilivyoshadadia Injili yake kuhusu Covid vipo,na vimefanya U Turn!

Wataalamu na Viongozi Sekta ya Afya walio hubiri Injili ya Magufuli kuhusu COVID Ndio hao Leo wanahubiri Injili kinyume!

NI AIBU KUU !
Nani atawaamini!
Mh Rais alikuwa Msaidizi wa Mh.Magufuli leo amefanya U Turn😁

Bahati mbaya Corona Haisubiri tupate Muafaka!

Hitimisho ni kuwa Tunahitaji Muafaka wa Kitaifa ili kuwapa Mamlaka wa Wananchi kuhusu Hatma ya Maisha yao!

Kama Rais Magufuli asingekuwa na Mamlaka ya Kiamla kwa vyovyote Hali isingekuwa hivi!

Wasaidizi wake wotewaliishi.naye kwa woga na unafiki...Bila Shaka imejidhihirisha kwenye Mwelekeo wa Nchi katika Janga hili la Covid!

Ni Chaguo la kila.mtu Kuchanja au kutochanjwa lakini

..Your Life Matters!
Poleni Sana Viongozi mliofanya U Turn najua mnaona aibu na Soni zimewajaa ila najua hamuwezi kuthubutu kujiudhuru!
 
Saud Arabia siyo ile iliyokuwa inawatrtea waarabu wenzao waphalestine. Hii ya sasa inawapuuza waphalestine. Nadhani umenielewa.
Hii ya sasa kuna genge la wahuni la watu wasiojulikana.
Likiongozwa na marekani.
 
Naandika Kwa NIA nzuri kabisa ili nipate kueleweshwa ukweli. Kama Wave ya Kwanza ya Covid -19 ilipotokea huko ulaya ndo watalaamu waliingia Lab kutengeneza chanjo, na walijikita zaidi kwenye kile kirusi cha China, ikaja wave ya pili, kirusi kikazidi kujibadilisha na Sasa ni ya tatu tuliyonayo hapa kwetu.

Sasa mtwambie hii Chanjo ya J&J mliyotuletea ndo mliyofanyia utafiti wa hii wave ya tatu au ni Ile ya Kwanza? Na kama mmetuletea chanjo ya wave ya Kwanza ya Korona hii ya tatu ni lini mliifanyia utafiti?

Sent from my 5033X_EEA using JamiiForums mobile app
 
Kwani kuna mabadiliko makubwa kwenye antigenic make-up kiasi kwamba hiyo viral protein inayolengwa haiwezi tena kuwa recognised na immune cells.
 
Hii chanjo niyawimbi la tano. Chanjo nikwaajiri ya yajayo siyo yaliyopita!!!

Ngoja tusubiri wataalamu waje wajibu
 
Wakati tunajadili ya j&j, modena wamepandisha bei kufuatia ongezeko la uhitaji wa chanjo hiyo.
 
Je kwa nini nalazimika kusaini fomu ya kujibebesha lawama pindi madhara yatokanayo na chanjo yatakaponipata?
 
Why upinge kitu ambacho hulazimishwi, unataka kachanjwe hutaki baki nyumbani na Mambo flani YAKO alisema ,mwendazake
 
SABABU 10 YA KWANINI SITACHANJWA

1.Wataalamu wa afya wameshindwa kuniakikishia usalama wangu baada yakuchoma chanjo,serikali inanitaka nijaze fomu kukiri wao kutokuhusika na madhara yeyote yatakayojitokeza.

2.Wataalam hawajatoa maelezo ya nini Kilichopo katika chanjo na kanuni zilizotumika katika utengeneaji.

3.Wataalam wameshindwa kuniakikishia chanjo itakaa muda gani mwilini,mwezi,miezi mwaka au miaka fumbo hili haijulikani

4.Baada yakuchoma chanjo bado nitalazimika kuvaa barakoa.

5.Baada yakuchoma chanjo bado nitaweza kupata maambukizi.

6.Nikipata chanjo bado nitalazimika kuweka social distance(kutokukaribiana na watu).

7.Ndugu zangu wote na mimi wakipata chanjo bado hatutatakiwa kukaribiana wala kukumbatiana.

8.Serikali iliyopita ilituakikishia chanjo hazifai na ilitoa mfano kuna NNCHI fulani walipewa chanjo ikidhaniwa kuzuia kansa ya shingo yakizazi,kumbe ilikuwa kuzuia kuzaa,sasa wakati huu hakuna wakukanusha hili na hata kutoa ufafanuzi juu ya ukweli huo(kuwa ya sasa haina hayo madhara au vingievyo)

9.Serikali imeshindwa kutupa maelezo ya kwanini ilichagua chanjo ya jonson and jonson kati ya chanjo nyingi zilizopo ingali jonson and jonson inatuhuma yakugandisha damu na kusababisha madhara kwa wamarekani.

10.Hakuna kanusho lolote dhidi ya chanjo hizi kubadili DNA,kusababisha utasa..

Chanjo ni HIARI ya mtu,ni kosa kuhamasisha kuchoma au kutokuchoma tuache iwe jambo la mtu mmoja mmoja binafsi nimechagua kutokuchanjwa
 
Hiyo ni kwa mujibu wa mtazamo wako,ushauri wa bure chanja kwa manufaa yako na ya taifa,kuchanja utajikinga wewe na wengine hivyo kuiweka nguvu kazi ya taifa salama.
 
Back
Top Bottom