Ukiupata rudi hapa utugawie. Mimi niliutumia miaka ya 80
Hazina madhara kweli?Zile ni fungus. Hivyo ukimega kakipande kadogo ukaweka ktk chombo kingine ina- multiply.
Aisee we jamaa umenifanya niuukumbuke huo mmea....nilikuwa sijamuelewa mleta mada, tena nakumbuka mama alikuwa anauweka kabatini na kuufungia ili tusimalize juisi yakeUmenikumbusha mbali mkuu, nakumbuka mama alikuaga ananipa juice yake, chachu tamu, likawa linazaa chapati nyingine.
Itabidi tukikutana na wachina tuwaulize, hata mimi natamani kujua inapopatikana, nikipata jibu nitakuambia
Hiyo simu ulinunua sh ngapi mkuu km unakumbuka?Mmmh! Mkuu, bahati mbaya sikubahatika kuupiga picha wakati bado niko nao!
Pia miaka hiyo simu hazija eneo sana, kama zilikuwepo basi kwa watu wachache sana, nakumbuka simu yangu ya kwanza kumiliki nilikuwa SIEMENS C 25 kubwa kama kipande cha Sabuni enzi hizo tunaziita "MSHINDI" (aina ya sabuni) tena nilikuwa hazina camera! Miaka ya mwanzoni mwa 2000! Kabla ya kumilika NOKIA enzi hizo tunaziita "JENEZA" aha aha haaa! Hatari sana mkuu!
Ingekuwa ninalo sasa mbona tayari picha muda mrefu tu!
Hazina madhara kweli?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Hii kitu alikuja nayo shangazi kama sio dingi kutoka mkoani mbeya.
Huu mmea hata Tanzania tunao sababu tuna utajiri wa species nyingi sana za mimea.
Ngoja nikutafutie jina na ukipatikana nitashare na ninyi hapa jina na ikibidi tugawane mbegu ni mzuri sana ile kitu tulikuwa tunaigida sana juice yake.
Tuliweka kwenye zaidi ya vyomba sita tukilina maji yake. Alikuja kuharibu bi mkubwa alipookoka akaambiwa na pastor wake kuwa kile kitu ni mapepo na ni maagano ya mizimu. Yule pastor choko sana hadi leo namind kichizi nikimuona natamani nimlabue makofi na mitama maaana ndie alimchanganya bi mkubwa akaona ule m'mea una uhausiano na maswala ya giza na kumbe ni ukosefu tu wa elimu ya mimea na tiba asili.
Bi mkubwa aliyamwaga yale masufuria yote kimya kimya ndo hadi leo sijuagi pa kuupata.
Hazina madhara yoyote it's safe for human consumption.Hazina madhara kweli?
Mmea mzuri sana unanikumbusha mbali ,naweza upata wapi huo mmea gheto ulikua unawekwa na bi mkubwa kwenye kile kifuniko cha jiko la kichina lisilotumika lile la mafuta ya Taa .Mleta mada nauhitaji
Mimi nakumbuka alipewaa mama yangu kwa ajili ya Figo ,unakunywa chai ule...Nakumbuka tulikuwa kunaweza chai ya rangu sio maji
mkuu vipi kama nitaenda kuuweka ziwani siutaishi maisha marefu sana!Eeewaaaa!!!
Hakika unaufahamu vizuri huu mmea! Ndio huo huo uliouelezea, mbegu yake ndio hiyo hiyo unapotanuka na kuubandua hiyo ndiyo mbegu yake mkuu!
Nilikaa nao karibu miaka 3 au 4 hivi, nilikuwa nauhudumia vizuri sana, na unapozaliana nilikuwa naupunguza na kuzitupa mbegu zake yaani yale mazalia yake.
Lakini sasa nikaja kusafiri na kujichelewa kurudi nikakuta umeshakufa kwa kunyauka, sasa natafuta kama kuna mtu ana huo mmea anisaidie utakapotoa mazalia yake (mbegu).
Shukrani sana!
mkuu vipi kama nitaenda kuuweka ziwani siutaishi maisha marefu sana!