Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

Nimefurahi sana kuona mada kuhusu huu mmea, nakumbuka miaka ya 90's tuliwahi kuutumia nyumbani na mama alisema kuwa aliutoa kwa bibi. Mama ameshafariki na nilitamani kweli kujua huu mmea chapati ni nini haswa lakini kila nikimuuliza bibi anasema haujui.

Nimefurahi ku

Tuko pamoja mkuu,

Tuendelee kuuliza uliza kwa watu huenda mmoja akabahatika kuupata sehemu na kushare na wengine! Penye wengi hapaharibiki neno na umoja ni nguvu!
 
Wakuu mrejesho ndo huu hapa, nilizinunua huku ile siku ya uzi. Mzigo umefika leo, kesho ntaanza kuichanganya maana ishakuwa usiku hapa.
Nikishachanganya nitawapa mrejesho pia
IMG_1694.jpg

IMG_1693.jpg
 
[emoji871]Binafsi niliutumia sana huu mmea.

[emoji871]Nilipewa mbegu yake na rafiki yangu mmoja kutoka Nshamba/Muleba.

[emoji871]Alikuwa jirani yangu pale Kijenge Arusha mwaka 1998.

[emoji871]Na mimi nilisafiri niliporudi nikakuta mke wangu kazembea na mmea umekufa.

[emoji871]Na yule Rafiki yangu alikwishahama wakati huo.
 
Kwa sisi tuliuita mkate wa Mecca. Miaka ya nyuma wengi waliotoka Hijja walirudi nao, na ukizaa/ totoa unampatia na mwenzio, ukweli ni kwamba mmea ule ulikuwa ni Tiba. Sasa hivi mahujaji wengi waakiridi waanarudi na vitu vya kippuuzi zikiwemo simu na dildo.
Kweli miaka ya 90 mzazi wangu aliletewa na hujaji mmoja. Wote Mungu awarehemu! Sijui ulipotelea wapi?? Ila tulikuwa nao pale nyumbani karibu miaka miwili mitatu
 
Kwa sisi tuliuita mkate wa Mecca. Miaka ya nyuma wengi waliotoka Hijja walirudi nao, na ukizaa/ totoa unampatia na mwenzio, ukweli ni kwamba mmea ule ulikuwa ni Tiba. Sasa hivi mahujaji wengi waakiridi waanarudi na vitu vya kippuuzi zikiwemo simu na dildo.
YANI MTU ANATOKA KUHIJI ANARUDI NA DILDO🤣🤣
 
Vipi mrejesho uliupata sidhani kama ukiamua kuutafuta utaukosa. Fika ubalozi wa China au mchina yeyeto akupe connection, ngoja nami nichek alibaba au wachina kupitia wasap
 
Habari wakuu,

Mwishoni mwa mwaka 1998 na mwanzoni mwa miaka 2000 kuna wanajeshi walienda nchini China kuchukua mafunzo ya ngazi Fulani. Baada ya muda Fulani walirejea nchini, walirudi na vitu mbalimbali ikiwemo zawadi, mmoja kati ya wanajeshi hao ambaye tulikuwa na undugu nae, alirudi na mmea fulani mfano wa chapati kubwa sana yenye rangi nyeupe kijivu, ambayo ilikuwa inawekwa kwenye maji, ndani ya sufuria au bakuli kubwa na kujazwa maji, kisha baada ya kama week tatu au mwezi mmoja unamimina Yale maji yake ambayo huwa yamebadirika rangi na kuwa na rangi kama ya chai ya rangi.

Maji hayo huwa na ladha tamu sana kama uchachu fulani au kama ile ladha ya rosela! Wengine uweka sukari au asali kwa kuongeza ladha zaidi. Chapati hiyo ya Kichina ambayo hukuwa kubwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, na pia hukuwa na kutoa machapati mengine mengi, kwa mwezi unaweza kuvuna mimea chapati hiyo kama miwili au mitatu. Yaani kimsingi hayo machapati mimea huzaliana kila mwezi au baada ya miezi miwili.

Pia hufa, kwasababu chochote kile kilicho na uhai hufa basi pia mmea huo aina ya chapati hufa, kwasababu huishi ndani ya maji, basi kila baada ya mwezi lazima ubadilishe maji yake na kuongeza mengine! Ukiusahahu na kutokuongeza maji basi mmea huo utaukuta umekauka kabisa na kufa, maji yote yameisha. Mmea huo hula maji tu!

Sasa basi baada ya kupewa mmea chapati huo tulijitahidi kuutunza sana na kufaidi juice yake tamu ambayo pia nasikia ni dawa ya magonjwa kadhaa ya mwili wa mwanadamu, ambayo hutumiwa sana kule China kwa matibabu kadhaa. Kwa bahati mbaya kipindi fulani nnilisafiri kwenda mkoani nikiamini kwamba nitawahi kurudi Dar na kuuhudumia mmea wangu, lakini mambo hayakuwa kama nilivyopanga kwani nilipata dharura na kuchelewa kurudi Dar. Nilipowasili nilikuta ule mmea chapati wangu umeshakauka kabisa kwa kukosa maji na kunyauka kabisa na hatimaye kufa!

Kiukweli nilisikitika sana sana, nimejaribu kuutafuta ule mmea bila mafanikio. Hivyo naomba kama kuna mtu yuko humu Jamiiforums anaufahamu ule mmea, au anao, please naomba sana kwa unyenyekevu anisaidie mbegu yake wanandugu! Naomba sana!
View attachment 2116778
Nimeuliza alibaba China unaweza ukapata unatumiwa hadi ulipo.
Contact zaidi zipo google watakupa link,but najua wachina nchini awakosi.
 
Nimefurahi sana kuona mada kuhusu huu mmea, nakumbuka miaka ya 90's tuliwahi kuutumia nyumbani na mama alisema kuwa aliutoa kwa bibi. Mama ameshafariki na nilitamani kweli kujua huu mmea chapati ni nini haswa lakini kila nikimuuliza bibi anasema haujui.

Nimefurahi ku
Ni lazima uweke kwwnye chombo kidogo? Jee nikiweka kwwnye jaba au tank kama una safari unaacha hata mwezi?
 
Ndio nami ndo nimepata kumbukumbu kwa nini sikuyatumia kabisa hayo maji ya hizo chapati za kichina.hiyi imani ya kwamba inauhusiano na mashetani nami niliisikia nikakaa mbali nayo kabisa kuna dada mmoja alipewa akaambiwa kuwa ni tiba ya magonjwa mengi.so yeye alikuwa anaumwa na sa hivi ni marehemu huyo dada ilikuwa miaka ya 95 hivi.kumbe ni tiba nzuri na aihusian na mizimu?
Haya bwana ngoja tuitafute
 
Habari wakuu,

Mwishoni mwa mwaka 1998 na mwanzoni mwa miaka 2000 kuna wanajeshi walienda nchini China kuchukua mafunzo ya ngazi Fulani. Baada ya muda Fulani walirejea nchini, walirudi na vitu mbalimbali ikiwemo zawadi, mmoja kati ya wanajeshi hao ambaye tulikuwa na undugu nae, alirudi na mmea fulani mfano wa chapati kubwa sana yenye rangi nyeupe kijivu, ambayo ilikuwa inawekwa kwenye maji, ndani ya sufuria au bakuli kubwa na kujazwa maji, kisha baada ya kama week tatu au mwezi mmoja unamimina Yale maji yake ambayo huwa yamebadirika rangi na kuwa na rangi kama ya chai ya rangi.

Maji hayo huwa na ladha tamu sana kama uchachu fulani au kama ile ladha ya rosela! Wengine uweka sukari au asali kwa kuongeza ladha zaidi. Chapati hiyo ya Kichina ambayo hukuwa kubwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, na pia hukuwa na kutoa machapati mengine mengi, kwa mwezi unaweza kuvuna mimea chapati hiyo kama miwili au mitatu. Yaani kimsingi hayo machapati mimea huzaliana kila mwezi au baada ya miezi miwili.

Pia hufa, kwasababu chochote kile kilicho na uhai hufa basi pia mmea huo aina ya chapati hufa, kwasababu huishi ndani ya maji, basi kila baada ya mwezi lazima ubadilishe maji yake na kuongeza mengine! Ukiusahahu na kutokuongeza maji basi mmea huo utaukuta umekauka kabisa na kufa, maji yote yameisha. Mmea huo hula maji tu!

Sasa basi baada ya kupewa mmea chapati huo tulijitahidi kuutunza sana na kufaidi juice yake tamu ambayo pia nasikia ni dawa ya magonjwa kadhaa ya mwili wa mwanadamu, ambayo hutumiwa sana kule China kwa matibabu kadhaa. Kwa bahati mbaya kipindi fulani nnilisafiri kwenda mkoani nikiamini kwamba nitawahi kurudi Dar na kuuhudumia mmea wangu, lakini mambo hayakuwa kama nilivyopanga kwani nilipata dharura na kuchelewa kurudi Dar. Nilipowasili nilikuta ule mmea chapati wangu umeshakauka kabisa kwa kukosa maji na kunyauka kabisa na hatimaye kufa!

Kiukweli nilisikitika sana sana, nimejaribu kuutafuta ule mmea bila mafanikio. Hivyo naomba kama kuna mtu yuko humu Jamiiforums anaufahamu ule mmea, au anao, please naomba sana kwa unyenyekevu anisaidie mbegu yake wanandugu! Naomba sana!
View attachment 2116778
Umenikumbusha mbali sana. Nilikuwa nao nyumbani kwangu nikasafiri dada wa kazi akasahau kuuwekea maji ukafa
 
Wakuu mrejesho ndo huu hapa, nilizinunua huku ile siku ya uzi. Mzigo umefika leo, kesho ntaanza kuichanganya maana ishakuwa usiku hapa.
Nikishachanganya nitawapa mrejesho pia
View attachment 2121002
P

View attachment 2121003
Mkuu naomba mbegu
 
Back
Top Bottom