Uchaguzi 2020 'Charisma' ya Tundu Lissu itazidi kumpa shida sana Magufuli na CCM kwa ujumla

Uchaguzi 2020 'Charisma' ya Tundu Lissu itazidi kumpa shida sana Magufuli na CCM kwa ujumla

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Charisma - compelling attractiveness or charm that can inspire devotion in others.

Kwa tafsiri ya kiswahili, Charisma ni ule mvuto mtu anaokuwa nao mpaka unatamani kama anaongea aendelee kuongea.

Katika siasa Charisma ni kitu cha umuhimu sana, kama huna Charisma, huwezi kuvutia watu wakakusikiliza.

CCM wana bahati mbaya sana kukosa viongozi wenye Charisma, ndo mana unaona kwenye kampeni wamekuwa wanatumia sana wasanii wa bongo fleva ili kuweka mvuto ambao ulistahili kuletwa na viongozi wao, kinyume chake ni sahihi kabisa, CHADEMA wana viongozi wenye Charisma ya hali ya juu sana, mtu kama Halima Mdee, Tundu Lissu, Mnyika, au Mbowe wakianza kuongea huwezi tamani ashushe mic, ni viongozi ambao wanaweza kuunganisha maneno mfululizo kwa lisaa lizima wakimwaga point ambazo hadhira inataka kuzisikia.

Nimemsikiliza leo Magufuli akiwa Shinyanga, honestly, unaona kabisa hata namna anavyounganisha sentensi, ni kama vile anakuwa anakosa coordination ya meneno. Magufuli anaweza kuongea sentensi kumi ambazo zinakinzana zenyewe kwa zenyewe, kitu ambacho kwa mtu unayemsikiliza ni rahisi sana kupoteza hamu ya kumsikiliza.

Ndo maana ya ule usemi wa kwamba, 'viongozi wanazaliwa' kama huna Charisma, huwezi kuongoza watu wakakupenda kwa sababu ni ngumu pia kwa mtu asiye na Charisma kuelewa changamoto za wengine. Ndo mana unamsikia Magufuli akituahidi tena kutumia mabilioni mengine ya kununua ndege, ni kama hajasikia na kuelewa vema kilio cha watanzania kwamba hizi ndege sio matumizi ya kipaumbele kwa taifa. Na hii ni moja wapo ya tabia za watu wasio na Charisma, daima hujali sana vipaumbele vyao dhidi ya wanaowazunguka.

Kama mambo yataendelea kwenda hivi, ni kwamba Magufuli ataonekana anaongea bila kuwa na hoja na mambo yanavoenda mvuto wa Magufuli kwa wapiga kura unazidi kupuputika, upande wa pili, Charisma inambeba Lissu kwa nguvu sana, wengine tulishakata tamaa na siasa lakini, namna Lissu anavofanya mambo mpaka sasa, ametuinua sana morali zetu, na hii yote ni nguvu ya Charisma aliyojaliwa ambayo wengine wamenyimwa.
 
Huu ni ukweli usionashaka...nmemfuatilia karibu mikutano miwili ya kampeni..huyu Tundu ni mtu makini sana kweny kupanga sentensi. Sema kwa kuwa siasa za kiafrica ni sayansi basi lakini kama si vingnevo huyu atakuapua kura nyingi za wananchi. Na ikulu a naiona kimo cha mbuzi asbui na mapema 28.10.2020!!!
 
Lissu anajua kujieleza,anajua kujenga hoja,anajua kuongea,anajua kujitetea na pia najua kuudhi.
Kuudhi Ni moja ya mbinu za mawakili katika kutaka kujua mpimzani wake anawaza ninioyoni.
Kwenye boksi la kura ,Lissu atashinda,
Kilichobaki Ni kupigania kutangazwa ushindi wake.
 
Sio kwamba ccm hawajui kuwa hawana mvuto, wanajua sana lakini hawawezi kukubali kushindwa, maana wanajua watakosa mlo, na kikubwa zaidi wengi wao wanaogopa kuishia jela kwa wizi na uovu wao kuwa hadharani.

Ndio maana ukisema neno mdahalo hapa ccm hawako tayari kwa hilo jambo, maana wanajua wanaenda kuumbuka.
 
Kilichowazi na ccm wanajua ni kwamba kwanza hawakushinda Zanzibar wala bara 2015 ndio maana ya rais kutangaza vita dhidi ya upinzani alipoingia tu madarakani. Chaguzi za madiwani na wabunge walionunua wote mnakumbuka ilikuwaje. Watz wanajua nn kilitokea December mwaka jana uchaguzi serikali za mitaa.....
Kimsingi na ccm wanajua hakuna
1. Wakulima
2. Wafanyakazi
3. Wafanyabiashara
4. Wanafunzi
Wakuichagua ccm na ndio chanzo cha haya yote kulazimisha kubaki madarakani kwa nguvu ya tume km alivoahidi rais lkn pia kwa nguvu ya dola km alivyosema Bashiru
 
Anakinzana balaa. juzi aliwadanganya watu wa ikungi eti anampenda lissu akakinzana na ile kauli ya siku ya ripoti ya makinikia kuhusu kazi za wanajeshi kule kwenye vita.

Atuachie nchi yetu hafai. hana utu. muuaji wa demokrasia. siyo mstaarabu.
 
Back
Top Bottom