Uchaguzi 2020 'Charisma' ya Tundu Lissu itazidi kumpa shida sana Magufuli na CCM kwa ujumla

Uchaguzi 2020 'Charisma' ya Tundu Lissu itazidi kumpa shida sana Magufuli na CCM kwa ujumla

Walau wewe kidogo una akili.

Ila manyumbu wenzio hata akili ya kutambua kuwa Lissu hatoshinda, hawana.
Ni kweli hatoshinda ila sidhani kuwa itakuwa ni vyema kujikatia tamaa kwenda kupiga kura. Walidhani kuwa cdm itaugomea huo uchaguzi wajilambie bwerereree sana leo tunalia kidomo juu. Lissu ni mwiba wa mchongoma kwetu. Jitu lina roho ya paka hili
 
Charisma haikupeleki ikulu. Kuna kasiri ka muhimu sana kanakupeleka ikulu

Kipaji cha Mungu huwezi kukichukuwa ikulu unaweza kuiba kura. Miaka mitano ikiisha Lissu atabaki na kipaji chake na Magu anabaki na kuomba watu wakumbuke aliyofanya. Ukiuliza Mkapa kafanya nini kwa miaka 10 watu hata hawajui! Watanzania wanasahau baada ya mwaka tu
 
SEMA HATOTANGAZWA MSHINDI JAPO ATASHINDA
Endapo watu wakimkubali sana Lissu, hapo ndo itakuwa ugumu sana kwa tume kupindua meza maana machafuko lazima.

Enzi ya kikwete na mkapa ilikuwa rahisi kuiba kura maana at least kikwete na mkapa walikuwa ni viongozi pia wenye mvuto.

Sahiv ni tofauti sana kwa magufuli
 
Wewe shule lazima ulikuwa unakuwa wa mwisho, hakuna ubushi hapo!
Hivi katika maelezo ya hicho kinachoitwa charisma umeona Kuna swali linauliza mshindi ninani? Hivi ukiwa CCM kitugani kinavuruga akili?
Eti mimi nilikuwa nakuwa wa mwisho shuleni.

Sawa, sikatai.

Ila we unayeniambia mimi nilikuwa nakuwa wa mwisho shuleni, hata kuandika kwa usahihi tu kunakushinda!

Hujui wapi pa kutumia herufi kubwa. Maneno mawili unayaunganisha na kuwa neno moja, kinyume na ilivyo.

Hata kwenye msamiati na tahajia umekosea!

‘ubushi’ ndo nini?

Aliyekuwa anakuwa wa mwisho darasani anaukosoa uandishi wako 🤣🤣🤣.

Jiangalie.
 
Ni kweli hatoshinda ila sidhani kuwa itakuwa ni vyema kujikatia tamaa kwenda kupiga kura. Walidhani kuwa cdm itaugomea huo uchaguzi wajilambie bwerereree sana leo tunalia kidomo juu. Lissu ni mwiba wa mchongoma kwetu. Jitu lina roho ya paka hili
Umeongea vema sana,. Lissu anatufundisha pia kutokuwa wanyonge kwenye maisha.

Maisha ni kupambana, anything can happen, CCM wakiendelea kuamini eti lazima washinde, watakuja kujuta sana
 
Charisma - compelling attractiveness or charm that can inspire devotion in others.

Kwa tafsiri ya kiswahili, Charisma ni ule mvuto mtu anaokuwa nao mpaka unatamani kama anaongea aendelee kuongea.

Katika siasa Charisma ni kitu cha umuhimu sana, kama huna Charisma, huwezi kuvutia watu wakakusikiliza.

CCM wana bahati mbaya sana kukosa viongozi wenye Charisma, ndo mana unaona kwenye kampeni wamekuwa wanatumia sana wasanii wa bongo fleva ili kuweka mvuto ambao ulistahili kuletwa na viongozi wao, kinyume chake ni sahihi kabisa, CHADEMA wana viongozi wenye Charisma ya hali ya juu sana, mtu kama Halima Mdee, Tundu Lissu, Mnyika, au Mbowe wakianza kuongea huwezi tamani ashushe mic, ni viongozi ambao wanaweza kuunganisha maneno mfululizo kwa lisaa lizima wakimwaga point ambazo hadhira inataka kuzisikia.

Nimemsikiliza leo Magufuli akiwa Shinyanga, honestly, unaona kabisa hata namna anavyounganisha sentensi, ni kama vile anakuwa anakosa coordination ya meneno. Magufuli anaweza kuongea sentensi kumi ambazo zinakinzana zenyewe kwa zenyewe, kitu ambacho kwa mtu unayemsikiliza ni rahisi sana kupoteza hamu ya kumsikiliza.

Ndo maana ya ule usemi wa kwamba, 'viongozi wanazaliwa' kama huna Charisma, huwezi kuongoza watu wakakupenda kwa sababu ni ngumu pia kwa mtu asiye na Charisma kuelewa changamoto za wengine. Ndo mana unamsikia Magufuli akituahidi tena kutumia mabilioni mengine ya kununua ndege, ni kama hajasikia na kuelewa vema kilio cha watanzania kwamba hizi ndege sio matumizi ya kipaumbele kwa taifa. Na hii ni moja wapo ya tabia za watu wasio na Charisma, daima hujali sana vipaumbele vyao dhidi ya wanaowazunguka.

Kama mambo yataendelea kwenda hivi, ni kwamba Magufuli ataonekana anaongea bila kuwa na hoja na mambo yanavoenda mvuto wa Magufuli kwa wapiga kura unazidi kupuputika, upande wa pili, Charisma inambeba Lissu kwa nguvu sana, wengine tulishakata tamaa na siasa lakini, namna Lissu anavofanya mambo mpaka sasa, ametuinua sana morali zetu, na hii yote ni nguvu ya Charisma aliyojaliwa ambayo wengine wamenyimwa.
Hata wewe maelezo yako yanakinzana
Kama ni dhana ya nan kiongozi kuzaliwa au kutengenezwa sijaona mahala popote palipo onyesha mvuto kama ni trait ya kiongozi bora bali kiongozi bora ndani yake kuna uwezo fulani wa kutenda na kufanya vitu vinavyo onekana kwa wale anao waongoza

Hivyo kwa wagombea wote wa kiti cha uraisi
2020 MAGUFULI ni kiongozi
Uongozi sio porojo,
Na pia kiongozi au uongozi hauna fomula moja bali kiongozi huitajika kutokana na nyakati na wakati tofauti tofauti ambapo unaweza kuta viongozi wanatofautiana kwa dhama zao

Hata mitume na manabii au wafalume hawakufanana kiutendaji bali tofauti zao zileendana na huitaji wa nyakati husika.
 
Kilichowazi na ccm wanajua ni kwamba kwanza hawakushinda Zanzibar wala bara 2015 ndio maana ya rais kutangaza vita dhidi ya upinzani alipoingia tu madarakani. Chaguzi za madiwani na wabunge walionunua wote mnakumbuka ilikuwaje. Watz wanajua nn kilitokea December mwaka jana uchaguzi serikali za mitaa.....
Kimsingi na ccm wanajua hakuna
1. Wakulima
2. Wafanyakazi
3. Wafanyabiashara
4. Wanafunzi
Wakuichagua ccm na ndio chanzo cha haya yote kulazimisha kubaki madarakani kwa nguvu ya tume km alivoahidi rais lkn pia kwa nguvu ya dola km alivyosema Bashiru
Hatutakubali watende huo uharamia wao,haturudi nyuma maana hili ni suala la kufa na kupona.Tunataka viongozi na siyo watawala.
 
baada ya uchaguzi natarajia kuona unaandika "tumeibiwa kura.."
kujiaminisha visivyo ukweli[emoji3]
Huu ni ukweli usionashaka...nmemfuatilia karibu mikutano miwili ya kampeni..huyu Tundu ni mtu makini sana kweny kupanga sentensi. Sema kwa kuwa siasa za kiafrica ni sayansi basi lakini kama si vingnevo huyu atakuapua kura nyingi za wananchi. Na ikulu a naiona kimo cha mbuzi asbui na mapema 28.10.2020!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
tambalizeni at work....
Sio kwamba ccm hawajui kuwa hawana mvuto, wanajua sana lakini hawawezi kukubali kushindwa, maana wanajua watakosa mlo, na kikubwa zaidi wengi wao wanaogopa kuishia jela kwa wizi na uovu wao kuwa hadharani. Ndio maana ukisema neno mdahalo hapa ccm hawako tayari kwa hilo jambo, maana wanajua wanaenda kuumbuka.
 
tulisikia the same juu ya Lowassa...
leo sio rafiki yetu kabisa
Kwa sababu mifumo inayosimamia uchaguzi sio huru, wazi, iso-haki na haiaminiki.

Lissu ni mshindi mioyoni mwa watu wengi...hiyo pekee inatosha.
 
Tapeli Huyu wa MIGA Leo haongelei kabisa habari ya Madini wala kushitakiwa hauitaji mvuto sisi Tunaitaji jembe lenye uthubutu Wa kubishana Wa watu Wa duniani na sio kuwanyeyekeaaa MAGUFURI TANO TENA
 
Lissu hatoshinda.,,
Nimecheka sana ,Mtu huna cheo chochote ccm wala hutambuliki

Mambo haya waachie Bia yetu,Gussie ,Pascal Mayalla huyu ni mzamiaji ccm bado nae hatambuliki

Wewe ni mwananchi wa kawaida ,Wenzako akina Bia yetu ,na Gussie ni insiders au wazee wa propaganda chamani ,Ccm ni kama maisha yao

Wewe mwezangu na mimi unajichosha tu,Hakuna anayekufahamu ccm

Fanya kazi mkuu,unaowatetea hawakufahamu hata sura
 
Back
Top Bottom