wagagagigi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2014
- 890
- 985
Umeongea ukweli mtupu mkuu.Charisma - compelling attractiveness or charm that can inspire devotion in others.
Kwa tafsiri ya kiswahili, Charisma ni ule mvuto mtu anaokuwa nao mpaka unatamani kama anaongea aendelee kuongea.
Katika siasa Charisma ni kitu cha umuhimu sana, kama huna Charisma, huwezi kuvutia watu wakakusikiliza.
CCM wana bahati mbaya sana kukosa viongozi wenye Charisma, ndo mana unaona kwenye kampeni wamekuwa wanatumia sana wasanii wa bongo fleva ili kuweka mvuto ambao ulistahili kuletwa na viongozi wao, kinyume chake ni sahihi kabisa, CHADEMA wana viongozi wenye Charisma ya hali ya juu sana, mtu kama Halima Mdee, Tundu Lissu, Mnyika, au Mbowe wakianza kuongea huwezi tamani ashushe mic, ni viongozi ambao wanaweza kuunganisha maneno mfululizo kwa lisaa lizima wakimwaga point ambazo hadhira inataka kuzisikia.
Nimemsikiliza leo Magufuli akiwa Shinyanga, honestly, unaona kabisa hata namna anavyounganisha sentensi, ni kama vile anakuwa anakosa coordination ya meneno. Magufuli anaweza kuongea sentensi kumi ambazo zinakinzana zenyewe kwa zenyewe, kitu ambacho kwa mtu unayemsikiliza ni rahisi sana kupoteza hamu ya kumsikiliza.
Ndo maana ya ule usemi wa kwamba, 'viongozi wanazaliwa' kama huna Charisma, huwezi kuongoza watu wakakupenda kwa sababu ni ngumu pia kwa mtu asiye na Charisma kuelewa changamoto za wengine. Ndo mana unamsikia Magufuli akituahidi tena kutumia mabilioni mengine ya kununua ndege, ni kama hajasikia na kuelewa vema kilio cha watanzania kwamba hizi ndege sio matumizi ya kipaumbele kwa taifa. Na hii ni moja wapo ya tabia za watu wasio na Charisma, daima hujali sana vipaumbele vyao dhidi ya wanaowazunguka.
Kama mambo yataendelea kwenda hivi, ni kwamba Magufuli ataonekana anaongea bila kuwa na hoja na mambo yanavoenda mvuto wa Magufuli kwa wapiga kura unazidi kupuputika, upande wa pili, Charisma inambeba Lissu kwa nguvu sana, wengine tulishakata tamaa na siasa lakini, namna Lissu anavofanya mambo mpaka sasa, ametuinua sana morali zetu, na hii yote ni nguvu ya Charisma aliyojaliwa ambayo wengine wamenyimwa.
Kitu chengine cha kuongezea ni jinsi audience wa Lissu wanavokuwa engaged anapoongea Lissu. Hawa watu ukiwaangalia unaona shauku yao ya kutaka kujua na kufahamu wanachoambiwa. Kwa ufupi wako very attentive na wenye shauku wa kusikia na kujuwa kila sentensi inayotoka mdomoni mwa Lissu.
Ama kwa upande wa Magu hali inakuwa ni tofauti kabisa. Utakuta watu hawako engaged kabisa na kinachoongewa. Wengina wanaongea, wengine wanafanya biashara na katika uwanja kila mmoja yuko na direction yake! Na wengine wakiwa na shauku ya kuwaona na kuwasikiliza wasanii.
Unaona kabisa kwamba watu wengi ndani ya hadhara za Magu kila mmoja kaendea lengo lake. Kwa tathmini ya haraka haraka unaweza kuona kwa asilimia 70 au zaidi hawana hamu na kinachoongewa na mgombea.