Uchaguzi 2020 'Charisma' ya Tundu Lissu itazidi kumpa shida sana Magufuli na CCM kwa ujumla

Uchaguzi 2020 'Charisma' ya Tundu Lissu itazidi kumpa shida sana Magufuli na CCM kwa ujumla

Mimi namwomba Mungu atende maajabu tu huku ,mkoloni mweusi inatosha aisee si kwa maumivu haya.
Mungu atusikie maana tukienda miaka mitano mingine kitakachotupata hakifurahishi.
Mkuu mimi nakwambia ukatili litaotutendea hili jitu hiyo miaka 5 ijayo ni Mungu tu ndie anajua! Nawaomba sana Watanzania wenzangu hii ndiyo golden chance yetu kumwadabisha! Let vote en masses tuone ataibaje hizo kura!
 
Mkuu nimekuelewa, nimekupata vizuri sana na Mungu akubariki uendelee kutoa hamasa huko uliko ingawa ID yako mkuu kwetu ni tusi sijui unatuachaje sasa? Shida yangu kwa Lissu itakuwa kujulikana kwake kule vijijini ambako watu wanalishwa matangopori eti wapinzani wataleta vita! Siasa za kipumbavu kabisa, halafu na tume nayo imekaa kimya tu! Nashauri chama kichspishe banners za picha ya Lissu na kila mgombea ubunge na udiwani apewe hiyo picha awe anazunguka nayo kwenye kampeni zake kama alivyofanya mzee Nyerere kwa Mkapa mwaka 1995. Watu vijijini hawamjui Lissu tutapigiwa huko!!
Hahahahaaa... Suala la ID linaniumiza kichwa sana, ila ntalishughulikia
 
Kiufupi tu ni kwamba jamaa hana charisma, na amekuwa anapata shida sana kujinadi kama mnavyojionea wenyewe. Ndiyo maana kampeni zake zimekuwa kutaja madege, meli, SGR na Stiegler's Gorge kana kwamba sisi tunakula hivyo vitu. Na kwa bahati mbaya sana hata wale wabunge 18 waliopita bila kuenguliwa (sio kupoingwa) hawana pia charisma ya kumsaidia boss wao.

Hii ni aibu kwa chama kikongwe kama CCM kukosa watu watu wa aina hiyo wakati iliwahi kuwa nao huko nyuma.
2015 alibebwa na mbeleko ya JK na Mkapa ambao walikuwa wapo vizuri
 
Naam , CHADEMA inatakiwa iweke mikutano mingi sana midogo midogo ngazi za kata na vijiji na wawe focused ni kijiji au kata ipi raia wake hawawajui wapinzani na faida zao iwapo wakipewa madaraka ili raia wafunguke bila hivyo huo ni upenyo wa ccm kuvukia
Huku mijini wanaeleweka hilo lipo wazi maana watu wa mijini ndiyo wanajua siasa na walichotendewa na utawala huu kwa miaka 5 (wanayo elimu ya uraia kwa upana zaidi)
Yaah kampeni zinatakiwa zijikite huko ndani ndani kabisa na ziambatane na elimu ya kupiga kura
 
Charisma ya Lissu ni kama ya marehemu Thomas Sankara, yani huyo alikuwa akiongea hata kama huelewi lugha unapata mzuka. Halafu wote wanafanana kwa kujali maendeleo ya watu.
CCM walete wanamuziki toka Nigeria na Marekani ndio fiesta yao itabamba. Otherwise jpm ataendelea kuwa gumzo kwa pumba atakazoongea , Lissu atakuwa gumzo kwa madini atakayotema.
Umepigilia msumari vizuri umenikumbusha, Sankara alikuwa moto sana nimeisoma historia yake
 
Lissu anashinda asubuhi sana na time lazima wamtangaze wakitaka vurugu mwaka huu basis wafanye hayo mambo zao
Tume wana hali ngumu sana huu mwaka, kujaribu kumbeba mtu asiyebebeka ni kazi ngumu sana, ingewezekana kwa mtu kama JK au Mkapa ila sio kwa Magufuli habebeki
 
Huwezi kuwa na maendeleo ya kudumu ya watu pasipo kwanza kuwa na msingi wa maendeleo ya vitu.

Mataifa makubwa yalianza kwa kujenga vitu miaka mingi iliyopita.

Wale black lives matter wanataka minara mingi ya wazungu maarufu ibomolewe kwa sababu ni watu waliofanya biashara ya watumwa waliofanya kazi ngumu ya kuyajenga maendeleo ya vitu, ambayo ndio msingi wa ubepari wenyewe.
Itakuwa unaongea hujui historia, hizi nchi za ulaya na marekani zilianza kuendelea kiuchumi baada ya kupiga hatua kwenye haki za binadamu.

Maendeleo ya watu siku zote ni kitu cha kwanza na cha msingi
 
Itakuwa unaongea hujui historia, hizi nchi za ulaya na marekani zilianza kuendelea kiuchumi baada ya kupiga hatua kwenye haki za binadamu.

Maendeleo ya watu siku zote ni kitu cha kwanza na cha msingi
Hujui unaloliongea. Wazungu wamekuja afrika kuchukua watumwa ili wakajenge viwanda na kulima.

Walishakuwa na makoloni kabla hata ya kufikiria demokrasia kwa tafsiri ya sasa.

Nenda kasome kwanza kabla ya kujadiliana na watu.
 
Hujui unaloliongea. Wazungu wamekuja afrika kuchukua watumwa ili wakajenge viwanda na kulima.

Walishakuwa na makoloni kabla hata ya kufikiria demokrasia kwa tafsiri ya sasa.

Nenda kasome kwanza kabla ya kujadiliana na watu.
Utakuwa unamis point kubwa sana, huwez fananisha moja kwa moja, enzi za utumwa na dunia ya sasa.

Kwahiyo unahalalisha utumwa dhidi ya maendeleo?

Hivi unafikiria vizur kweli?
 
kama kungekuwa na uchaguzi huru na wa haki, ndani ya sanduku la kura ccm kushinda labda kwa asilimia 51 sio zaidi ya hapo
 
Siyo charismatic, ila ni fundi wa kutukana. Na kwa maana hiyo kwenye siasa zetu za kiafrika hiyo inatafasiri ya fundi wa siasa.
 
Charisma ya Lissu ni kama ya marehemu Thomas Sankara, yani huyo alikuwa akiongea hata kama huelewi lugha unapata mzuka. Halafu wote wanafanana kwa kujali maendeleo ya watu.
CCM walete wanamuziki toka Nigeria na Marekani ndio fiesta yao itabamba. Otherwise jpm ataendelea kuwa gumzo kwa pumba atakazoongea , Lissu atakuwa gumzo kwa madini atakayotema.
This time mgombea tunaye aisee
 
Kwa sisi watu wataalamu wa Sayansi ya Siasa tunaposhuhudia mgombea wa Chama Kikubwa Kikongwe (Vanguard Party ..ya Kijamaa) anapelekeshwa hivi tunajua tuna kitu hakipo sawa!
Kwa hii miaka mitano mfumo wa Utawala ulifsnya jitihada kubwa ,nyingi za kuua CDM matokeo yake Ni kinyume! Je Nini kimesababisha haya!
Mosi,mabadiliko makubwa ya kifikra ,na hii inaashiria Watanzania wao tayari kwa mabadiliko.Kinachosekana Ni wakala wa kuongoza haya mabadiliko! Na Sasa yaelekea Tundu anajaribu kuziba ombwe hili! CCM walitakiwa wajiuluze Sana kwa yaliyotokea 2015! ,Ambapo almanusura watu wampeleke Lowasa Ikulu !
Lowasa angekuwa na uwezo wa kujenga hoja Kama Tundu sijui Hali ingekuwaje!?
Pili,Kuna tatizo kwenye mfumo wa Uongozi wa CCM . Pengine Mwenyekiti Hana washauri wazuri au hashauriki.
Sababu ya tatu Ni Mwenyekiti kushika hatamu! Tumexhuhudia miaka 5 ya Zidumu Fikra za Mwenyekiti! Mawaziri,Wabunge,Wakuu wa Idara na Taasisi ,RC,DC ,WEO,Madiwani wote wanamtukuza Mwenyekiti! Na Bahati mbaya sana hili linafanyika kinafiki.
Nne',Kosa kubwa wanalofanya CCM,ni kutumia nguvu kuwanyamazisga wapinzani.Leo hii nguvu kubwa ileile inatumika kunadi Sera ziluzotukuzwa kwa miaka mitano!
Tano,CCM wameshindwa kubaini kuwa kizazi kiaminifu' na Sera za Chama bila kujali chochote kinapotea kwa Kasi. Hawa walizaliwa ,wamekua na TANU,CCM na Nyerere huwaambii kitu!
Mwisho,CCM Ni muhimu wajiandae kuyapokea mabadilko makubwa Sana katika Fikra za Watanzania. Ni aibu na fedheha mtu mzima akitaka kuongea na wananchi kutumia nguvu kubwa namna hii ..wasanii na wachekeshaji!
Umewaambia ukweli wote.
 
Charisma - compelling attractiveness or charm that can inspire devotion in others.

Kwa tafsiri ya kiswahili, Charisma ni ule mvuto mtu anaokuwa nao mpaka unatamani kama anaongea aendelee kuongea.

Katika siasa Charisma ni kitu cha umuhimu sana, kama huna Charisma, huwezi kuvutia watu wakakusikiliza.

CCM wana bahati mbaya sana kukosa viongozi wenye Charisma, ndo mana unaona kwenye kampeni wamekuwa wanatumia sana wasanii wa bongo fleva ili kuweka mvuto ambao ulistahili kuletwa na viongozi wao, kinyume chake ni sahihi kabisa, CHADEMA wana viongozi wenye Charisma ya hali ya juu sana, mtu kama Halima Mdee, Tundu Lissu, Mnyika, au Mbowe wakianza kuongea huwezi tamani ashushe mic, ni viongozi ambao wanaweza kuunganisha maneno mfululizo kwa lisaa lizima wakimwaga point ambazo hadhira inataka kuzisikia.

Nimemsikiliza leo Magufuli akiwa Shinyanga, honestly, unaona kabisa hata namna anavyounganisha sentensi, ni kama vile anakuwa anakosa coordination ya meneno. Magufuli anaweza kuongea sentensi kumi ambazo zinakinzana zenyewe kwa zenyewe, kitu ambacho kwa mtu unayemsikiliza ni rahisi sana kupoteza hamu ya kumsikiliza.

Ndo maana ya ule usemi wa kwamba, 'viongozi wanazaliwa' kama huna Charisma, huwezi kuongoza watu wakakupenda kwa sababu ni ngumu pia kwa mtu asiye na Charisma kuelewa changamoto za wengine. Ndo mana unamsikia Magufuli akituahidi tena kutumia mabilioni mengine ya kununua ndege, ni kama hajasikia na kuelewa vema kilio cha watanzania kwamba hizi ndege sio matumizi ya kipaumbele kwa taifa. Na hii ni moja wapo ya tabia za watu wasio na Charisma, daima hujali sana vipaumbele vyao dhidi ya wanaowazunguka.

Kama mambo yataendelea kwenda hivi, ni kwamba Magufuli ataonekana anaongea bila kuwa na hoja na mambo yanavoenda mvuto wa Magufuli kwa wapiga kura unazidi kupuputika, upande wa pili, Charisma inambeba Lissu kwa nguvu sana, wengine tulishakata tamaa na siasa lakini, namna Lissu anavofanya mambo mpaka sasa, ametuinua sana morali zetu, na hii yote ni nguvu ya Charisma aliyojaliwa ambayo wengine wamenyimwa.
inahitaji uwe umekunywa valuu kumskiza JIWE, hamna mvuto zaidi ya kuanza na Stigla, ndege, Wanawake weupe,
 
Naam , CHADEMA inatakiwa iweke mikutano mingi sana midogo midogo ngazi za kata na vijiji na wawe focused ni kijiji au kata ipi raia wake hawawajui wapinzani na faida zao iwapo wakipewa madaraka ili raia wafunguke bila hivyo huo ni upenyo wa ccm kuvukia
Huku mijini wanaeleweka hilo lipo wazi maana watu wa mijini ndiyo wanajua siasa na walichotendewa na utawala huu kwa miaka 5 (wanayo elimu ya uraia kwa upana zaidi)

Upo sahihi... Watafanyia kazi ushauri wako...
 
Back
Top Bottom