Uchaguzi 2020 'Charisma' ya Tundu Lissu itazidi kumpa shida sana Magufuli na CCM kwa ujumla

Jamaa kilichobakia sasa, anatakiwa tu kusoma hotuba aliyoandikiwa na wasaidizi wake, na tena asome "word by word" na kwa utulivu na wala pasipo kuingiza vionjo vyake mwenyewe ama utani wowote ule.

Kwa maana hata akijaribu kufanya utani anajikuta anatumia maneno magumu ambayo hutuma ujumbe kwa walengwa kama anatoa kashfa. Akikwazika ama kuudhiwa hapo ndipo inageuka kuwa balaa nyingine, hasira zote zinakuwa ktk mafaili anayolala nayo chumbani kwake, hapo ndipo tumbua na teuzi zinapoanzia kwa wasaidizi wake.

Wewe ogopa mtu ambaye wasaidizi wake wengi wa karibu waliokuwa serikalini wamekimbia nyadhifa zao ili kutaka kwenda kutafuta unafuu wa "stresses" ktk ajira za mhimili wa bunge.
 
Lissu hatoshinda.,,
CCM walifanikiwa sana kuiba kura enzi ya Mkapa na Kikwete kwa sababu hao wawili walikuwa ni viongozi wenye Charisma na mvuto.

Huu mwaka itakuwa ngumu sana kwa Magufuli na CCM kufanya janja janja maana kwenye kampeni wanaenda kushindwa vibaya.

Kwa ufupi Lissu anachokifanya ni kuamsha hisia za nguvu ya umma, ndo maana bado nna imani huu mwaka chochote chaweza tokea
 
Huu mwaka naaamini utazaa matokeo tofauti, anything can happen. Mi huwa naamini hakuna kinachoshindikanaga hii dunia. Halafu pia udhaifu wa Magufuli ndio utawapa shida wataotaka kumpa ushindi wa mezani. Ni ngumu sana kumbeba asiyebebeka
 
Amen🙏
 
Charisma haikupeleki ikulu. Kuna kasiri ka muhimu sana kanakupeleka ikulu
Ingekuwa tunaamini sana hicho unachokiita siri, Africa ingekuwa bado inatawaliwa na wazungu.

Kilichotufanya Africa ikapata uhuru ni uhodari wa viongozi wazuri wenye Charisma kama kina Nyerere.

Kwahiyo sielewi kwanini una downplay nguvu ya Charisma.
 
Kiukweli upande wa upinzani tulikuwa tushakata tamaa mm nikiwa mmojawapo, lakini molari imekuja kupanda ghafla
Issue kubwa kwa sasa ni kuhakikisha kwanza tundu lissu anakaa midomoni pa watu.

Siku ya kura watanzania tukapige kura kwa wingi, then tuone sasa huo ushindi wa mezani unakujaje.

Huu mwaka ni wa kipekee sana, bado naamini
 
anakinzana balaa. juzi aliwadanganya watu wa ikungi eti anampenda lissu akakinzana na ile kauli ya siku ya ripoti ya makinikia kuhusu kazi za wanajeshi kule kwenye vita.

atuachie nchi yetu hafai. hana utu. muuaji wa demokrasia. siyo mstaarabu.
Maana yake magufuli anahubiri asichokiamini hata yeye. Ni muongo kupindukia.

Mtu anayepingana na kauli zake mwenyewe siwezi kumpa kura yangu. At least ntatembea kwa ufahari kwamba nafsi yangu ilishamkataa
 
Unajua huyu jamaa alijinadi sana (mtu wa press)kila siku saa hivyo watanzania ni kama walimzoea sana sasa hata asimame kwenye jukwaa la shaba ule mvuto haupo tena watu washamwona wa kawaida sana.
 
Mara nyingi jamaa akifanya utani lazima awaaibishe wanawake, sijui ni kwanini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…