Uchaguzi 2020 Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe

Uchaguzi 2020 Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe

Police hawawezi kusaidia mtu ambaye anawatukana anawakashfu, harafu akipigwa na wahuni wake anaowahamasisha wafanye vurugu mnawalilia tena police wawasaidie, iingieni sasa bara barani ! Simlisema kaagiza barabara zifungwe?
Huyo lissu wenu niwakupigwa na vijana tu wapenda amani nasiyo wakupigwa na police.

HAKUNA RAIS AMEWAHI KUZUIA WAPINZANI KUINGIA KIJIJINI KWAKE .........Aibu kubwa kabisa
 
Lissu ni vigumu kumshinda kwa hoja,njia pekee ya kumshinda ni kumpiga kwa risasi au mawe kama tulivyofanya Chato
 
Kulikuwa na ulazima wa kutumia risasi kwenye maandamano hayo..?
BEN SAANANE, AZORY wako wapi?

Tumia akili... Lissu alipigwa risasi kwa kosa gani?
hapakuwa na ulazima wa kutumia risasi lkn pia hapakuwa na ulazima kwa viongozi wetu wa chadema kuhamasisha maandamano yasiyo halali,
fahamu kuwa mimi sikubaliani na aina yoyote ya uvunjifu wa amani, wala siamini kuwa unaweza kudai haki kwa kuvunja haki za wengine......fuata utaratibu kudai haki....kama unaushahidi kilichotokea kuhusu saanane, azory na Lisu nenda kwenye vyombo utoe ushahidi ili hatua zichukuliwe.....usilalame pembeni au kufuata maneno ya kusikia...tumia akili yako kutafakari vuzuri.
 
angalia kifo cha mwanafunzi akwilina kilisababishwa na ujeuri wa wanasiasa...hatimaye mtu asiye na hatia akafa, je kama mwenyekiti asinge hamasisha maandamano ha lazima....kifo kinge tokea? hapana.

Hivyo mambo mengi wanasiasaa wanayafanya kwa kuwatoa muhanga wasio na hatia.....tunataka wawatangulize watoto zao mbele ya maandamano kama kweli wana uchungu wa kukomboa wananchi.


Watoto wao Kivipi wakati nimeshakuambia kuwa dunia hii kuna watu wameumbwa ili watetee maisha ya wengine.

Hivi nyie CCM madaraka ndio mnatoaga watoto wenu kwenda kupambana na majambazi au Magaidi?

Hivi vurugu zinatokana na Watu kupiga kura na kamapeni au zinatokana na dhuluma zinazofanywa na Wasimamizi ambao kiukweli wanapaswa kusimamia Haki.?

Hivi ni wapi ambapo hua hapatokei fujo haki inapokosekana.

Ni mpumbavu tu atakuunga mkono kwa sababu hujui gharama za watu wanaojitolea kwa ajili ya wengine ilivyokubwa.
Hata CCM wanawatangulia polisi ambao ni watoto wa maskini kwenda kuua watu na kupata maadaui huku wao wakinywa bia na kujilimbikizia mali . Haoa hao polisi akipewa rushwa ya buku mbili wanamfukuza kazi kama mbwa na kumtungia sheria ya kikokotoo. Hiyo ndiyo haki! Watu walioingia madarakani kwa rushwa na dhulma watawezaje kwenda kuongoza watu na kupinga rushwa ?
Nyie ndio mnaojiwaza tu matumbo yenu ndio maana hamjali hata ujai wa watu wengine alimradi mnapata kwa kupitia ujambaza kuuza madawa na mikataba mibovu . Nchi imejaa mikataba mibovu kwa sababu hamjali kuisoma kwa makini ili muifanyie marekebisho ,mnachoangalia ni 10% . Wabunge wa CCM hawataki uhuru wa Bunge na Bunge Live ili watete wengine. Wako pale kuangalia nafsi zao ili Mwenyekiti asije akawafukuza au kukata majina yao. Hiyo ndiyo dunia unayoitaka . Dunia ya watu wanaofanana na wanyama. Dunia ya watu ambao hata akipita na kuona Unaporwa au Kupigwa watu wakae kimya mana hayawahusu na hawawezi kuingilia kumsaidia mtu mana wanaweza wakaumizwa kwa kumtetea mwingine.
Mnataka dunia ambayo Polisi wakipigiwa siku kuwa kuna uhalifu waogope kwa sababu nao ni binadamu wanajali maisha yao na familia zao , na anayeibiwa ni mtu mwingine.

Kila unachokifurahia leo kuna watu waliumia kwa sababu hiyo.
Leo wakina Gwajima Kakobe na Wengine unaowaona wakiunga mkono fahari za Dunia na kukataa Haki na usawa kwa wanadamu huku wakihakasisha kuwa wengine ni wasaliti na hawapaswi kuishi ,wakesahau kuwa kuna waliopigania Haki ya kuabudu na uhuru wa kuabudu. Marehemu Moses kolola aliteswa sana alipoanza kuhubiri Ulokole Tanzania wakati wa Awamu ya kwanza na kuitwa mchochezi kwa sababu tu aliyakosoa makanisa makongwe na hayo ndiyo yaliyokuwa na matajiri wengi na watawala walisali huko. moses Kolola alijitoa kutetea kila anachokiamini mpaka alipokuja Mwinyi ambaye ni muislam lakini mwenye Utu na aliyeguswa na shida za wengine akaamua kuwa Kolola asibughudhiwe kwani ana uhuru wa kuamini anachoona kinafaa ,akasema Ruksa. Mwinyi akapigwa vita na wagandamizaji na waroho wa damu za watu wanaopenda kuona binadamu wenzao wakiteseka kwa umaskini na kukosa uhuru huku wao wakiwa na maisha safi.

Suala la Akwilina lilipaswa liwaguse wahusika wote.
Aliyepiga risasi binadamu mwenzake kwa sababu ya ukereketwa alipaswa awajibishwe.
Mkurugenzi aliyeacha kutimiza wajibu wake kwa haki alipaswa awajibishwe.
Mbowe aliyehamasisha maandamano bila kibali alipaswa naye awajibishwe. Hiyo ndiyo haki !! Damu ya Akwiline ,Damu ya Karume,Damu ya Dr.Sengondo Mvungi,Damu ya Alfonsi mawazo, Damu ya Wazanzibari wapatao 27 2001 , Damu ya Sokoine, Damu ya Horace Kolimba, Damu ya Azori Gwanda, Damu ya Ben Saanane iliyomwagwa kwa sababu tu ya misimamo yao na mawazo yao Hakika Mungu na asili ya Viumbe itajibu kwa vizazi vya wahusika.
 
hapakuwa na ulazima wa kutumia risasi lkn pia hapakuwa na ulazima kwa viongozi wetu wa chadema kuhamasisha maandamano yasiyo halali,
fahamu kuwa mimi sikubaliani na aina yoyote ya uvunjifu wa amani, wala siamini kuwa unaweza kudai haki kwa kuvunja haki za wengine......fuata utaratibu kudai haki....kama unaushahidi kilichotokea kuhusu saanane, azory na Lisu nenda kwenye vyombo utoe ushahidi ili hatua zichukuliwe.....usilalame pembeni au kufuata maneno ya kusikia...tumia akili yako kutafakari vuzuri.
Kumbe kipindi Aquilina anapigwa risasi we ulikuwepo na ulishuhudia wala hukuambiwa?
Ulipeleka ushahidi?

Maandamano ya kudai haki ni uvunjifu wa amani..?
Ila kupiga watu risasi, kuteka na kuua watu ni uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura sio?
 
Natamani kujua washambuliaji ni akina nani, wametumwa na nani na kwa maslahi gani, so far polisi wamechukua hatua gani?

Haya mambo yanaleta picha mbaya sana kwa ccm
Police walikuwa wanaangalia mapigano
 
Alitaka abembelezwe wakti anawzodoa kila siku?
Sasa wampende kwa lipi?

Kila siku chato chato,
Yeye anfikili chato wanaishi wanayama hawahitaji mandiliko,
Ajifunze kutumi domo lake vizuri.
mandiliko
 
Huko jimboni kwa Lissu watu wanampenda Magufuli ndio maana hawakumrushia mawe. Ukisema kwamba hawakumrushia kwasababu ya mamlaka yake, Basi angalau hata wangemzomea tu.

Kiukweli, ni ngumu Sana Lissu kukubalika Chato, Kama uliwahi kufika utakubaliana na mimi.Huyo mnaemuita jiwe ni kama mtemi wao, huwaambii kitu kabisa juu ya Magufuli, kwahiyo sishangai hivyo vitendo vilivyotokea huko(na wala haiwezi kuwa kikundi kilicho andaliwa)

Pamoja na hayo hiyo haimzuii mgombea wa chama pinzani kufanya kampeni zake Kama kweli democracy inazingatiw.Hivyo sheria unapaswa ichukue mkondo wake kwa wote waliofanya huo uvunjifu wa amani.
Umeongopa mkuu mkutano ulikuwa na nyomi na vijana kwa elfu 50 wanarusha mawe
 
Tangu 1995 wapinzani wanatuhumiwa kuwa waleta fujo, vita na vurugu lakini hakuna ushahidi wa kumpopo au kupopoana kutoka kwao kwanda ccm.

Haya ya chato nayo ni ya aina yake.
TANZANIA MPYA IYO
 
Wapinzani acheni kulia lia, juzi Kati hapa Magufuli alivamiwa na vijana wa Chadema kwenye kampeni huko Bukoba, Cha kushangaza viongozi wa Chadema ndo walikuwa wa Kwanza kushabikia hicho kitendo. Kama kweli mna nia njema mnatakiwa muwe wa Kwanza kukemea pale wanachama wenu wanapowafanyia viongozi au wanachama wa vyama vingine.
[emoji16]
 
Hakuna siku wana wa CHATO wamenifurahisha kama jana yaani wamesimamisha msafara kwa masaa kadhaa kwa kuupopoa na mawe .
 
Back
Top Bottom