Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Tukiwa na Taifa la watu kama wewe ni hatari sana.
Watawala ndio wanaotaka iwe hivyo lakini wao hawafanyi hivyo mana wanajua kuwa siasa ni sehemu ya maisha yao.
CCM wengi wanajali familia zao na maisha yao ndio kama unavyosema na ndio maana haya maovu yote yanatokea.
Ni wanyama tu ndio wanaojali maisha yao na watoto wao tu. Lakini Binadam anapaswa kujali maisha ya kila mmoja yawe ya haki. Ndio maana kuna wanajeshi wanaotoa maisha yao kwa ajili ya wengine waishi kwa amani na raha mustarehe. Mara nyingi hawa ni wale wanaotoka katika familia duni na wamekosa Fursa. Huwezi ukamkuta mtoto wa Waziri anakua Polisi au Mwalimu wa shule ya msingi au Sekondari ya Kata. Huwezi ukamuona mtoto wa Rais anakua Mgambo akalinde Geti la soko au la ushuru wa mazao.
Binafsi nawaheshimu sana watu wanaosimama upande wa maskini na upande Dhaifu. Hao ndio wanaopanda mbegu ya haki na mabadiliko tangu enzi za manabii.
Hivi unadhani Gwajima anaweza kugombea ubunge kupitia Chama cha upinzani wakati ni bilionea na ameshazoea maisha ya Raha.
Mara nyingi hua namtafakari JPM kuwa kama ni kweli ana uchungu na nchi hii mpaka anaona kuwa urais ni mzigo mkubwa je, ni kwa nini alishiriki katika maamuzi yote mabaya yaliyoliletea taifa hili hasara kubwa na kuibiwa tangu awamu ya Tatu?
Kwa nini hakuwahi kuipinga serikali na kuikosoa wazi wazi badala yake amekua akiitumia serikali kuwaumiza wananchi wakati akijua wazi kabisa kuwa Makosa yote yalisababishwa na serikali zilizopita. Mfano kuacha watu wajenge hovyo halafu anakuja anatumia dola kuwavunjia bila fidia .
Alipaswa akatae na kusema hawa ni watu wanyonge na maskini siwezi kuwavunjia bila kuwalipa fidia mana serikali ndiyo ilizembea watu wakawekeza fedha zao hapo. Hajawahi kusema wala kuumizwa na uonevu wa watu zaidi ya kuwaumiza . Nyumba za serikali ziliuzwa zote kwa makada wa CCM kwa bei ya kupeana huku wakijua wazi kuwa Tanzania ni nchi ya KIJAMAA lakini hakuwahi kupinga huo uporaji wa Mali za umma uliofanywa na wanaCCM kwa uroho wa kumiliki Mali zote za nchi hii.
Hakawahi kufanya kama alivyofanya Mrema alipoipinga serikali kwenye Kashafa ya Chavda na nyingine ,akaamua kuipinga serikali na akafukuzwa uwaziri kwa kusimamia Haki. Mrema alipata umaarufu wa kweli pamoja na kukosa Urais kutokana na kizingiti cha Mabilionea wanaomiliki Mali zote za nchi hii na vyeo vyote na familia zao. Mrema alikua ni mzalendo wa kweli mtetezi wa wanyonge mana alijitoa mhanga kupoteza madaraka ili asimamie haki.
Hawa wengine ni wazalendo wa kupigania maisha yao kama unavyoshauri ili wapate maisha mazuri.
Tumshukuru Mungu kwa kuwaleta duniani watu wasioangalia maisha yao binafsi. Ingekua wote wana roho za ubinafsi utumwa na ukoloni mpaka Leo ungekuwa upo Duniani . Afrika kusini imepata Uhuru kwa sababu ya vijana waliokua wamejitolea kupigania Haki.
CCM inaongozwa na mabilionea waliotumia Fursa ya Kujiita wajamaa na kupora Mali zote za umma kupitia madaraka.
Nyumba zote za Osterbay. Masaki, Upanga , Na maeno yote muhimu kwenye miji yote iliporwa na Makada wa CCM wakiopo na waliopita . Walishirikiana kujilimbikizia mali kupitia madaraka.
Watu kama hao ambao kwao uongozi ni biashara inayowatajirisha sana huku wakiwa wanaweza kufanya wanachotaka kwa MTU yeyote bila kuulizwa na MTU yeyote usipokua MTU mmoja tu ambaye ni Rais ,kwa maana kwamba akikaa kimya ndio basi; kamwe huwezi kushindana nao bila kuwa na watu wanaoweza kujitolea na kukabilana nao .
WanaCCM wengi wanaogonbea mpaka Udiwani ni wale wenye utajiri mkubwa , wanachofanya ni kumwaga pesa na kuandaa vijana ili wafanye vurugu hata kuua watu na wakija polisi kuchunguza wanawahonga mapesa ili taarifa zibadilishwe ionekane kuwa hakuna jambo baya lililofanywa na WanaCCM hao hivyo panakua hakuna Kesi.
Uroho wa Makada wa CCM umezalisha taifa la watu waovu wasiojali uhai wa MTU mwingine asiye na faida ya kimadaraka kweo.
Ditopile marehemu alipiga MTU risasi hadharani lakini kutokana na ukada wake wa CCM kesi ilibadilika na kuwa ndogo kabisa na kuachiwa. Mungu ndiye aliyeamua mwenyewe kama atakavyoendekea kuamua dhidi ya madhalimu..
Haki itasimama hata kama Viongozi wa dini wote watanunuliwa na kusema kuwa wao ndio wanaoamua ipi ni haki na ipi ni dhuluma. Yani kwa sasa viongozi wa dini hawajui kutofautisha kati ya haki na wajibu wa serikali kujenga miundo mbinu kwa kodi za watu. Kwao miundo mbinu ni kazi ya MTU anayejitolea na sio Kuwa na Bunge linalopanga kuwa Pale pajengwe daraja na likajengwa na Bajeti ikatilewa bila kutesa na kuuana kwa ushabiki.
Yaani kwa sasa mpaka viongozi wa dini wanaongea kwa kuuma meno utafikiri kuna mtu amechukua sadaka yao akainunulia sigara. Mchungaji anaongea kwa hasira kabisa na kwa chuki utafikiri Naye ni mgombea kama Gwajima . Eti tumchgue Huyu ni mchaMungu na yule ni msaliti . Wamesahau kuwa Yesu alikataa kupewa Fahari za dunia kwa kupinga kumsujudia Shetani. Viongozi wa dini wameonyeshwa fahari ya dunia na kumsuhudia CCM mkuu.
Hii ni post bora kabisa katika Uzi huu. Ni watu wachache sana wanaoweza kuwaza hivi, na kuweka mawazo yao vyema katika mtiririko huu.