Uchaguzi 2020 Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe

Uchaguzi 2020 Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe

Hujajibu lolote, mtu katoka katoro kapigwa jiwe chato akimshabikia chizi aliemtukana Mama magufuli.
Dawa itawaingia tu. Huwezi dharirisha wana chato then wakuache tu, mikutano yote kwanzia mbogwe amezõmewa. Haya akaseme kwa Robert.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo mnataka kujenga Taifa la watu wasioweza kuvuliana . Yani kila mtu akikerwa asifuate sheria aamue kuchukua upanga na kuwaua waliomuuzi.?
Aisee !! ndio agano jipya kati ya mungu wa ccm na wanachama wake.

Mtaliangamiza taifa hili kama ndivyo mnavyotaka iwe hivyo.
Hivi unajua ugaidi unaanzishwa na watu waliochoka kuteswa na bikadamu wenzao.
Yani CCM mnapewa kila kitu kwa kodi za wote halafu mnashindwa kuwa wavumilivu na kusimia sheria ? Ni jambo baya sana kudhani kuwa Kumsema mtu aliyepewa uongozi wa umma ni dhambi inayopaswa kuua mtu au kumjeruhi. Kwani wakimsema Magufuli aliyenufaika kwa kodi za wote kwa miaka zaidi ya 25 atapungukiwa nini.?
Na kwa Taarifa yako emponza sana Magufuli mana mngshauri aheshimu Demokrasia angeheshimika sana ndani na nje ya nchi. Uchaguzi huu angeshinda kwa kishindo na kwa raha na amani moyoni mwake. Hivi hata akishinda unategemea atakubali kustaafu akashtakiwe au kukosa heshima na upendo kwa Watu.?

Mbona viongozi wa CCM wameenda Zanzibar wakapokelewa vizuri japo kuna mashehe wanateswa na serikali ya CCM? Huo ndio uungwana na uvumilivu ambao viongozi wa umma wanapaswa kuwa nao.
 
Matusi ya Lisu kwa watu wa chato huwezi kuyaelewa mpaka uchukue akili zako ulizomkabidhi akushikie
Acheni kutudanganya kana kwamba nyie ndo mnajua kutafsiri Lugha za Matusi anazotumia Lissu kuna Lugha zilikuwa zinatumika mtaani Kuanzia 2015 Kama vile Tumekabidhi Nchi kwa Washamba nk kumbe ni sera ya Chadema kudhalilisha jamii fulani,Lissu azunguke Sana Kanda ya Ziwa sisi tulishampata Rais Magufuli tangu anazozunguka Ughaibuni kifupi anapoteza Muda hashindi.
 
Lissu hua anasema Nchi inaendeshwa kidikteta...Mara nyingine anasema MAGUFULI anajifanya mfalme je ni kweli anamaanisha ? Je ni kweli anaamini anachosema maana huwezi ukaenda stronghold ya mfalme ukapige kampeni labda iwe ndani ya nchi ya kidemokrasia sasa yeye anaamini MAGUFULI ni dikteta alafu wakati huohuo anaenda kufanya kampeni kwake ( kwa diktete kweli?)
Umejiuliza ni kwanini Maghufuli alifanya campaign Ikungi na kutoka salama ?!. Kwanini mpinzani wake asitafute kura Chato ?!. Na mbona kwingine mikutano ilikuwa salama isipokuwa Chato ?!.

Mnasema Amani huku mnashambulia watu kwa mawe ?!. Amani ya wapi !!
 
Acheni kutudanganya kana kwamba nyie ndo mnajua kutafsiri Lugha za Matusi anazotumia Lissu kuna Lugha zilikuwa zinatumika mtaani Kuanzia 2015 Kama vile Tumekabidhi Nchi kwa Washamba nk kumbe ni sera ya Chadema kudhalilisha jamii fulani,Lissu azunguke Sana Kanda ya Ziwa sisi tulishampata Rais Magufuli tangu anazozunguka Ughaibuni kifupi anapoteza Muda hashindi.
Kwa kura yako moja ?!
 
Kwenye hoja hata mgombea wao huwa anaogopa anakimbilia kutekana na kupiga watu risasi si bure ndio maana hataki kusikia neno mdahalo ataangamia
Alafu katika hotuba zake zote sijawahi kumsikia akiongelea au kukemea haya maswala ya utekaji, vijana wa CCM kufanya fujo katika misafara na mikutano ya Chadema meaning anabariki.
 
Tukiwa na Taifa la watu kama wewe ni hatari sana.

Watawala ndio wanaotaka iwe hivyo lakini wao hawafanyi hivyo mana wanajua kuwa siasa ni sehemu ya maisha yao.
CCM wengi wanajali familia zao na maisha yao ndio kama unavyosema na ndio maana haya maovu yote yanatokea.

Ni wanyama tu ndio wanaojali maisha yao na watoto wao tu. Lakini Binadam anapaswa kujali maisha ya kila mmoja yawe ya haki. Ndio maana kuna wanajeshi wanaotoa maisha yao kwa ajili ya wengine waishi kwa amani na raha mustarehe. Mara nyingi hawa ni wale wanaotoka katika familia duni na wamekosa Fursa. Huwezi ukamkuta mtoto wa Waziri anakua Polisi au Mwalimu wa shule ya msingi au Sekondari ya Kata. Huwezi ukamuona mtoto wa Rais anakua Mgambo akalinde Geti la soko au la ushuru wa mazao.

Binafsi nawaheshimu sana watu wanaosimama upande wa maskini na upande Dhaifu. Hao ndio wanaopanda mbegu ya haki na mabadiliko tangu enzi za manabii.

Hivi unadhani Gwajima anaweza kugombea ubunge kupitia Chama cha upinzani wakati ni bilionea na ameshazoea maisha ya Raha.
Mara nyingi hua namtafakari JPM kuwa kama ni kweli ana uchungu na nchi hii mpaka anaona kuwa urais ni mzigo mkubwa je, ni kwa nini alishiriki katika maamuzi yote mabaya yaliyoliletea taifa hili hasara kubwa na kuibiwa tangu awamu ya Tatu?

Kwa nini hakuwahi kuipinga serikali na kuikosoa wazi wazi badala yake amekua akiitumia serikali kuwaumiza wananchi wakati akijua wazi kabisa kuwa Makosa yote yalisababishwa na serikali zilizopita. Mfano kuacha watu wajenge hovyo halafu anakuja anatumia dola kuwavunjia bila fidia .

Alipaswa akatae na kusema hawa ni watu wanyonge na maskini siwezi kuwavunjia bila kuwalipa fidia mana serikali ndiyo ilizembea watu wakawekeza fedha zao hapo. Hajawahi kusema wala kuumizwa na uonevu wa watu zaidi ya kuwaumiza . Nyumba za serikali ziliuzwa zote kwa makada wa CCM kwa bei ya kupeana huku wakijua wazi kuwa Tanzania ni nchi ya KIJAMAA lakini hakuwahi kupinga huo uporaji wa Mali za umma uliofanywa na wanaCCM kwa uroho wa kumiliki Mali zote za nchi hii.

Hakawahi kufanya kama alivyofanya Mrema alipoipinga serikali kwenye Kashafa ya Chavda na nyingine ,akaamua kuipinga serikali na akafukuzwa uwaziri kwa kusimamia Haki. Mrema alipata umaarufu wa kweli pamoja na kukosa Urais kutokana na kizingiti cha Mabilionea wanaomiliki Mali zote za nchi hii na vyeo vyote na familia zao. Mrema alikua ni mzalendo wa kweli mtetezi wa wanyonge mana alijitoa mhanga kupoteza madaraka ili asimamie haki.

Hawa wengine ni wazalendo wa kupigania maisha yao kama unavyoshauri ili wapate maisha mazuri.

Tumshukuru Mungu kwa kuwaleta duniani watu wasioangalia maisha yao binafsi. Ingekua wote wana roho za ubinafsi utumwa na ukoloni mpaka Leo ungekuwa upo Duniani . Afrika kusini imepata Uhuru kwa sababu ya vijana waliokua wamejitolea kupigania Haki.

CCM inaongozwa na mabilionea waliotumia Fursa ya Kujiita wajamaa na kupora Mali zote za umma kupitia madaraka.
Nyumba zote za Osterbay. Masaki, Upanga , Na maeno yote muhimu kwenye miji yote iliporwa na Makada wa CCM wakiopo na waliopita . Walishirikiana kujilimbikizia mali kupitia madaraka.

Watu kama hao ambao kwao uongozi ni biashara inayowatajirisha sana huku wakiwa wanaweza kufanya wanachotaka kwa MTU yeyote bila kuulizwa na MTU yeyote usipokua MTU mmoja tu ambaye ni Rais ,kwa maana kwamba akikaa kimya ndio basi; kamwe huwezi kushindana nao bila kuwa na watu wanaoweza kujitolea na kukabilana nao .

WanaCCM wengi wanaogonbea mpaka Udiwani ni wale wenye utajiri mkubwa , wanachofanya ni kumwaga pesa na kuandaa vijana ili wafanye vurugu hata kuua watu na wakija polisi kuchunguza wanawahonga mapesa ili taarifa zibadilishwe ionekane kuwa hakuna jambo baya lililofanywa na WanaCCM hao hivyo panakua hakuna Kesi.

Uroho wa Makada wa CCM umezalisha taifa la watu waovu wasiojali uhai wa MTU mwingine asiye na faida ya kimadaraka kweo.
Ditopile marehemu alipiga MTU risasi hadharani lakini kutokana na ukada wake wa CCM kesi ilibadilika na kuwa ndogo kabisa na kuachiwa. Mungu ndiye aliyeamua mwenyewe kama atakavyoendekea kuamua dhidi ya madhalimu..

Haki itasimama hata kama Viongozi wa dini wote watanunuliwa na kusema kuwa wao ndio wanaoamua ipi ni haki na ipi ni dhuluma. Yani kwa sasa viongozi wa dini hawajui kutofautisha kati ya haki na wajibu wa serikali kujenga miundo mbinu kwa kodi za watu. Kwao miundo mbinu ni kazi ya MTU anayejitolea na sio Kuwa na Bunge linalopanga kuwa Pale pajengwe daraja na likajengwa na Bajeti ikatilewa bila kutesa na kuuana kwa ushabiki.

Yaani kwa sasa mpaka viongozi wa dini wanaongea kwa kuuma meno utafikiri kuna mtu amechukua sadaka yao akainunulia sigara. Mchungaji anaongea kwa hasira kabisa na kwa chuki utafikiri Naye ni mgombea kama Gwajima . Eti tumchgue Huyu ni mchaMungu na yule ni msaliti . Wamesahau kuwa Yesu alikataa kupewa Fahari za dunia kwa kupinga kumsujudia Shetani. Viongozi wa dini wameonyeshwa fahari ya dunia na kumsuhudia CCM mkuu.
Mkuu hii comment yako kwa heshima na taadhima nakuomba uifanye iwe uzi unaojitegemea kwani imeshiba na ina ujazo wote unaotosha kulisha ubongo wa msomaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye video ikionesha wana CCM wakirusha mawe atume hapa! Matukio ya kutengenezwa yamepitwa na wakati! Pia gari lililovunjwa silioni naona tu kama mtu kavunja mwenyewe tena na kajiwe kadogo hakutaka hasara kubwa!

Chadema ya Lisu acheni kutafuta kick za kipumbavu!! Tanzania ni nchi ya amani. Kila siku unawatukana wana Chato leo unawafata tena ni mara ya tatu unaenda kanda ya ziwa! Tanzania kubwa pambana na hali yako. Magufuli sio size yako!

Queen Esther
Eti anajidai kuwa amekuja kumsema kwao, na group alilotoka nalo geita na katoro ili ajaze chato.
Halafu viongozi wa dini wanamrambamramba miguu jpm.siwapendi wale viongozi wa dini hatarii
Mpende mwamakula na katimba kwani ni haki yako pia, yupo na bagonza.
Hao hawakutoshi?
 
Nyinyi huku chini hamuelewi kabisa yanayotokea,wanasiasa huwaaminisha vile wanavyotaka.Siasa ni somo pana sana,achilia mbali swala la kuishabikia kama baadhi ya watu wanavyofanya hapa Jf na huko uraiani😃,anaehusika nayo moja kwa moja, atakwambia.

Otherwise, nikutakie asubuhi njema kijana.

Yaani nimecheka kwa nguvu, halafu inaonekana ww utakuwa ni Mzee lazima, maana ndio huwa wanatumiaga maneno kama haya ya kwako. Yaani watu tuone mtu katekwa kabisa uniambie siasa ni somo pana sana! Mimi nazungumzia uhalisia wa siasa, ww unaniletea habari ulizokaririshwa kwenye chuo cha siasa hapo kivukoni. Kaa Kimya tu maana huna jipya.
 
angalia kifo cha mwanafunzi akwilina kilisababishwa na ujeuri wa wanasiasa...hatimaye mtu asiye na hatia akafa, je kama mwenyekiti asinge hamasisha maandamano ha lazima....kifo kinge tokea? hapana.

Hivyo mambo mengi wanasiasaa wanayafanya kwa kuwatoa muhanga wasio na hatia.....tunataka wawatangulize watoto zao mbele ya maandamano kama kweli wana uchungu wa kukomboa wananchi.
Mbowe ndiye aliyewaambia askari wamuue Akwilina ?
Hivi wenzetu mnatumia ubongo upi kufikiria ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umejiuliza ni kwanini Maghufuli alifanya campaign Ikungi na kutoka salama ?!. Kwanini mpinzani wake asitafute kura Chato ?!. Na mbona kwingine mikutano ilikuwa salama isipokuwa Chato ?!.

Mnasema Amani huku mnashambulia watu kwa mawe ?!. Amani ya wapi !!
Chadema mnatengeneza movie za kihindi Tunataka Amani hatutaki vita
 
Back
Top Bottom